Welcome to Ugfacts.net/ke. On this page you will find details on the following topics

KUCCPS Admission Letters KUCCPS Student Portal KUCCPS Admission Lists
FREE KNEC KCSE Past Papers FREE KNEC KCPE Past Papers List of All Past Papers 
Fees Structure for 2024-2025 KNEC KCPE KNEC KCSE
Intakes and Admissions 2024-2025 List of Courses Offered Latest Jobs in Kenya 2024-2025
TVET Applications 2024-2025 TSC KNUT
KDF Recruitment Kenya Police Recruitment Kenya Prisons Service Recruitment

Your Opinions and Questions Matter. Kindly leave your comments below and we shall attend to you promptly.

KNEC KCSE Kiswahili Paper 3 – 2014 Homa-Bay Mock

KNEC KCSE Kiswahili Paper 3 – 2014 Homa-Bay Mock

2014 Homa-Bay Mock

Kiswahili Paper 3

SEHEMU YA A (Alama 20)

FASIHI SIMULIZI Swali Ya Lazima

1.

(a)Maigizo ni nini? (al.2)
(b) Taja vipera vyovyote viwili vya maigizo (al.10)
(c) Eleza dhima zozote tano za maigizo (al.10)
(d) Jadili njia zinazotumiwa na kizazi cha sasa kuendeleza utanzu huu. (al.6)

 20 marks

SEHEMU YA B (Alama 20)

RIWAYA : KIDAGAA KIMEMWOZEA : Ken Walibora

2.

“Nilikwambia twende ukakataa……si kuona, tuone ndipo tuambe”
(a) Weka dondoo katika muktadha wake (al.4)
(b) Fafanua hulka za mswemewa (al.6)
(c) Taja tamadhali ilitumika katika dondoo (al.2)
(d) Eleza umuhimu wa yanayorejelewa (al.4)
(e) Jadili umuhimu wa msomaji (al.4)

 20 marks

3.

“Nchi ya Tomoko imejawa na uozo” tetea kauli hii kwa mujibu wa riwaya ya kidagaa
kimemwozea

 20 marks

SEHEMU YA C (Alama 20)

TAMTHILIA: MSTAHIKI MEYA

4.

Fafanua mbinu walizotumia wanacheneo kujikomboa

 20 marks

5.

“…kina raha gani watoto wetu wanapofukuzwa shule kwa sababu hatuwezi kuwalipia karo?
kuna raha gani……………….
(a) Weka dondoo katika muktadha wake (al.4)
(b) Eleza sifa za msemewa (al.4)
(c) Jadili umuhimu wa msemaji (al.2)
(d) Dondoo limetumiwa tamathali zipi? (al.4)
(e) Wanacheneo wamezonga na matatizo mengi tetea kauli hii kulingana na tamthilia (al.6)

 20 marks

SEHEMU YA D (Alama 20)

HADITHI FUPI: DAMU NYEUSI (Ken Walibora S. Mohamud)

6.

Jadili maswala ibuka ukirejelea visa viNne kutoka kwa hadithi zifuatazo.
(i) Mke wangu
(ii) Samaki wa nchi za joto
(iii) Damu nyeusi
(iv) Gilasi ya mwisho makaburini

 20 marks

7.

“…….Nani kakwambia kwamba mimi unanihusudu”
(a) Weka dondoo katika muktadha wake (al.4)
(b) Ni nini dhamira ya kisa kinachotajwa? (al.2)
(c) Kisa kinachorejewa kinaakisi jamii ya kisasa. Tetea (al.10)
(d) Msanii Mohamed Ghassanyamefanikiwa kutumia kinaya. Tetea kwa mifano minne (al.4)

 20 marks

SEHEMU YA E (Alama 20)

USHAIRI

8.

