Welcome to Ugfacts.net/ke. On this page you will find details on the following topics

KUCCPS Admission Letters KUCCPS Student Portal KUCCPS Admission Lists
FREE KNEC KCSE Past Papers FREE KNEC KCPE Past Papers List of All Past Papers 
Fees Structure for 2024-2025 KNEC KCPE KNEC KCSE
Intakes and Admissions 2024-2025 List of Courses Offered Latest Jobs in Kenya 2024-2025
TVET Applications 2024-2025 TSC KNUT
KDF Recruitment Kenya Police Recruitment Kenya Prisons Service Recruitment

Your Opinions and Questions Matter. Kindly leave your comments below and we shall attend to you promptly.

KNEC KCSE Kiswahili Paper 2 – 2014 Cross Country Mock

KNEC KCSE Kiswahili Paper 2 – 2014 Cross Country Mock

2014 Cross Country Mock

Kiswahili Paper 2

1. UFAHAMU (Alama 15)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

1.

Wakati wananchi katika kila pembe ya dunia waliadhimisha siku ya wapendanao maarufu kama Valentine Day, kwa mitindo mbalimbali, hali hiyo ilikuwa tofauti kwa baadhi ya wanaume nchini Kenya, baada ya kulalamikakuhusu kunyanyaswa na wake zao.

Kulingana na Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Haki za Wanaume nchini, idadi ya wanaume wanaopigwa nawake zao imeongezeka mno. Alisema juzi kuwa utafiti wa chama chake umeonyesha kuwa harakati za kumpa uwezo mwanamke zimeathiri maadili na kuwasababisha kuwadharau wanaume. Mwanaharakati huyo anadai kuwa tatizo hilo limechochewa zaidi na hali ya kuwa wanawake wengi sas wana kipato kikubwa kuliko waume zao.

Mwishoni mwa wiki Polisi walimtia mbaroni mwanamke mmoja mjini Nyeri mkoani kati, baada ya
kumshambulia mumewe na kumjeruhi vibaya kwa panga. Mwanamume huyo bado anapata matibabu
hospitalini. Yeye alirudi nyumbani kama amevaa miwani ndipo akakatwa katwa usoni na uchunguzi kuhusu tukio hilo bado unaendelea.

Inadaiwa kuwa zaidi ya wanaume 460,000 walinyanyaswa na wake zao mwaka jana na kwamba utafiti wa shirika la kuwatetea wanaume unaonyesha kesi nyingi za wanaume kuteswa na wake zao zinaripotiwa katika Mkoa wa kati.

Hata hivyo, baadhi ya wanaume katika eneo hilo wameunga mkono hatua ya wanawake kuwashambulia waume zao. Wanasema kuwa, wanapigwa kwa sababu wamekosa kuwajibika kwa familia zao. Wanadai kuwa wanaume wengine hawajulikani nyumbani kwao. Wake zao wanawajua makasisi ambao huja kuwaombea kuhusu matatizo ya nyumbani huku mbwana zao wakizama katika ulevi. Wanawake na wanaume wa Nyeri wametak serikali ikomeshe uuzaji na unywaji pombe haramu ambayo imechangia sana ugomvi wa kinyumbani.

Maswali
(a) Upe ufahamu huu anwani mwafaka. (alama 1)


(b) Eleza sababu za wanaume kupigwa katika ndoa. (alama 4)

(c) Mwandishi anamaanisha nini anaposema kuwa wanaume wengine hawajulikani nyumbani kwao.(alama 2)(d) Fafanua majukumu ya makasisi katika jamii kwa mujibu wa kifungu hiki. (alama 2)(e) Eleza mabadiliko katika asasi ya ndoa kwa mujibu wa kifungu hiki. (alama 3)
(f) Eleza maana ya vifungu hivi kama vilivyotumika katika tungo. (alama 3)

(i) Mwanaharakati

(ii) Amevaa miwani

(iii) Waliadhimisha

 15 marks

2. UFUPISHO (Alama 15)

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali

2.

Hali ya usafiri nchini imeimarika si haba baada ya Wizara ya Uchukuzi kutoa sheria mpya kuhusiana na magari ya abiria. Tangu kutolewa kaw sheria hii, ajali za barabara zimepungua kwa ailimia kubwa. Visa vya magari ambayo yalikuwa yakianza safari na hayakudiriki kufika kwenye vituo vyake vimepungua na nidhamu ya wafanyikazi katika matwana za kubeba abiria imeimarika si haba.

Mikanda ya usalama imesaidia mno kusalimisha maisha ya abiria wakati wowote patokeapo ajali. Polisi wa barabarani wamekuwa macho kuwasaka wanaohalifu amri ya kujifunga mkanda wa usalama. Abiria wengi ambao wamezoea kupuuza kila mara wamejikuta wamebururwa hadi vituo vya polisi na baadaye mahakamani kutozwa faini. Wale ambao wamezoea ule mchezo wa Toa kitu kidogo hujaribu kuwapenyezeasharubati askari hawa. Ole wao, ikiwa watakumbana na askari mwadilifu watakunywa shubiri maradufu!

Siku za kisogoni ungekutana na mabasi ambayo yalikuwa yameshiba abiria yakatapika. Baadhi ya abiria ambao daima walikuwa kwenye mbio za kifika walikokuwa wakienda, walijining’iniza kama kima kwenye mapaa na mbavu za mabasi. Wengine walijiangukia kama magunia ya mchele na kujivinjikia viungo vyao. Waliosalimika walijishukuru kwa uangalifu wao na kuendelea na hulka yao ya kuchezea tope. Siku hizi, tabia hii ya kuyasheheneza magari kupindukia imesahaulika kabisa. Wale wanaojaribu kubeba abiria wengi kupita kiasi huzomewa na abiria wengine na kuaibika. Kila mtu sasa yu macho kuhakikisha kwamba usalama barabarani umedumishwa.

