Welcome to Ugfacts.net/ke. On this page you will find details on the following topics

KUCCPS Admission Letters KUCCPS Student Portal KUCCPS Admission Lists
FREE KNEC KCSE Past Papers FREE KNEC KCPE Past Papers List of All Past Papers 
Fees Structure for 2024-2025 KNEC KCPE KNEC KCSE
Intakes and Admissions 2024-2025 List of Courses Offered Latest Jobs in Kenya 2024-2025
TVET Applications 2024-2025 TSC KNUT
KDF Recruitment Kenya Police Recruitment Kenya Prisons Service Recruitment

Your Opinions and Questions Matter. Kindly leave your comments below and we shall attend to you promptly.

Kenya Certificate of Primary Education

Kenya Certificate of Primary Education

Kenya Certificate of Primary Education

Kiswahili

Sehemu ya Kwanza

Ukarimu ni……..1………Mtu……..2………na ukarimu……..3……..kwa misemo kama vile……..4……..Ukarimu ni……..5………ambayo……..6……..kufunzwa mwanajamii……..7………

1. A. tabia ya kuwasaidia wengine bila malipo

B. hali ya kuwatambua walio na malipo

C. mazoea ya kuwaonea wengine huruma wakilipishwa

D. mwenendo wa kuchangisha wanaolipwa

2. A. asingekuwa B. asipokuwa C. asiokuwa D. asikokuwa

3. A. hurejelewa B. hurejeleana C. hurejelea D. hurejeleka

4. A. moyo mzito B. panya wa nyumba C. shingo ngumu D. joka la mdimu

5. A. maarifa B. stadi C. maadili D. nasaha

6. A. yanastahili B. inastahili C. zinastahili D. unastahili

7. A. wowote B. yeyote C. lolote D. yoyote

……..8………na Kani katika kidato cha kwanza. Kani alikuwa…….9…..wanafunzi bora ……..10………kuona. Hakukata tamaa hata……..11……..masomoni. Kani alikuwa rafiki wa dhati. Alinisaidia ……..12……..aina za maneno kama vile……..13…….ambayo ni vivumishi. Pia alinifunza kutenga silabi katika maneno mbalimbali. Kwa mfano, neno ‘nywesheana’ lina silabi……..14………Aidha, aliniambia kwamba umoja wa sentensi, ‘Mazulia hayo yao yalifumwa na washonaji wale, ni:……..15……… 8. A. Nimekutana B. Ningekutana C. Nilikutana D. Nikakutana

9. A. miongoni mwa B. mkabala mwa C. baadhi ya D. mithili ya

10. A. niliyewahi B. niliowahi C. aliowahi D. aliyewahi

11. A. alipoharibikiwa B. alipoharibiwa C. alipoharibikia D. alipoharibia

12. A. kumfunza B. kujifunza C. kutufunza D. kuwafunza

13. A. C. sana, nene, fupi, kama kijanja, tano, langu, leo B. D. nyingine, ajabu, mwenyewe, kisha kadha, yule, chungu, lote

14. A. 5 B. 6 C. 4 D. 3

15. A. Zulia hilo lao lilifiimwa na washonaji wale

B. Mazulia hayo yao yalifumwa na mshonaji yule

C. Zulia hilo lake lilifumwa na mshonaji yule

D. Mazulia hayo yake yalifumwa na washonaji wale

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi.

16. Maneno yafuatayo yanafuatana vipi katika kamusi?

(i) shtaka (ii) somea (iii) sinia (iv) sebule

A. iv, i, iii, ii

B. iv, ii, i, iii

C. iv, iii, i, ii

D. iv, i, iii, ii

17. Ni jibu lipi lenye mpangilio sahihi wa aina za maneno katika sentensi ifuatayo? Wanafunzi hawa ni hodari kuliko wengine.

A. nomino, kivumishi, kitenzi, kivumishi, kihusishi, kiwakilishi;

B. nomino, kitenzi, kiwakilishi, kivumishi, kihusishi, kivumishi;

C. nomino, kielesi, kitenzi, kivumishi, kiunganishi kiwakilishi;

D. nomino, kielesi, kitenzi, kihusishi, kiunganishi, kivumishi.

18. Ni jibu lipi lisiloambatanishwa ipasavyo?

A. koo jimbi

B. mjomba halati

C. shaibu buda

D. mavyaa bavyaa

19. Chagua jibu lenye kivumishi kilichoundwa kutokana na kitenzi.

A. ita — mwito

B. sahau — sahaulifu

C. agiza — maagizo

D. vumilia — uvumilivu

20. Ni sentensi ipi inayoonyesha kusudi la tendo?

A. Suna aliingia zizini akawafungulia ng’ombe, akaelekea malishoni.

B. Malika alituambia twende tukavue samaki.

C. Wafanyakazi walifanya bidii wakamaliza kazi hiyo.

D. Wageni watakuja watakapokamilisha shughuli.

21. Sentensi, ‘Sauna aliwafanya Siki na Patu waandike insha,’ inamaanisha;

A. Sauna aliwaandikisha Siki na Patu insha.

B. Sauna aliwaandikishia Siki na Patu insha.

C. Siki na Patu walimwandikia Sauna insha.

D. Siki na Patu waliandikia insha kwa Sauna.

22. Chagua jibu lenye viambishi vya neno: funguliana.

A. fu-a-na

B. li-an-a

C. fu-an-a

D. li-a-na

23. Chagua senstensi iliyoafikishwa ipasavyo.

A. Vifaa vyote — vile vilivyoagizwa jana — vimeletwa.

B. Lo, hilo kubwa hivyo, utaliweza?

C. Magunia haya hayatoshi! tutanunua mengine.

D. Mweka hazina (aliyeteuliwa) hapa jana rit (mwenye) bidii.

24. Ni sentensi ipi iliyo katika hali timilifu?

A. Magari hayapiti hapa siku hizi.

B. Mitaro hiyo haijachimbwa vyema.

C. Nguo yake haikuoshwa ipasavyo.

D. Wimbo hautaimbishwa na kiongozi.

25. Onyesha sentensi iliyounganisha sentensi zlfuatazo ipasavyo.

Makaa alijaribu kuliokoa dau hilo. Makaa hakufaulu.

