KCPE Past Papers 2017 Kiswahili
Kenya Certificate of Primary Education
Kiswahili
Sehemu ya Kwanza
Mazugumzo_1___kanuni fulani ili _2___Lugha_3___msemaji lazima _4___ na msikilizaji _5___ sivyo kuwasiliana hakutapatikana.Mtu _6___ kuzugumza huanza qwa kutamka sauti _7___sauti hizi huwa ghuna.Mfano wa sauti ghuna ni _8___
1.A huzingatiwa B. huzingatiana C. huzingatia D. huzingatisha
2.A kuzifanikisha B. kumfanikisha C. kuyafanikisha D. kuifanikisha
3.A anayommia B. anapotumia C. anaotumia D. anavyotumia
4.A ueleweke B. aeleweke C. lieleweke D. ieleweke
5.A lau B. Tena C. bali D. Wala
6.A akijifunza B. amejifunza C. akajifunza D. anajifunza
7.A. Baadhi ya B. Mithili ya C. Zaidi ya D. Licha ya
8.A. m,f,g,th B. v,z,dh,w C. ch, s, d,t D. n, gh, h, k
Sherehe ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwangu _9___ . Niliamka alfajiri na mapema 10 _ Nilikuwa na hamu kuu ya kuona dada na kaka zangu wa toka nitoke yaani;_11___ wangu. Baada ya kupata kiamshakinywa, _12___ kuelekea sokoni _13___ nilinunua mboga za kila aina, si kabeji, si mchicha, si _14___ sukumawiki _15___ alimradi nilikuwa na vingi vya kununua.
9.A Itakuwa ikiwadia B. ikiwailiwadia C. ikawainawadia D. ilikuwaimewadia
10.A kujitayarisha B. kupatayarisha C. kuwatayarisha D. kuzitayarisha
11.A Wanunua B. Masomo C. Maumbu D. Wakoi
12.A Nilishika usukani B. nilishikatariki C. nilishika kani D. nilishika zamu
13.A ambayo B. ambao C. ambalo D. ambako
14.A kicha cha B. chane ya C. tita la D. mtungo wa
15.A ; B. – C. … D. !
Kutoka swali la 16 mpaka 30, chaguaj ibu sahihi.
16.Wingi wa, “Ua wa nyumba yaks umejengwa
na fundi mwenye bidii,” ni:
A. Ua wa nyumba zake umejengwa na mafundi wenye bidii.
B. Nyua za nyumba zao zimejengwa na mafimdi wenye bidii.
C. Nyua za nyumba zao zimej engwa na fundi mwenyc bidii.
D. Ua wa nyumba zao umejengwa na fundi mwenye bidii.
17.Neno, “kiliundiwa” lina silabi ngapi?
A.6
B.3
c.4
D.5
18.Chagua jibu lenye nomino zilizo katika ngeli ya I-ZI pekee.
A. pamba, taa
B. kucha, sahani
C. kuta, ngoma
D. nyuta, kamba
19.Nijibu lipi lenye maelezo sahihi?
A. Kipaj i ni sehemu ya kichwa inayohifadhi ubongo.
B. Goti ni sehemu ya mguu inayounganisha muundi na wayo.
C. Kiwiko huunganisha kiga_nja na sehemu ya juu ya mkono.
‘ D. Ufizi ni mfupa uliopo baina ya mdomo wa juu na wa chini.
20.Chagua ukanushc Wa:
Maembe yalitiwa kapuni yakaiva.
A. Maembe hayajatiwa kapuni na hayaivi.
B. Maembe hayakutiwa kapuni wala hayakuiva.
C. Maembe hayakutiwa kapuni yaive.
D. Maembe hayajatiwa kapuni yakaiva.
21.Chagua jibu lenye nomino iliyoundwa kutokana na nomino.
A. angaza – mwanga
B. samehe — msamaha
C. babaika ~ babaifu
D. mpishi — mapishi.
22.Usemi wa taarifa wa, “Mtavihifadhi vitabu
vyenu kwenye kabati,” mwalimu akatuambia, n1
A. Mwalimu alituambia kwamba tumvihifadhi vitabu vyetu kwenye kabati.
B. Mwalimu alituambia kwamba tungevihifadhi vitabu vyetu kwenye kabati.
C. Mwalimu alimambia kwamba tumevihifadhi vitabu vyetu kwenye kabati.
D. Mwalirnu aliruambia kwamba tulivihifadhi vitabu vyetu kwenye kabati.
23.Chagua aina za maneno yaliyopigiwa mstari.
Wageni file walialikwa tilakini wengjug hawakualikwa.
A. kivumishi, kielezi, kiwakilishi
B. kiwakilishi, kihusishi, kielezi
C. kielezi, kihusishi, kiwakilishi
D. kihusishi, kivumishi, kielezi
24.Kauli zilizopigiwa mstari zimetumia tamathali gani za usemi?
Tui ni chiriku anaweza kutamka maneno mia moja kwa sekunde.