Vidhibiti mwendo vimechangia pakubwa kupunguza idadi ya ajali barabarani. Siku hizi, hakuna gari la abiria ambalo linapaswa kuendeshwa kwa kasi ya zaidi ya kilomita themanini kwa saa. Jambo hili limewafanya madereva kuweza kuyadhibiti magari yao vyema itokeapo kuwa kutatokea gari lingine kwa ghafla upande ule mwingine. Madereva ambao huzidisha kasi iliyopendekezwa hutozwa faini.

Udereva sasa umekuwa kazi yenye haiba na hadhi zaidi kuliko hapo awali. Madereva na utingo hujitambulisha kwa kuvaa sare nadhifu. Aidha, wameajiriwa kwa masharti Fulani ambayo mwajiri na dereva mwenyewe sharti azingatie. Jambo hili limewakinga madereva na utingo dhidi ya unyanyasaji wa matajiri wao.

Ni kweli kuwa hali ya usafiri imekuwa bora zaidi na vifo kutokana na ajali vimepungua. Hata hivyo, pana haja ya hali ya barabara kuimarishwa zaidi. Baadhi ya barabara zina mashimo ambayo mara nyingine huwafanya madereva kugongana na magari mengine wanapojaribu kuyahepa mashimo haya. Aidha, baadhi ya madereva hawawi waangalifu sana barabarani. Hukiuka sheria za barabarani na kusababisha ajali. Madereva wengine wameanza kuvitengeneza vidhibiti mwendo upya ili kuzidhisha kasi ya magari yao, hali ambayo imeanza kuongeza ajali za barabarani. Madereva wengine huendesha magari huku wakiwa wamelewa chakari. Jambo hili huwanya kuendesha ovyo barabarani na wakati mwingine kusababisha ajali. Ni muhimu kuhakikisha kwamba madereva wanaokiuka sheria mpya za barabarani wametiwa mbaroni, la sivyo nchi hii itarudia yale maradhi ya awali. Waendeshaji magari ya kibinafsi pia hawana budi kuwa waangalifu kwani wao ndio husababisha baadhi ya ajali.

Maswali
(a) Fupisha aya mbili za kwanza. Tumia maneno 50-55 (alama 6)

MtayarishoJibu(b) Ni nini maoni ya mwandishi kuhusu suluhisho la kudumu kwa ajali za barabarani. Tumia maneno 40-50.(alama 9)

Mtayarisho


Jibu 15 marks

3. SARUFI (Alama 40)

Jibu maswali yoke.

3.

Kwa kutoa mifano, tofautisha ala sogezi na ala tuli.

 1 marks

4.

Taja vipasho vyote vya lugha.

 2 marks

5.

Ainisha maneno tofauti katika sentensi ifuatayo:
Wenye baiskeli wamo hatarini ………………………………………………………

 2 marks

6.

Tofautisha sauti

/z/ …………………………………………………….

/sh/ …………………………………………………….

 2 marks

7.

Tunga sentensi ukitumia kitenzi hiki katika kauli ya kutendesha:
Cha (kupambazuka)

 2 marks

8.

Tunga sentensi moja moja kuonyesha matumizi ya alama hizi za uakifishaji:
(i) Parandesi …

(ii) Kistari kifupi

 2 marks

9.

Sahihisha sentensi hii:
Yule mama amewai leta mandizi toza

 2 marks

10.

Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii:
Nguo yake imeshoneka

 2 marks

11.

Ukitumia mifano mwafaka, dhihirisha matumizi mawili ya neno ‘kwa’.

 2 marks

12.

Changanua sentensi hii kwa njia ya matawi.
Atakayefikishwa hapa ni mgeni

 4 marks

13.

Unda kitenzi kimoja kutokana na neno jasiri

 1 marks

14.

Tunga sentensi mbili sahihi ili kubainisha maana mbili za kiambishi – ndi -.

 2 marks

15.

Andika kifungu hiki katika usemi halisi:
Mzazi alimwambia mtoto wake kuwa isingekuwa juhudi zake masomoni hangeibuka bora kitaifa.

 3 marks

16.

Eleza kazi ya kihisishi katika sentensi hii.
Kefule! Tangu lini mzazi akamlaani mwanawe?

 1 marks

17.

Bainisha mofimu katika neno: Alipogongewa

 3 marks

18.

Kanusha sentensi hii kwa wingi katika hali ya kuamrisha.
(i) Geuka polepole ………………

(ii) Kula …………………………………

 3 marks

19.

Tofautisha sentensi hizi:
(i) Ningefanya kazi ningepata mali
(ii) Ningalifanya kazi ningalipata mali

 2 marks

20.

Onyesha kiima na chagizo katika sentensi hii:
Mkulima alimfungia ng’ombe kamba

 2 marks

21.

Tunga sentensi moja ili kudhihirisha matumizi ya ngeli ya KU-KU.

 1 marks

4. ISIMU JAMII (Alama 10)

Soma mazungumzo haya kisha ujibu maswali.

22.

Kamau: Karibu kastoma.
Chebet: (Akisogea karibu) Asante.
Kamau: Hii ni mia tano, mia tatu nah ii mia.
Chebet: Kwani hakuna ys shilingi kumi?
Kamau: Hei! Wewe huoni dollar imepanda na pia petrol imepanda.
(1) Tambua sajili hii na utoe idhibati. (alama 2)

(2) Taja na kueleza sifa nne za mazungumzo haya. (alama 8)

 10 marks

Leave a Comment