A. Mithili ya Makaa kujaribu kuliokoa dau hilo, hakufaulu.

B. Licha ya Makaa kujaribu kuliokoa dau hilo, hakufaulu.

C. Makaa alijaribu kuliokoa dau hilo madhali hakufaulu.

D. Makaa alijaribu kuliokoa dau hilo walau hakufaulu.

26. Chagua sentensi yenye kivumishi kiulizi.

A. Leo wameapishwa wangapi?

B. Wasusi, wanaelekea wapi?

C. Huyu atavikwa pete gani?

D. Mashubaka haya yalitengenezwa lini?

27. Methali “Fimbo ya mbali haiui nyoka” huambiwa mtu anayetegemea walio mbali kutatulia matatizo yake. “Kiserema hulima kikashinda jembe zima,” huambiwa:

A. Mtu anyejiona kuwa maarufu sana katika jambo kuliko wengine.

B. Mtu anyeziona hali za wengine kuwa za kawaida kuliko zao.

C. Mtu anayedharau matatizo yake kuliko ya wengine.

D. Mtu anayepuuza makubaliano ya wengine kuliko yao.

28. Chagua usemi wa taarifa wa sentensi ifuatayo. “Shule zitafunguliwa lini?” Yohana akauliza.

A. Yohana alitaka kujua wakati ambapo shule zingefunguliwa.

B. Yohana aliuliza ikiwa shule zitafunguliwa.

C. Yohana aliuliza wakati ambapo shule zinafunguliwa.

D. Yohana alitaka kujua ikiwa shule zingefunguliwa.

29.Ikiwa juzi ilikuwa Jumanne, mtondo itakuwa:

A. Ijumaa

B. Jumapili

C. Jumamosi

D. Jumatatu

30. Akisami, 3/8 kwa maneno ni:

A. sudusi tatu

B. thuluthi nane

C. tusui nane

D. thumni tatu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.

Msemo,“Vijana ndio viongozi wa kesho”, hutolewa na wengi bila kuwazia maana yake. Hata hivyo, ni dhahiri kwamba mtu anapoupigia darubini msemo huu, utamwelekeza kugundua kuwa vijana ni mbegu ambayo inahitaji kupaliliwa ili kukifaa kizazi chao na cha siku za usoni. Tunaposema kwamba vijana ni viongozi wa kesho, tunamaanisha kwamba vijana ndio wanaotarajiwa kuchukua usukani wa kuidhibiti jamii yao wakati utendakazi wa watangulizi wao unapofikia kikomo kutokana na umri au maradhi.

Ni muhimu kujiuliza, “Ni kwa vipi vijana wanaweza kuwa tegemeo la kesho?” Kwanza kabisa, ibainike kwamba vijana, kwa sababu ya umri wao mbichi, wana mifupa myepesi, hivyo utendakazi wao huwa bora kuliko wa watu wa makamo au wale waliobugia chumvi nyingi. Isitoshe. kwa sababu ya bongo zao kuwa changa, vijana huweza kujifunza kwa urahisi mbinu mpya na bora za kuendeleza nchi.

Bila shaka ukitazama katika mazingira yako, unapata kwamba aghalabu vijana ndio wenye ustadi wa hali ya juu katika kutumia teknolojia ya kisasa. Hali hiyo inachangia kuimarisha ubunifu na kuboresha hali ya maisha.

Sijui kama unafahamu kwamba ile huduma ya simu almaarufu MPESA ambayo imeifanya Kenya kutia fora kitaifa na kimataifa ilibuniwa na kijana. Hali kadhalika, vijana wana nafasi kubwa katika kuendeleza maaadili na mshikamano wa kijamii. Kundi hili lina ushawishi mkubwa kwa raia.

Kwa vile vijana ndio wengi nchini, wanaweza kuifikia asilimia kubwa ya raia na kuiathiri, ama kwa njia hasi, au chanya. Si ajabu kupata kwamba mizozo mingine nchini, japo huenda inazuliwa na wazee, hupaliliwa na kuendelezwa zaidi na vijana waliopotoshwa na wazee hawa.

lsitoshe, kwa vile vijana wanaaminiana na kuthaminiana sana, wao wanaweza kusaidia kubadili mienendo ya wenzao. Ukichunguza katika jamii unamoishi, utapata kwamba vijana wengi huhiari kuwafichulia wenzao siri zao badala ya wazazi wao. Hili labda husababishwa na tofauti za kiumri na kimtazamo kati ya vijana na wazazi, au kile vijana wanachokiita, ‘ukali wa wazazi’.

Kwa sababu ya kuaminiana kwa vijana, utapata kwamba vijana wengi wameweza kuwashauri wenzao dhidi ya kuchukua hatua zisizo za busara kama vile kujiingiza katika ndoa za mapema, kushiriki mapenzi kiholela na hata kujitia kitanzi.

Umuhimu wa vijana hauwezi kupuuzwa. Licha ya kwamba wao ndio wanotarajiwa kuklendeleza kizazi cha jamii yao, wao ndio wanorithishwa desturi za jamii yenyewe ili kuziendeleza. Ni jukumu la wanajamii kuhakikisha kwamba wamewatayarisha vijana kukabiliana na majukumu yao.

Jamii haina budi kuhakikisha kwamba asilimia kubwa ya vijana imepata elimu ili kupata stadi za kuzalisha mali na kuendeleza uongozi ufaao.