A. majazi, nahau
B. tasfida, kinaya
C. sitiari, chuku
D. tashbihi, ishara
25.Chagua jibu Iisilolingana na mengine.
A. unga ~ kata
B. laini — ngumu.
C. kurnbuka — sahau
D. imara —- thabili
26.Chagua sentensi yenye “ki” ya wakati.
A. Wachezaji wanaimba wakishangilia.
B. Kikataa hicho kililimwa kikatoa mazao mengi.
C. Fundi alikishona kitambaa vizuri.
D. Wafanyakazi wanaifanya kazi hiyo kivivu.
27.Onyesha kauli ya kutendea ya sentensi zifuatazo: Munga alitengeneza gari. Munga alikuwa kiwandani.
A.Munga alitengenezea gad kiwandani.
B.Kiwandani Walimtengenezea Munga gari.
C.Munga alitengenezewa gari kiwandani.
D.Kiwandani kulitengenezewa gafi la Munga.
28.Chagua sentensi yenye maelezo sahihi.
A. Kukoga ni kuondoa uchafu mwilini na kukonga ni kutawanyia vitu mahali.
B. Kufuta ni kusukuma kitu kuelekea uliko na kuvuta ni kunusa.
C. Kusuka ni kutikisa kitu ilhali kuzuka ni kutokea kwa jambo.
D. Kutunga ni kupitisha uzi mahali ilhali kudunga ni kutoboa shimo.
29.Chagua sentensi iliyoakifishwa ipasavyo.
A. Lo, huoni unamzuia mwenzako?
B. Heza – alisema — Koru tutakutana kesho.
C. Mugou (yule mtangazaji hodari) amepata,
Tuzo ya Mtangazaji Bora.
D. Yafuatayo ndiyo yanayotarajiwa, kusajiliwa, kulipa karo, kuanza masomo.
30.Chagua semensi ambayo inaunganisha sentensi zifizatazo ipasavyo.
Gari Iilikuwa jipya. Gari halikumpendeza.
A. Gari lilikuwajipya madhali halikurnpendeza.
B. Licha ya gari kuwa jipya, halikumpendeza.
C. Gari lilikuwa jipya angaa halikumpendeza.
D. Mithili ya gari kuwa jipya, halikumpendeza.
Soma kzfimgu kzfimtacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.
Usalama ni moj awapo ya mahitaji ya kimsingi katika maisha ya binadamu. Nchi isiyowahakikisha raia wake usalama hujidhalilisha; ni sawa na kuku ambaye aonapo mwewe kukimbiza roho yake hukubakiwaacha vifaranga Wake kuwa kitoweo cha mwewe. Ukosefu Wa usalama hauathiri lu mtu binafsi, bali pia huathiri nchi na majirani wake.
Mathalani, vita vya kikabila vinapozuka nchini, raia, kwa kuhofia usalarna wao, hukimbilia kwa makabila mengine na hata nchi jirani. Wakimbizi hawa, licha ya kuwa wategemezi wa wafadhili wao, hupoteza hadhi yao kama binadamu, kwani daima mhitaji huwa mtumwa.
Isitoshe, katika nchi ambamo ukosefu wa usalama urneshamiri, uchumi hutetereka. Shughuli nyingi za uzalishaji mali na uwekezaji hugonga mwamba.
Wawekezaji wa ndani na nje huhofia kupoteza mali na roho zao. Hali hii hupalilia zaidi makali ya ukosefu wa nafasi za kazi na umaskini.
Maeneo mengi kalika nchi zilizo na tatizo la ukosefu wa usalama hukabiliwa na uchechefu wa wafanyakazi. Raia kindakindaki wa sehemu hizi hupungua.
Si ajabu kupata kwamba katika baadhi ya maeneo, wenyeji hawadiriki kujenga humo, kisa na maana; wanahofia kuchomewa nyumba zao na magaidi wanaodai asilimia kubwa ya fedha ili wasitekeleze uhalifu huu.
Matokeo ya haya ni kwamba shughuli za kiuchumi kama vile ufugaji zimeachiwa wachache, hususan wazee ambao hawana hamu ya kuhamia mijini.
Hali kadhalika, jamii isiyo na usalama huvuruga misingi ya mshikamano wa kijamii. Ni dhahiri kwamba wanajamii ambao Wanaendeleza vitendo kama vile wizi wa mifiigo, unyakuzi Wa ardhi, ubakaji, na ulawiti hupalilia zaidi utengano miongoni mwao.
Vitendo hivi huzua chuki, kisasi, kutoaminiana na mara nyingine husababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe. Katika hali hii baadhi ya raia huumizwa, wengine hufa n’a Wengine kuachiwa majei-aha ya moyo.
Tatizo la ukosefu wa usalama linapozungumziwa, watu moja kwa moja huwanyooshea vidole polisi na walinda usalama wengine.