VITA VYA NDIMI
Huyo !Amshike huyo !
Hakuna bunduki wala kifami
Bomu na risasi hata hawazijui
Lakini mno wanashambuliana
Kwa ndiMi zilizonolewa kwa makali
Vipande vya matusi silaha zao
Yu imara mmoja wao
Akirusha kombora la nenO zito!
Linitingishe adui wake
Na kumgusa hisia kwa pigo kuu
Pigo linalochoma moyoni kama kichomi
Kuchipuza joto la hasira na kisasi
Katika mapigano yaso na kikomo
Filimbi ya suluhu inapulizwa kuwaamua!
Ni nai anayekubali suluhu?
Roho zinakataa katakata
Huku ukaidi ukinyemelea na kutawala kote
Mapandikizi ya watu yakipigana
Vita shadidi visivyo ukomo
Vita vya ndimi!
Magharibi sasa
Jua linapungia mkono machweo
Nalo giza likinyemelea kwa kiburi na
Kasi
Sisikii tena sauti za mIsonyo
Mate ya watesi yamekauka
Makanwa yao yamelemewa na uchovu
Sasa wameshikana mikono
Ishara ya suluhu

Maswali
(a)Hili ni shairi la aina gani? (al.1)
(b) Eleza dhamira ya mshairi (al.2)
(c) Eleza siFa za utunzi alizotumia mshairi (al.3)
(d) Taja tamathali zozote tatu alizotumia mshairi (al.3)
(e) Eleza toni ya mshairi katika beti tatu za awali (al.1)
(f) Eleza hatima ya yanayozungumziwa kwenye shairi (al.1)
(g) Mshairi ametumia alama hisi kwingi. Eleza umuhimu wake (a.1)
(h) Itambue nafsi neni katika shairi (al.1)
(i) Andika mishororo ya kwanza mitatu ubeti wa 4 kwa lugha ya nathari (a.3)
(j) Toa maana ya msamiati huu (al.2)
(i) Kombora
(ii) Misonyo

 20 marks

9.

Ndege mwema na muruwa, katu haishi tunduni
Hataki kufadhiliwa, muda yumo utumwani
Japo mnyonyoe mbawa, mwisho wake utahuni
Ndege kuishi tunduni, ni nguvu amezidiwa
Ndege ataka yoyoma, nasiyahi msituni
Apite akisimama, shinani na mitawini
Haridhiki kwa mtama, na maji ya kikombeni
Ndege kuishi tunduni, ni nguvu amezidiwa
Ndege mwema wa hishima mwema mno wa kughani
Tundu huliona chama, japo liwe la thamani
Huporomosha yakwe kima, na kufanya faraghani
Ndege kuishi tunduni, ni nguvu amezidiwa
Ndege mpambe kwa zari, na lulu na marijani
Upambe yake suduri, kwa almasi kidani
Tunduni atahajiri, ili awe huriani
Ndege kuishi tunduni, ni nguvu amezidiwa
Ndege mwema wa busara, hatoishi kifungoni
Anayo kubwa hasara, kukosa nyumba ya mani
Lamkera lamkera, tundu la dhahabu kwani
Ndege kuishi tunduni, ni nguvu amezidiwa
Ndege maumbile yake, na waja hayalingani
Yeye hutaka wenzake wafukuzane hewani
Jambo la kuishi pweke, kamwe humridhiani
Ndege kuishi tunduni, ni nguvu amezidiwa
Baiti zangu ni haba, nakonea kituoni
Ndege huficha mahaba, kama yumo kifungoni
Hali ndege akashaba, kwani yumo adhabuni
Ndege kuishi tunduni, ni nguvu amezidiwa

Maswali
(a) Lipe shairi anwani mwafaka (al.1)
(b) Fumbua maana ya ndege anayerejelewa (al.1)
(c) Shairi hili ni la mkondo gani? (al.3)
(d) Eleza muundo wa ubeti wa nne (al.3)
(e) Fafanua uhuru aliotumia mshairi (al.4)
(f) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari (al.4)
(g) Jadili dhamira ya mshairi (al.2)
(h) Fafanua maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa na mshairi (al.2)

 20 marks

Leave a Comment