Kadhalika, ni muhimu kuhakikisha kwamba vijana hawabakii tu kuwa viongozi wa kesho katika kauli na maandishi yetu.Washirikishwe katika uongozi wenyewe wakiwa wadogo ili ifikapo wakati wa kuzichukua nyadhifa za ngazi za juu waweze kuzimudu ipasavyo. Wanaotumia msemo, ‘Viongozi wa kesho kumaanisha kwamba vijana hawana nafasi katika uongozi wa sasa nao waonywe dhidi ya haya.

Wakumbushwe kuwa iwapo watang’ang’ania kubaki uongozini hata wanapofikia umri wa kustaafu, wanaendelea kuua ari ya vijana ya kuwajibikia uongozi wa jamii yao.

31. Kulingana na kifungu, vijana ndio viongozi wa kesho kwani wao:

A. wakiheshimiwa vizuri wataweza kuanzisha kizazi kijacho;

B. wakitayarishwa vyema wanaweza kuiletea jamii neema baadaye;

C. wakitambuliwa ipasavyo wanaweza kuifahamisha jamii faida yao baadaye;

D. wakiamuliwa ipasavyo, wanaweza kuandaliwa mamlaka yajayo.

32. Aya ya kwanza imeonyesha kwamba:

A. Umri na hali ya afya ya mtu huathiri matokeo ya kazi yake.

B. Kutokuwepo kwa vijana hupunguza matumaini ya kurithi mamlaka.

C. Kutowafikiria vijana hudhoofisha uongozi unaotangulia.

D. Unyonge wa mwili huathiri kubadilishana kwa zamu kazini.

33. Katika jamii yenye watu wachanga:

A. Njia mpya za kukabiliana na umri hustawishwa.

B. Udumishaji wa teknolojia ya kisasa huwa maarufu.

C. Mikakati bora ya kufanikisha maendeleo huanzishwa.

D. Hali ya kubuni mitandao huwa ya kimataifa.

34. Kulingana na aya ya tatu:

A. Mizozo ya wazee waliopotoka hutangazwa zaidi na vijana.

B. Vijana hufichua siri za wengine kuliko

wazazi wao.

C. Kuaminiana miongoni mwa vijana huwafanya wengine wasiuawe.

D. Vijana ndio wanaoweza zaidi kuendeleza matendo mema katika jamii.

35. Vijana wanaweza kuleta mapinduzi yafaayo nchini kwa vile:

A. Mizozo inapoanzishwa wao huwa na ushauri tofauti.

B. Siri zinapotokea nyumbani wao huwafichulia wenzao.

C. Wanapendana na kujitambulisha na kila mmoja wao.

D. Wanafunzana na kuelewa tofauti za wazazi.

36.Chagua jibu lisilo sahihi kwa mujibu wa kufungu: Vijana:

A. wanawaogopa wazazi wao kwa vile watu wanajua ni wakali;

B. huwaficha wazazi mambo kwa sababu ni wa kizazi kingine;

C. wanachangia katika utoaji nasaha katika jamii;

D. wanaweza kubadilisha na kuyaokoa maisha ya wenzao.

37. Mwandishi ameonyesha kwamba vijana ndio:

A. wanaopaswa kuanzisha elimu ya jamii;

B. wanaopitisha matendo na imani za jamii;

C. wanaotarajiwa kuhusiana na vizazi;

D. wanaowaonyesha mbinu za kutafuta mali kwao.

38.Chagua maana ya ‘anapoupigia darubini’.

A. anapousisitiza kwa uaminifu.

B. anapouelewa kwa dhati.

C. anapoufafanua kwa mapana.

D. anapouchunguza kwa kina.

39.Kulingana na aya ya mwisho kufanikiwa kwa vijana kunategemea:

A. kupewa majukumu ya uongozi wakiwa wachanga;

B. muda wanaochukua kufunzwa uongozi na jamii;

C. kustaafu uongozini kwa wazee wenye busara;

D. hamu wanayopata baada ya kuchukua uongozi.

40. Wanachokiita ‘ukali wa wazazi’ ina maana kwamba mwandishi:

A. anakana kuwa wazazi ni wakali;

B. anahofia kuwa wazazi ni wakali;

C. anadai kuwa wazazi ni wakali;

D. ameamini kuwa wazazi ni wakali.

Soma kifungu kffuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.

Kisa kuhusu shughuli ya wanyama kuchimba kisima husimuliwa kwa msisimko mkubwa katika jamii nyingi. Inasemekana kuwa wanyama, wakiongozwa na mfalme wao Simba, walikuwa wakiishi kwa amani na ushirikiano. Siku hizo, shida za mnyama mmoja zilikuwa za wanyama wote. Wale waliokuwa maskini walisaidiwa kwa chakula.

Wale ambao walikuwa wenye tamaa kama vile Fisi hawakusita kuonywa dhidi ya kutamani vya wengine. Wale waliokuwa watepetevu na wenye hila kama Sungura nao walishauriwa kuchanika kwenye mpini.

Alimradi kila mnyama alijifunga masombo kujenga jamii yenye utu na ustawi.

Hali iliendelea kuwa shwari, jamii ya wanyama ikijitosheleza kwa chakula msimu baada ya mwingine hadi mvua ilipogoma kunyesha.

Ukame mkubwa ulijiri; ardhi na mimea ikakauka, wanyama na makinda wao wakawa katika hatari ya kupukutishwa na njaa pamoja na jua lililowaka kama tanuri.

Baada ya kuwaza na kuwazua, Simba aliitisha mkutano wa wanyama ili washauriane kuhusu namna ya kukabiliana na hali ambayo ilikuwa tayari kukiangamiza kizazi cha wanyama.

Mkutano ulianza saa tatu asubuhi.

Kila mnyama alijihimu kufika rnapema. Kobe na Sungura ndio waliokuja wamechelewa kama desturi. Basi baada ya kusafisha koo, Simba a1isema,“Ndugu zangu, nimewaita hapa ili kujadiliana kuhusu jinsi tunavyoweza kukabiliana na hali ya ukame na njaa iliyotukumba. Ingawa maghala yetu bado yana nafaka, hali hii ya ukame ikiendelea, mifugo wetu watakufa.”

