Welcome to Ugfacts.net/ke. On this page you will find details on the following topics

KUCCPS Admission Letters KUCCPS Student Portal KUCCPS Admission Lists
FREE KNEC KCSE Past Papers FREE KNEC KCPE Past Papers List of All Past Papers 
Fees Structure for 2024-2025 KNEC KCPE KNEC KCSE
Intakes and Admissions 2024-2025 List of Courses Offered Latest Jobs in Kenya 2024-2025
TVET Applications 2024-2025 TSC KNUT
KDF Recruitment Kenya Police Recruitment Kenya Prisons Service Recruitment

Your Opinions and Questions Matter. Kindly leave your comments below and we shall attend to you promptly.

KNEC KCSE Kiswahili Paper 3 Question Paper / 2016 KCSE KAMDARA JET Examination

KNEC KCSE Kiswahili Paper 3 Question Paper / 2016 KCSE KAMDARA JET Examination

2016 KCSE KAMDARA JET Examination

Kiswahili Paper 3

SEHEMU YA A (Alama 20)

USHAIRI: Swali la lazima

1.

ULIYATAKA MWENYEWE: D.P.B Massamba
Alikwamba wako mama, kajifanya hupuliki,
Kakuasa kila jema, ukawa ng’oo! hutaki,
Sasa yamekusakama, popote hapashikiki,
Uliyataka mwenyewe!

Babayo lipokuonya, ukamwona ana chuki,
Mambo ukaboronganya, kujifanya hushindiki,
Sasa yamekunganya, kwa yeyote hupendeki,
Uliyataka mwenyewe!

Mazuri uliodhania, yamekuletea dhiki,
Mishikeli miamia, kwako ona haitoki,
Mwanzo ungekumbukia, ngekuwa huaziriki,
Uliyataka mwenyewe!

Dunia nayo hadaa, kwa fukara na maliki,
Ulimwenguni shujaa, hilo kama hukumbuki,
Ya nini kuyashangaa? Elewa hayafutiki,
Uliyataka mwenyewe!

Mwenyewe umelichimba, la kukuzika handaki,
Ulijidhania simba, hutishiki na fataki,
Machungu yamekukumba, hata neno hutamki,
Uliyataka mwenyewe!

Kwa mno ulijivuna, kwa mambo ukadiriki,
Na tena ukajiona, kwamba we mstahiki,
Ndugu umepatikana, mikanganyo huepuki,
Uliyataka mwenyewe!

Majuto ni mjukuu, huja kinyume rafiki,
Ungejua mwisho huu, ungetenda yalo haki,
Uko roho juujuu, popote hapakuweki,
Uliyataka mwenyewe!

Maswali
a) Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 2)
b) Tambua njia mbili anazotumia mtunzi wa shairi hili kuusisitiza ujumbe wake. (alama 2)
c) Taja na utoe mifano ya aina zozote mbili za tamathali za usemi zilizotumika katika shairi.
(alama 4)
d) Andika ubeti wa tatu katika lugha nathari/ tutumbi.

e) Kwa kutoa mfano mmoja mmoja onyesha aina mbili za idhini ya kishairi katika shairi hili.
(alama 4)
f) Bainisha toni ya shairi hili. (alama 2)
g) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi. (alama 2)
(i) Mstahiki
(ii) Hupuliki

 20 marks

SEHEMU YA B (Alama 20)

RIWAYA: KIDAGAA KIMEMWOZEA-KEN WALIBORA Jibu Swali la 2 au 3

2.

“Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Ni nini sifa za mvuto zinazowaleta pamoja mzungumzaji na mzungumziwa. (alama 4)
c) Tambua na ufafanue mbinu inayotumika katika dondoo. (alama 2)
d) Kwa mifano mwafaka fafanua tanzia hiyo inayorejelewa katika dondoo. (alama 10)

 20 marks

3.

Kuvunjwa kwa haki na sharia lilikuwa jambo la kawaida chini ya uongozi wa Mtemi Nasaba
Bora.Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea riwaya.

 20 marks

SEHEMU YA C (Alama 20)

TAMTHILIA: MSTAHIKI MEYA – TIMOTHY AREGE Jibu swali la 4 au 5

4.

“Iwapo umefanya, yapo mengi ambayo hayakunyoka.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Tambua mbinu moja iliyotimika katika muktadha wa dondoo. (alama 2)
c) Fafanuakaulikwamba’yapomengiambayohayakunyoka”. (alama 8)
d) Eleza jinsi baadhi ya wahusika walivyojaribu kuyanyoosha. (alama 6)

 20 marks

5.

Kwa kutoa mifano kumi, eleza vizingiti walivyokumbana navyo Wanacheneo wakati wa
kupigania mageuzi.

 20 marks

SEHEMU YA D (Alama 20)

HADITHI FUPI DAMU NYEUSI NA HADITHI NYINGINE K. WALIBORA NA S.A. MOHAMMED

6.

“Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Bainisha tamathali mbil iza usemi zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 4)
c) Huku ukitoa mifano, thibitisha maudhui sita ambayo yamejitokeza katika hadithi ya Damu Nyeusi
na wanayoyaendeleza. (alama 12)

 20 marks

SEHEMU YA E (Alama 20)

FASIHI SIMULIZI Jibu Swali la 7 au 8

7.

(a) Maigizo ni nini? (alama 2)
(b) Taja sifa nne za maigizo. (alama 4)
(c )Eleza mambo manne anayopaswa kufanya mwigizaji ili kufanikisha uigizaji wake. (alama 8)
(d) Ni nini umuhimu wa maigizo. (alama 6)
8. Kushiriki ni mbinu moja ya kukusanya data katika utafiti wa kazi za fasihi simulizi.
a) Eleza hoja tano kuhusu umuhimu wa mbinu ya kushiriki. (alama 10)
b) Eleza hoja tano za udhaifu wa mbinu ya kushiriki. (alama 10)

 20 marks

Leave a Comment