Welcome to Ugfacts.net/ke. On this page you will find details on the following topics

KUCCPS Admission Letters KUCCPS Student Portal KUCCPS Admission Lists
FREE KNEC KCSE Past Papers FREE KNEC KCPE Past Papers List of All Past Papers 
Fees Structure for 2024-2025 KNEC KCPE KNEC KCSE
Intakes and Admissions 2024-2025 List of Courses Offered Latest Jobs in Kenya 2024-2025
TVET Applications 2024-2025 TSC KNUT
KDF Recruitment Kenya Police Recruitment Kenya Prisons Service Recruitment

Your Opinions and Questions Matter. Kindly leave your comments below and we shall attend to you promptly.

KNEC KCSE Kiswahili Paper 3 Question Paper / 2016 KCSE MOKASA Joint Examination

KNEC KCSE Kiswahili Paper 3 Question Paper / 2016 KCSE MOKASA Joint Examination

2016 KCSE MOKASA Joint Examination

Kiswahili Paper 3

1.HADITHI FUPI: (Alama 20)

DAMU NYEUSI NA HADITHI NYINGINE 1. Swali la lazima

1.

“Hakujua maisha yake yangechukua mkondo upi. Mzo wa majuto ulimwandama. Ulimwengu
wake ulivurugika, akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Taja na kueleza tamathali ya usemi kwenye dondoo hili. (alama 4)
(c) Kwa kutolea mifano, onyesha jinsi anwani Kanda la Usufi inavyoafiki hadithi husika.
(alama 12)

 20 marks

2. SEHEMU YA RIWAYA (Alama 20)

Kidagaa Kimemwozea: Ken Walibora Jibu swali kla 2 au la 3

2.

“Nyamaza boza wewe. Wadhani sisi kazi tunaanza leo? Tumekutana na wauaji wangapi?
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Dondoo hili linadokeza maudhui gani? Kwa kutoa mifano saba kwenye riwaya, bainisha
jinsi maudhui hayo yanavyojitokeza. (alama 16)

 20 marks

3.

Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bil kutarajiwa. Fafanua.

 20 marks

3. SEHEMU YA TAMTHILIA (Alama 20)

MSTAHIKI MEYA: Timothy Arege

4.

Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Fafanua nafasi ya wanaorejelewa kuwa “ walifanya vizuri kuja” katika tamthilia hii.
(alama 4)
(c) Migogoro katika tamthilia hii hazikusuluhishwa vyema. Jadili. (alama 12)

 20 marks

5.

Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.

 20 marks

4.SEHEMU YA USHAIRI (Alama 20)

6.

Nitafukuzwa mbinguni
Kwa ushairi wangu mbaya
Lakini hata motoni nitaimba:
Wanasema
Wanasiasa ni kama jizi
Lililosukuma mtoto pembeni
Na kunyonya ziwa la mama
Wakati amelala usingizi usiku.

Wanasema
Mwanasiasa afapo
Tumejikomboa na domo
Moja pana lizibwalo na mchanga
Na kilima cha simenti ngumu
Lisikike tena hadharani.

Wanasema pia
Kusema haki
Kwa kawaida
Wanasiasa hatuwapendi.
Kupiga kura ni hasira za mkizi
Ni basi tu. Ni Ah!
Ah!
Wanamalizia
Nchi mmefiilisi waacheni walimu
Wakajenga taifa jipya.

Kama hamwezi kuona mbali
Bure kuweka mkono usoni,
Bure hakuna kichwa
Kama hamwezi kufikiri.

Ng’ombe amekamuliwa na wazungu
Waarabu, wahindi na wao
Sasa anatoa damu
Vilivyobaki ni chai ya rangi
Na madomo mapana zaidi
Yaliyo bado hai.
Kuimba nimeimba

(a) Mshairi ana dhamira gani? (alama 2)
(b) Shairi hili ni la kukatisha tama, tetea rai hii. (alama 2)
(c) Onyesha matumizi mawili ya mishata. (alama 2)
(d) Eleza mbinu zozote nne za lugha zilizotumika katika shairi hili. (alama 4)
(e) Andika ubeti wa mwisho katika lugha tutumbi. (alama 4)
(f) Fafanua umbo la shairi hili. (alama 3)
(g) Eleza maana ya mafungu ya maneno ya maneno yafuatayo: (alama 3)
(i) kupiga kura ni hasira ya mkizi
(ii) kuweka mkono usoni
(iii) ng’ombe amekamuliwa.

 20 marks

7.

7. SABUNI YA ROHO
Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
Ndiwe suluhu za zama, waja wakukimbilia,
Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
Ndiwa sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvinja mlima.

Matajiri wanakujua, wema wako wameonja,
Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
Sura zao ‘mefufua, wanazuru kila njanja,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
Watazame mayatima, kwao kumekua duni,
Webebe waliokuwa, wainue walio chini,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Ndiwe mvunja mlima, wapi kapata uwezo,
Umezua uhasama, waja kupata mizozo,
Ndiwe chanzo cha zahama, umewatia vikwazo,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Umevunja usuhuba, familia zazozana,
Waliokuwa mahabuba, kila mara wagombana,
Roho zao umekaba, majumbani wachinjana,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
Niondoe jahanamu, ya ufukara wa simu,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika,
Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

Maswali
(a) Taja nafsi nenewa. Thibitisha. (alama 2)
(b) Eleza toni ya nafsi neni. (alama 1)
(c) Eleza arudhi zozote nne zilizozingatiwa katika utunzi wa shairi hili. (alama 4)
(d) Mshairi anawasilisha ujumbe gani katika mleo wa ubeti wa sita? (alama 1)

(e) Ukitoa mfano eleza mbinu zozote tatu za lugha alizotumia mshairi. (alam 3)
(f) Andika ubeti wa nne katika lugha nathari. (alam 4)
(g) Jadili jinsi mshairi anatumia ruhusa ya mshairi. (alama 2)
(h) Kwa kurejelea mpangilio wa vina eleza bahari ambamo shairi hili linaweza
kuainishwa. (alam 1)
(i) Fafanua maana ya : (alama 2)
(i) ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima
(ii) jehanamu

 20 marks

5.FASIHI SIMULIZI (Alama 20)

8.

(a) Eleza maana ya mivigha. (alama 2)
(b) Fafanua sifa zozote nne za mivigha. (alama 8)
(c) Taja hasara zozote nne zinazohusishwa na mivigha. (alama 4)
(d) Eleza njia zozote tatu unazoweza kutumia kukusanya data kuhusu mivigha. (alama 6)

 20 marks

Leave a Comment