Kila mnyama alitoa maoni yake. Hatimaye waliafikiana kwamba wachimbe kisima kwa zamu ili wapate maji ya kunywa na kunyunyizia mimea. Simba alimwomba Nyumbu aandike ratiba ya jinsi kazi itakavyoendelea.

Alisema pia kwamba ikiwa katika siku ya kwanza maji yakatakuwa yamepatikana, basi atakayekuwa ameyapata atatunukiwa zawadi. Kauli hii ilimfanya kila mnyama kutaka kuwa wa kwanza kuchimba.

Mabishano makali yalitokea hadi pale Simba mwenyewe alipoamua kwamba ndiye atakayekuwa wa kwanza, kisha afuate Ndovu, Twiga Kifaru… na mwishowe Sungura. Alipotaja jina la Sungura, wanyama, hasa wale wakubwa, walicheka. wakishangaa vipi Sungura na umbo lake dogo atakavyoweza kuutifua udongo kupata maji.

Zamu ya Simba ilifika, akaelekea kulikokuwa kumetengwa kuchimbwa kisima. Alitifua udongo kwa maringo na nguvu zake zote lakini kilichotokea ni vumbi tu.

Aliondoka huku amejiinamia na kusimama kando. Ndovu alijua kwamba unene wake utamwezesha kutekeleza yale yaliyomshinda Simba. Alijaribu mara ya kwanza, ya pili, ya tatu… matokeo yakawa yale yale ya Simba. Ndovu alishusha pumzi kubwa, akatikisa kichwa na kuondoka, akaketi chini ya mti na kushika tama. Twiga, Kifaru na Duma walifuata lakini matokeo hayakuwa tofauti na ya wenzao; wote waliigonga ardhi kwa vichwa vyao, wakasalimiwa na vumbi tu.

Sasa ilikuwa zamu ya Sungura. Wanyama walimtazama kwa bezo huku wakijua kuwa Sungura hataweza lolote. Sungura aliinama kando ya mti mmoja mkubwa, akatoa mtaimbo na kuuchomeka kwenye kichwa chake.

Wanyama wengine walipomwona walicheka hadi mbavu zikavunjika. Sungura aliitalii ardhi kwa makini kabla hajaanza kuichimba kwa mtaimbo uliokuwa kichwani mwake. Baada ya dakika kumi za kuchimba, milizamu ya maji ilijitokeza ghafla na kuwalovya wanyama wote.

Ardhi sasa ilijaa unyevu, mimea ikaanza kuchipuka mara moja. Wanyama walimtazama Sungura kwa mshangao mkuu. Hakuna aliyenena lolote, wote waliinamisha nyuso chini.

Sungura alichukua kipaza sauti na kusema kwa fahari kuu, “Ndugu zangu, wakati wa vita wale wanaonusurika si walio na silaha kali bali wale wanaojua namna na wakati wa kuzitumia silaha hizo”.

41. Kulingana na aya ya kwanza, wanyama:

A. waliishi kwa amani kutokana na uongozi wa Simba;

B. walijali masilahi ya wale waliokuwa wanyonge;

C. walishangazwa na wanyama waliotamani vitu;

D. walichangamkia hadithi zilizohusu kuboresha hali zao.

42. Maendeleo katika jamii ya wanyama yalitokana hasa na:

A. kuwapa nasaha waliokuwa na matatizo;

B. kuwaonya wanyama wenye ubinafsi;

C. uwajibikaji wa pamoja wa wanyama;

D. uelekezaji wa wale wasiotia bidii.

43. Chagua athari za ukame kwa mujibu wa aya ya pili.

A. kiangazi kikali, hofu ya kupoteza uhai;

B. kukauka kwa mito, kutaabika kifikira;

C. kuongezeka kwa joto, kutojitosheleza kwa lishe:

D. kupotea kwa makinda, wanyama kusikitika.

44. Kulingana na kifungu, ni kawaida kwa:

A. Simba kuomba maoni ya wanyama;

B. Sungura kufika baada ya muda uliokubaliwa;

C. Wanyama kufurahia akiba ya nafaka;

D. Mifugo kuuawa wakati wa kiangazi.

45. Aya ya nne imebainisha kwamba:

A. Kutamani kuwa bingwa kunaweza kuzua utengano.

B. Kutarajia kumaliza kwanza kunaweza kuleta kutoelewana.

C. Kutegemea kufanikiwa maishani kunaweza kuonyesha kufarakana.

D. Kutaka kupata faida kunaweza kusababisha ugomvi.

46. Kwa nini wanyama walicheka?

A. Jina la Sungura liliwakumbusha kupuuza kazi kwake.

B. Kimo cha Sungura kilidhaniwa na wanyama kuwa udhaifu.

C. Kuja mwishoni kwa Sungura kungezuia kupatikana kwa maji.

D. Kustaajabisha kwa Sungura kulionyesha uwezo wa wanyama wakubwa.

47.Kifungu kimebainisha kwamba:

A. Jambo likifanywa na wanaowazia majivuno hutatizika.

B. Jambo likitendwa kwa kuwaiga wengine huonyesha kinyume.

C. Jambo likiwekewa mikakati ifaayo huwa na matokeo yaliyotarajiwa.

D. Jambo likishughulikiwa bila kuharakishwa huleta mabadiliko mema.

48. “Ndugu zangu, wakati wa vita wale wanaonusurika si walio na silaha kali bali wale wanaojua namna na wakati wa kutumia silaha hizo”.

Chagua methali inayoweza kujumuisha ujumbe wa kauli hii.

A. Makaa hayaoki nyama.

B. Kisu kibutu hakichinji kuku.

C. Jina la sifa huletwa na matendo.

D. Chombo imara hustahimili mawimbi makali.

49. “Walicheka hadi mbavu zikavunjika”, imetumia tamathali gani ya usemi?

