Welcome to Ugfacts.net/ke. On this page you will find details on the following topics

KUCCPS Admission Letters KUCCPS Student Portal KUCCPS Admission Lists
FREE KNEC KCSE Past Papers FREE KNEC KCPE Past Papers List of All Past Papers 
Fees Structure for 2024-2025 KNEC KCPE KNEC KCSE
Intakes and Admissions 2024-2025 List of Courses Offered Latest Jobs in Kenya 2024-2025
TVET Applications 2024-2025 TSC KNUT
KDF Recruitment Kenya Police Recruitment Kenya Prisons Service Recruitment

Your Opinions and Questions Matter. Kindly leave your comments below and we shall attend to you promptly.

KNEC KCSE Kiswahili Paper 3 Question Paper / 2015 KCSE Kirinyaga West

KNEC KCSE Kiswahili Paper 3 Question Paper / 2015 KCSE Kirinyaga West

2015 KCSE Kirinyaga West

Kiswahili Paper 3

SEHEMU A (Alama 20)

Swali la lazima Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo

1.

1. Ningali kinda nishike, viungo vi teketeke,
Sinipe simi nizuke, na vichaka nivifyeke,
Dhibiti nivuvumke, usidiriki makekeke,
Pulika usikiuke, mpe mtoto hakiye,

2. Mungavunja haki yake, madhara milele kwake,
Wa kiume na wa kike, mpeni yaliyo yake,
Kwa makini mumshike, kadiri makamo yake,
Pulika msikiuke mpe watoto haki yake.

3. Kwanza ni watani wake, Uandae aridhike,
Atuze mtima wake, maudhi yasimshike,
Kuta nne zizunguke, na hofu imbanduke,
Pulika msikiuke, mpe mtoto haki yake.

4. Pili ni chakula chake, ‘jengeke siha yake,
Mpe titi alishike, anyonye asihinike,
Kuta nne zizunguke, na hofu imbanduke,
Pulika msikiuke, mpe mtoto haki yake.

5. Mpe tiba ‘sidhurike, ndwele asiathirike,
Fikira zimpanuke, atambue rika lake,
Penye daraja avuke, mvushe asighurike,
Pulika msikiuke, mpe mtoto haki yake.

6. Angakuwa chekecheke, apande shule avuke,
Mpe taaluma yake, adhibiti apanuke,
Ufundi na dhima zake, ayashike ajivike,
Pulika msikiuke, mpe mtoto hakiye.

7. Jifanye kipenzi chake, mpende asihinike,
Amani ijae kwake, daima asikereke,
Vizito usimtwike, visivyo vipimo vyake,
Pulika msikiuke, mpe mtoto hakiye.

8. Elimu chuo ashike, apanuke bongo lake,
Atende jukumu lake, ahudumie wenzake,
Ajue wajibu wake, atende asitepweke,
Pulika msikiuke, mpe mtoto hakiye.

9. Hima kwa Muumba wake, muhimidi aongoke,
Roho yake isafike, ahera asisumbuke,
Neema imzunguke, maovu yamuepuke,
Pulika msikiuke, mpe mtoto hakiye.

Maswali
a) Nafsi neni ametaja haki zinazomstahiki mtoto. Zitaje na uzifafanue. (alama 4)
b) Eleza kwa kutoa mifano mbinu mbili zinazotumiwa na mshairi kutosheleza mahitaji ya kiarudhi
c) Bainisha umuhimu wa tamathali zozote mbili za usemi zilizotumika katika shairi hili (alama 4)
d) Eleza ubeti wa tano kwa lugha nathari (alama 4)
e) Taja na ufafanue toni ya mshairi (alama 2)

f) Eleza maana ya misamiati ifuatayo (alama 2)
i) Mtima
ii) Asihinike
iii) mbi
iv) asighurike

 20 marks

SEHEMU B (Alama 20)

TAMTHILIA: Timothy Arege: Mstahiki Meya Jibu swali la 2 au 3

2.

“Mtu huvuna alichopanda. Ukipanda pojo huweza kuvuna kunaziu”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Thibitisha kuwa warejelewa walikuwa wamepanda pojo (alama 10)
c) Eleza sifa za mnenewa (alama 6)

 20 marks

3.

Tamthilia ya Mstahiki Meya inamulika na kupiga vita utawala dhalimu katika mataifa ya kiafrika. Jadili

 20 marks

SEHEMU C (Alama 20)

RIWAYA: Ken Walibora: Kidagaa Kimemwozea Jibu swali 4 au 5

4.

“Aliwaonea gere wanawake wengine katika eneo la Sokomoko waliovaa rinda moja………..”
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake (alama 4)
b) Eleza sifa na umuhimu wa anayemfanya mrejelewa kuwaonea wanawake wengine gere (alama 10)
c) Jadili maudhui matatu yanayodokezwa katika dondoo hili (alama 6)

 20 marks

5.

“Mla naye huliwa zamu yake ifikapo.”
Thibitisha kauli hii kwa kuirejelea riwaya ya kidagaa kimemwozea.

 20 marks

6.

Onyesha jinsi swala la ubaguzi linavyodhihirika katika hadithi zozote nne.

 20 marks

SEHEMU D (Alama 20)

HADITHI FUPI: Ken Walibora : Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine Jibu swali la 6 au 7

7.

“Hawakurudhisha macho tu, bali pia walicheza michezo ya ujana ama wakijua au kutojua kuwa ujana una tegemeo.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Dhihirisha namna ‘Michezo ya ujana’ ya wanaorejelewa ilivyosambaratisha tegemeo la ujana wao. (alama 8)
c) Jadili ukweli wa kauli kwamba, “Tamaa mbele mauti nyuma” ukirejelea hadithi ya “Tazamana na mauti”(alama 8)

 20 marks

SEHEMU E (Alama 20)

FASIHI SIMULIZI

8.

a) Eleza sifa nne za ushairi simulizi (alama 8)
b) Taja na uelezee aina tatu za magizo (alama 6)
c) Jadili mbinu nne za kimtindo za methali huku ukitoa mifano mwafaka (alama 4)
d) Eleza umuhimu wa hekaya katika jamii (alama 4)

 20 marks

Leave a Comment