A. chuku

B. sitiari

C. nahau

D. ishara

50. Chagua maana ya ‘kushika tama’ kwa mujibu wa kifungu.

A. kuhuzunika

B. kunung’unika

C. kukasirika

D. kuhangaika

Maswali na Majabu

Kenya Certificate of Primary Education

Kiswahili

Sehemu ya Kwanza

Ukarimu ni……..1………Mtu……..2………na ukarimu……..3……..kwa misemo kama vile……..4……..Ukarimu ni……..5………ambayo……..6……..kufunzwa mwanajamii……..7………

1. A.✔ tabia ya kuwasaidia wengine bila malipo

B. hali ya kuwatambua walio na malipo

C. mazoea ya kuwaonea wengine huruma wakilipishwa

D. mwenendo wa kuchangisha wanaolipwa

2. A. asingekuwa B.✔ asipokuwa C. asiokuwa D. asikokuwa

3. A.✔ hurejelewa B. hurejeleana C. hurejelea D. hurejeleka

4. A. moyo mzito B. panya wa nyumba C. shingo ngumu D.✔ joka la mdimu

5. A. maarifa B. stadi C.✔ maadili D. nasaha

6. A.✔ yanastahili B. inastahili C. zinastahili D. unastahili

7. A. wowote B.✔ yeyote C. lolote D. yoyote

……..8………na Kani katika kidato cha kwanza. Kani alikuwa…….9…..wanafunzi bora ……..10………kuona. Hakukata tamaa hata……..11……..masomoni. Kani alikuwa rafiki wa dhati. Alinisaidia ……..12……..aina za maneno kama vile……..13…….ambayo ni vivumishi. Pia alinifunza kutenga silabi katika maneno mbalimbali. Kwa mfano, neno ‘nywesheana’ lina silabi……..14………Aidha, aliniambia kwamba umoja wa sentensi, ‘Mazulia hayo yao yalifumwa na washonaji wale, ni:……..15………

8. A. Nimekutana B. Ningekutana C.✔ Nilikutana D. Nikakutana

9. A.✔ miongoni mwa B. mkabala mwa C. baadhi ya D. mithili ya

10. A. niliyewahi B.✔ niliowahi C. aliowahi D. aliyewahi

11. A.✔ alipoharibikiwa B. alipoharibiwa C. alipoharibikia D. alipoharibia

12. A. kumfunza B.✔ kujifunza C. kutufunza D. kuwafunza

13. A. C. sana, nene, fupi, kama kijanja, tano, langu, leo B. D.✔ nyingine, ajabu, mwenyewe, kisha kadha, yule, chungu, lote

14. A. 5 B. 6 C.✔ 4 D. 3

15. A. Zulia hilo lao lilifiimwa na washonaji wale

B. Mazulia hayo yao yalifumwa na mshonaji yule

C.✔ Zulia hilo lake lilifumwa na mshonaji yule

D. Mazulia hayo yake yalifumwa na washonaji wale

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi.

16. Maneno yafuatayo yanafuatana vipi katika kamusi?

(i) shtaka (ii) somea (iii) sinia (iv) sebule

A. iv, i, iii, ii

B. iv, ii, i, iii

C. iv, iii, i, ii

✔ D. iv, i, iii, ii

17. Ni jibu lipi lenye mpangilio sahihi wa aina za maneno katika sentensi ifuatayo? Wanafunzi hawa ni hodari kuliko wengine.

A.✔ nomino, kivumishi, kitenzi, kivumishi, kihusishi, kiwakilishi;

B. nomino, kitenzi, kiwakilishi, kivumishi, kihusishi, kivumishi;

C. nomino, kielesi, kitenzi, kivumishi, kiunganishi kiwakilishi;

D. nomino, kielesi, kitenzi, kihusishi, kiunganishi, kivumishi.

18. Ni jibu lipi lisiloambatanishwa ipasavyo?

A. koo jimbi

B. mjomba halati

C.✔ shaibu buda

D. mavyaa bavyaa

19. Chagua jibu lenye kivumishi kilichoundwa kutokana na kitenzi.

A. ita — mwito

B.✔ sahau — sahaulifu

C. agiza — maagizo

D. vumilia — uvumilivu

20. Ni sentensi ipi inayoonyesha kusudi la tendo?

A. Suna aliingia zizini akawafungulia ng’ombe, akaelekea malishoni.

B. Malika alituambia twende tukavue samaki.

C.✔ Wafanyakazi walifanya bidii wakamaliza kazi hiyo.

D. Wageni watakuja watakapokamilisha shughuli.

21. Sentensi, ‘Sauna aliwafanya Siki na Patu waandike insha,’ inamaanisha;

A.✔ Sauna aliwaandikisha Siki na Patu insha.

B. Sauna aliwaandikishia Siki na Patu insha.

C. Siki na Patu walimwandikia Sauna insha.

D. Siki na Patu waliandikia insha kwa Sauna.

22. Chagua jibu lenye viambishi vya neno: funguliana.

A. fu-a-na

B. li-an-a

C. fu-an-a

D.✔ li-a-na

23. Chagua senstensi iliyoafikishwa ipasavyo.

A.✔ Vifaa vyote — vile vilivyoagizwa jana — vimeletwa.

B. Lo, hilo kubwa hivyo, utaliweza?

C. Magunia haya hayatoshi! tutanunua mengine.

D. Mweka hazina (aliyeteuliwa) hapa jana rit (mwenye) bidii.

24. Ni sentensi ipi iliyo katika hali timilifu?

A. Magari hayapiti hapa siku hizi.

B. Mitaro hiyo haijachimbwa vyema.

C. Nguo yake haikuoshwa ipasavyo.

D. Wimbo hautaimbishwa na kiongozi.

25. Onyesha sentensi iliyounganisha sentensi zlfuatazo ipasavyo.

Makaa alijaribu kuliokoa dau hilo. Makaa hakufaulu.

A. Mithili ya Makaa kujaribu kuliokoa dau hilo, hakufaulu.

B. Licha ya Makaa kujaribu kuliokoa dau hilo, hakufaulu.

C. Makaa alijaribu kuliokoa dau hilo madhali hakufaulu.

D. Makaa alijaribu kuliokoa dau hilo walau hakufaulu.

26. Chagua sentensi yenye kivumishi kiulizi.

A. Leo wameapishwa wangapi?

B. Wasusi, wanaelekea wapi?

C.✔ Huyu atavikwa pete gani?

D. Mashubaka haya yalitengenezwa lini?

27. Methali “Fimbo ya mbali haiui nyoka” huambiwa mtu anayetegemea walio mbali kutatulia matatizo yake. “Kiserema hulima kikashinda jembe zima,” huambiwa:

A.✔ Mtu anyejiona kuwa maarufu sana katika jambo kuliko wengine.

B. Mtu anyeziona hali za wengine kuwa za kawaida kuliko zao.

C. Mtu anayedharau matatizo yake kuliko ya wengine.

D. Mtu anayepuuza makubaliano ya wengine kuliko yao.

28. Chagua usemi wa taarifa wa sentensi ifuatayo. “Shule zitafunguliwa lini?” Yohana akauliza.

A.✔ Yohana alitaka kujua wakati ambapo shule zingefunguliwa.

B. Yohana aliuliza ikiwa shule zitafunguliwa.

C. Yohana aliuliza wakati ambapo shule zinafunguliwa.

D. Yohana alitaka kujua ikiwa shule zingefunguliwa.

29.Ikiwa juzi ilikuwa Jumanne, mtondo itakuwa:

A. Ijumaa

B.✔ Jumapili

C. Jumamosi

D. Jumatatu

30. Akisami, 3/8 kwa maneno ni:

A. sudusi tatu

B. thuluthi nane

C. tusui nane

D. thumni tatu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.

Msemo,“Vijana ndio viongozi wa kesho”, hutolewa na wengi bila kuwazia maana yake. Hata hivyo, ni dhahiri kwamba mtu anapoupigia darubini msemo huu, utamwelekeza kugundua kuwa vijana ni mbegu ambayo inahitaji kupaliliwa ili kukifaa kizazi chao na cha siku za usoni. Tunaposema kwamba vijana ni viongozi wa kesho, tunamaanisha kwamba vijana ndio wanaotarajiwa kuchukua usukani wa kuidhibiti jamii yao wakati utendakazi wa watangulizi wao unapofikia kikomo kutokana na umri au maradhi.

Ni muhimu kujiuliza, “Ni kwa vipi vijana wanaweza kuwa tegemeo la kesho?” Kwanza kabisa, ibainike kwamba vijana, kwa sababu ya umri wao mbichi, wana mifupa myepesi, hivyo utendakazi wao huwa bora kuliko wa watu wa makamo au wale waliobugia chumvi nyingi. Isitoshe. kwa sababu ya bongo zao kuwa changa, vijana huweza kujifunza kwa urahisi mbinu mpya na bora za kuendeleza nchi.

Bila shaka ukitazama katika mazingira yako, unapata kwamba aghalabu vijana ndio wenye ustadi wa hali ya juu katika kutumia teknolojia ya kisasa. Hali hiyo inachangia kuimarisha ubunifu na kuboresha hali ya maisha.

Sijui kama unafahamu kwamba ile huduma ya simu almaarufu MPESA ambayo imeifanya Kenya kutia fora kitaifa na kimataifa ilibuniwa na kijana. Hali kadhalika, vijana wana nafasi kubwa katika kuendeleza maaadili na mshikamano wa kijamii. Kundi hili lina ushawishi mkubwa kwa raia.

Kwa vile vijana ndio wengi nchini, wanaweza kuifikia asilimia kubwa ya raia na kuiathiri, ama kwa njia hasi, au chanya. Si ajabu kupata kwamba mizozo mingine nchini, japo huenda inazuliwa na wazee, hupaliliwa na kuendelezwa zaidi na vijana waliopotoshwa na wazee hawa.

lsitoshe, kwa vile vijana wanaaminiana na kuthaminiana sana, wao wanaweza kusaidia kubadili mienendo ya wenzao. Ukichunguza katika jamii unamoishi, utapata kwamba vijana wengi huhiari kuwafichulia wenzao siri zao badala ya wazazi wao. Hili labda husababishwa na tofauti za kiumri na kimtazamo kati ya vijana na wazazi, au kile vijana wanachokiita, ‘ukali wa wazazi’.

Kwa sababu ya kuaminiana kwa vijana, utapata kwamba vijana wengi wameweza kuwashauri wenzao dhidi ya kuchukua hatua zisizo za busara kama vile kujiingiza katika ndoa za mapema, kushiriki mapenzi kiholela na hata kujitia kitanzi.

Umuhimu wa vijana hauwezi kupuuzwa. Licha ya kwamba wao ndio wanotarajiwa kuklendeleza kizazi cha jamii yao, wao ndio wanorithishwa desturi za jamii yenyewe ili kuziendeleza. Ni jukumu la wanajamii kuhakikisha kwamba wamewatayarisha vijana kukabiliana na majukumu yao.

Jamii haina budi kuhakikisha kwamba asilimia kubwa ya vijana imepata elimu ili kupata stadi za kuzalisha mali na kuendeleza uongozi ufaao.

Kadhalika, ni muhimu kuhakikisha kwamba vijana hawabakii tu kuwa viongozi wa kesho katika kauli na maandishi yetu.Washirikishwe katika uongozi wenyewe wakiwa wadogo ili ifikapo wakati wa kuzichukua nyadhifa za ngazi za juu waweze kuzimudu ipasavyo. Wanaotumia msemo, ‘Viongozi wa kesho kumaanisha kwamba vijana hawana nafasi katika uongozi wa sasa nao waonywe dhidi ya haya.

Wakumbushwe kuwa iwapo watang’ang’ania kubaki uongozini hata wanapofikia umri wa kustaafu, wanaendelea kuua ari ya vijana ya kuwajibikia uongozi wa jamii yao.

31. Kulingana na kifungu, vijana ndio viongozi wa kesho kwani wao:

A. wakiheshimiwa vizuri wataweza kuanzisha kizazi kijacho;

B.✔ wakitayarishwa vyema wanaweza kuiletea jamii neema baadaye;

C. wakitambuliwa ipasavyo wanaweza kuifahamisha jamii faida yao baadaye;

D. wakiamuliwa ipasavyo, wanaweza kuandaliwa mamlaka yajayo.

32. Aya ya kwanza imeonyesha kwamba:

A.✔ Umri na hali ya afya ya mtu huathiri matokeo ya kazi yake.

B. Kutokuwepo kwa vijana hupunguza matumaini ya kurithi mamlaka.

C. Kutowafikiria vijana hudhoofisha uongozi unaotangulia.

D. Unyonge wa mwili huathiri kubadilishana kwa zamu kazini.

33. Katika jamii yenye watu wachanga:

A. Njia mpya za kukabiliana na umri hustawishwa.

B. Udumishaji wa teknolojia ya kisasa huwa maarufu.

C.✔ Mikakati bora ya kufanikisha maendeleo huanzishwa.

D. Hali ya kubuni mitandao huwa ya kimataifa.

34. Kulingana na aya ya tatu:

A. Mizozo ya wazee waliopotoka hutangazwa zaidi na vijana.

B. Vijana hufichua siri za wengine kuliko

wazazi wao.

C. Kuaminiana miongoni mwa vijana huwafanya wengine wasiuawe.

D.✔ Vijana ndio wanaoweza zaidi kuendeleza matendo mema katika jamii.

35. Vijana wanaweza kuleta mapinduzi yafaayo nchini kwa vile:

A. Mizozo inapoanzishwa wao huwa na ushauri tofauti.

B. Siri zinapotokea nyumbani wao huwafichulia wenzao.

C.✔ Wanapendana na kujitambulisha na kila mmoja wao.

D. Wanafunzana na kuelewa tofauti za wazazi.

36.Chagua jibu lisilo sahihi kwa mujibu wa kufungu: Vijana:

A.✔ wanawaogopa wazazi wao kwa vile watu wanajua ni wakali;

B. huwaficha wazazi mambo kwa sababu ni wa kizazi kingine;

C. wanachangia katika utoaji nasaha katika jamii;

D. wanaweza kubadilisha na kuyaokoa maisha ya wenzao.

37. Mwandishi ameonyesha kwamba vijana ndio:

A. wanaopaswa kuanzisha elimu ya jamii;

B.✔ wanaopitisha matendo na imani za jamii;

C. wanaotarajiwa kuhusiana na vizazi;

D. wanaowaonyesha mbinu za kutafuta mali kwao.

38.Chagua maana ya ‘anapoupigia darubini’.

A.✔ anapousisitiza kwa uaminifu.

B. anapouelewa kwa dhati.

C. anapoufafanua kwa mapana.

D. anapouchunguza kwa kina.

39.Kulingana na aya ya mwisho kufanikiwa kwa vijana kunategemea:

A. kupewa majukumu ya uongozi wakiwa wachanga;

B. muda wanaochukua kufunzwa uongozi na jamii;

C. kustaafu uongozini kwa wazee wenye busara;

D.✔ hamu wanayopata baada ya kuchukua uongozi.

40. Wanachokiita ‘ukali wa wazazi’ ina maana kwamba mwandishi:

A.✔ anakana kuwa wazazi ni wakali;

B. anahofia kuwa wazazi ni wakali;

C. anadai kuwa wazazi ni wakali;

D. ameamini kuwa wazazi ni wakali.

Soma kifungu kffuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.

Kisa kuhusu shughuli ya wanyama kuchimba kisima husimuliwa kwa msisimko mkubwa katika jamii nyingi. Inasemekana kuwa wanyama, wakiongozwa na mfalme wao Simba, walikuwa wakiishi kwa amani na ushirikiano. Siku hizo, shida za mnyama mmoja zilikuwa za wanyama wote. Wale waliokuwa maskini walisaidiwa kwa chakula.

Wale ambao walikuwa wenye tamaa kama vile Fisi hawakusita kuonywa dhidi ya kutamani vya wengine. Wale waliokuwa watepetevu na wenye hila kama Sungura nao walishauriwa kuchanika kwenye mpini.

Alimradi kila mnyama alijifunga masombo kujenga jamii yenye utu na ustawi.

Hali iliendelea kuwa shwari, jamii ya wanyama ikijitosheleza kwa chakula msimu baada ya mwingine hadi mvua ilipogoma kunyesha.

Ukame mkubwa ulijiri; ardhi na mimea ikakauka, wanyama na makinda wao wakawa katika hatari ya kupukutishwa na njaa pamoja na jua lililowaka kama tanuri.

Baada ya kuwaza na kuwazua, Simba aliitisha mkutano wa wanyama ili washauriane kuhusu namna ya kukabiliana na hali ambayo ilikuwa tayari kukiangamiza kizazi cha wanyama.

Mkutano ulianza saa tatu asubuhi.

Kila mnyama alijihimu kufika rnapema. Kobe na Sungura ndio waliokuja wamechelewa kama desturi. Basi baada ya kusafisha koo, Simba a1isema,“Ndugu zangu, nimewaita hapa ili kujadiliana kuhusu jinsi tunavyoweza kukabiliana na hali ya ukame na njaa iliyotukumba. Ingawa maghala yetu bado yana nafaka, hali hii ya ukame ikiendelea, mifugo wetu watakufa.”

Kila mnyama alitoa maoni yake. Hatimaye waliafikiana kwamba wachimbe kisima kwa zamu ili wapate maji ya kunywa na kunyunyizia mimea. Simba alimwomba Nyumbu aandike ratiba ya jinsi kazi itakavyoendelea.

Alisema pia kwamba ikiwa katika siku ya kwanza maji yakatakuwa yamepatikana, basi atakayekuwa ameyapata atatunukiwa zawadi. Kauli hii ilimfanya kila mnyama kutaka kuwa wa kwanza kuchimba.

Mabishano makali yalitokea hadi pale Simba mwenyewe alipoamua kwamba ndiye atakayekuwa wa kwanza, kisha afuate Ndovu, Twiga Kifaru… na mwishowe Sungura. Alipotaja jina la Sungura, wanyama, hasa wale wakubwa, walicheka. wakishangaa vipi Sungura na umbo lake dogo atakavyoweza kuutifua udongo kupata maji.

Zamu ya Simba ilifika, akaelekea kulikokuwa kumetengwa kuchimbwa kisima. Alitifua udongo kwa maringo na nguvu zake zote lakini kilichotokea ni vumbi tu.

Aliondoka huku amejiinamia na kusimama kando. Ndovu alijua kwamba unene wake utamwezesha kutekeleza yale yaliyomshinda Simba. Alijaribu mara ya kwanza, ya pili, ya tatu… matokeo yakawa yale yale ya Simba. Ndovu alishusha pumzi kubwa, akatikisa kichwa na kuondoka, akaketi chini ya mti na kushika tama. Twiga, Kifaru na Duma walifuata lakini matokeo hayakuwa tofauti na ya wenzao; wote waliigonga ardhi kwa vichwa vyao, wakasalimiwa na vumbi tu.

Sasa ilikuwa zamu ya Sungura. Wanyama walimtazama kwa bezo huku wakijua kuwa Sungura hataweza lolote. Sungura aliinama kando ya mti mmoja mkubwa, akatoa mtaimbo na kuuchomeka kwenye kichwa chake.

Wanyama wengine walipomwona walicheka hadi mbavu zikavunjika. Sungura aliitalii ardhi kwa makini kabla hajaanza kuichimba kwa mtaimbo uliokuwa kichwani mwake. Baada ya dakika kumi za kuchimba, milizamu ya maji ilijitokeza ghafla na kuwalovya wanyama wote.

Ardhi sasa ilijaa unyevu, mimea ikaanza kuchipuka mara moja. Wanyama walimtazama Sungura kwa mshangao mkuu. Hakuna aliyenena lolote, wote waliinamisha nyuso chini.

Sungura alichukua kipaza sauti na kusema kwa fahari kuu, “Ndugu zangu, wakati wa vita wale wanaonusurika si walio na silaha kali bali wale wanaojua namna na wakati wa kuzitumia silaha hizo”.

41. Kulingana na aya ya kwanza, wanyama:

A.✔ waliishi kwa amani kutokana na uongozi wa Simba;

B. walijali masilahi ya wale waliokuwa wanyonge;

C. walishangazwa na wanyama waliotamani vitu;

D. walichangamkia hadithi zilizohusu kuboresha hali zao.

42. Maendeleo katika jamii ya wanyama yalitokana hasa na:

A. kuwapa nasaha waliokuwa na matatizo;

B. kuwaonya wanyama wenye ubinafsi;

C.✔ uwajibikaji wa pamoja wa wanyama;

D. uelekezaji wa wale wasiotia bidii.

43. Chagua athari za ukame kwa mujibu wa aya ya pili.

A.✔ kiangazi kikali, hofu ya kupoteza uhai;

B. kukauka kwa mito, kutaabika kifikira;

C. kuongezeka kwa joto, kutojitosheleza kwa lishe:

D. kupotea kwa makinda, wanyama kusikitika.

44. Kulingana na kifungu, ni kawaida kwa:

A. Simba kuomba maoni ya wanyama;

B. Sungura kufika baada ya muda uliokubaliwa;

C. Wanyama kufurahia akiba ya nafaka;

D.✔ Mifugo kuuawa wakati wa kiangazi.

45. Aya ya nne imebainisha kwamba:

A.✔ Kutamani kuwa bingwa kunaweza kuzua utengano.

B. Kutarajia kumaliza kwanza kunaweza kuleta kutoelewana.

C. Kutegemea kufanikiwa maishani kunaweza kuonyesha kufarakana.

D. Kutaka kupata faida kunaweza kusababisha ugomvi.

46. Kwa nini wanyama walicheka?

A. Jina la Sungura liliwakumbusha kupuuza kazi kwake.

B.✔ Kimo cha Sungura kilidhaniwa na wanyama kuwa udhaifu.

C. Kuja mwishoni kwa Sungura kungezuia kupatikana kwa maji.

D. Kustaajabisha kwa Sungura kulionyesha uwezo wa wanyama wakubwa.

47.Kifungu kimebainisha kwamba:

A. Jambo likifanywa na wanaowazia majivuno hutatizika.

B. Jambo likitendwa kwa kuwaiga wengine huonyesha kinyume.

C.✔ Jambo likiwekewa mikakati ifaayo huwa na matokeo yaliyotarajiwa.

D. Jambo likishughulikiwa bila kuharakishwa huleta mabadiliko mema.

48. “Ndugu zangu, wakati wa vita wale wanaonusurika si walio na silaha kali bali wale wanaojua namna na wakati wa kutumia silaha hizo”.

Chagua methali inayoweza kujumuisha ujumbe wa kauli hii.

A. Makaa hayaoki nyama.

B. Kisu kibutu hakichinji kuku.

C. Jina la sifa huletwa na matendo.

D.✔ Chombo imara hustahimili mawimbi makali.

49. “Walicheka hadi mbavu zikavunjika”, imetumia tamathali gani ya usemi?

A.✔ chuku

B. sitiari

C. nahau

D. ishara

50. Chagua maana ya ‘kushika tama’ kwa mujibu wa kifungu.

A.✔ kuhuzunika

B. kunung’unika

C. kukasirika

D. kuhangaika

1 thought on “Kenya Certificate of Primary Education”

Leave a Comment