Raia kwajumla huwa wepesi kusema,“Tunai sihi serikali imhakikishie usalama.” Jambo la kusikitisha ni kwamba wanaoiomba serikali kuwahakikishia usalama ndio kwa mfano, wanaojenga kando ya mito na kujifia katika hatari ya kusombwa na maji. Wengine wanatarajia serikali kuwahakikishia usalama huku wakiabiri magari yaliyojaa watu pomoni bila kuwazia hatari inayowakabili.
Wapo wengine ambao huhatarisha usalama wao kwa kunywa pombe haramu na kuambulia upofu. Wengine nao hula vyakula vyenye kemikali zinazoathiri afya zao. Wapo Wengine wanaojitia hatarini kwa kupuuza wito wa serikali wa kuhakikisha kuwa wamcjua anayeishi karibu nao, na kwamba wamewaangaza Wale ambao wanashukiwa kuwa pingamizi kwa usalama.
Isitoshe, kuna Wale ambao huhatarisha usalama wao kwa kutumia njia za kijadi za matibabu kama vile akjna mama kujifungulia nyumbani bila Wakunga maalum; jambo ambalo huhatarisha maisha ya Inzazi na mtoto pia.
Wengine hushiriki, vitendo viovu kama vile utunguaji mimba na kujisababishia vifo. Ni dhahiri kwamba kudumishwa kwa usalama kunahitaji mchango wa kila mwanajarnii.
Kama kila mtu angejifunga masombo kushughulikia usalama wake na wajirani, huenda hakungekuwa na haja ya polisi na hata walinda lango.
31.Kulingana na aya ya kwanza:
A. Mzazi asiyewalinda wanawe hupoteza hadhi yake kama mlezi.
B. Binadamu asiyepata anachohimji hualhirika anapoachwa na mzazi.
C. Mzazi 1-nwenye ubinafsi huhatarisha maisha yake kama mlezi.
D. Binadamu mwenye woga hushindwa kuwadhibiti Wanawe kama mzazi.
32.Vita vya kikabila:
A. husababisha kukimbizana kwa majirani;
B. huwafanya watu kuwa watumishi Wa maj irani;
C. huwafanya watu hupoteza heshima yao;
D. husababisha kutopatikana kwa mali.
33.Aya ya tatu imeonyesha kwamba:
A. Schemu zilizo na ukosefu wa usalama hazina wafanyakazi.
B. Tamaa inasababisha ukosefu wa usalama katika j amii.
C. Maeneo yenye ukosefu wa usalama hayana majengo ya wenyeji.
D. Kutokuwepo kwa usalama husababisha kutomiliki mifugo wengi.
34.Kulingana na kifungu, athari za ukosefu wa usalama ni:
A. kupungua kwa uzalishaji mali, kutokuwa B. wajenzi;mifugo michache, kutengana na wazee;
C. kushuldana, uharibifu wa mali;
D. kuuawa, kupata vidonda mwilini.
35.Mwandishi amedhihirisha kwarnba:
A. Walinda usalama huelekezewa lawama baada ya uhalifu kutokea.
B. Wenye magari yaliyojaa kote huhataflsha usalama.
C. Usalama unahusu kujua wanakotoka majirani wasioaminika.
D. Utulivu unaonyesha uwajibikaji wa serikali inapohitajika.
36.“Wanaoiomba serlkali kuwahakikishia usalama ndio kwa mfano, wanaojenga kando ya mito na kujitia katika hatari ya kusombwa na maji.”
Onyesha methali inayoweza kutumiwa kuwaonya watu hawa.
A. Mti huchongewa na tundaze.
B. Mto huvunjika kingo iliyo mbovu.
C.Ukibebwa usilevyelevye miguu.
D.Ukipanda pantosha utavuna pankwisha.
37.Ni wazi kwamba kudumisha usalama kunahitaji:
A. raia wenyewe kuyatambua matafizo ya waishio kwao;
B. Wanajamii Wenyewe kufahamu mchango wa serikali;
C. uwajibikaji Wa mtu binafsi katika shughuli zake;
D. kujifunza aina za lisha hora wenyewe.
38.Kulingana na kifimgu serikali:
A. inawataka watu kuwaogopa wanaodhaniwa kuwa wahalifu;
B. inawashaufl watu kuepuka kupata watoto nyumbani;
C. inawaonya Watu dhidi ya mauaji wakiwa wachanga;
D. inawahimiza watu kujua mienendo ya majirani wao.
39.Wazo kuu linalojitokeza katika aya ya mwisho, ni:
A. Usalama unadumishwa kwa mtu kuishi karibu na nyumbani.
B. Inamjuzu mtu kuwazia usalama unaoelezewa na wanajamii.
C. Ni muhimu mtu kujitahidi kuhakikisha usalama kwake na katika mazingira yake.
D. Maafisa mtaani hawahitajiki pale watu wanapoamini ni salama.
40.Chagua maana ya kindakindaki kwa mujibu wa kifilngu.
A. waliozaliwa hapo
B. waliohitajika hapo C.waliopatikana hapo.
D.waliothaminiwa hapo.
Somu kifungu kwmtacho kisha ujibu maswali 41 mpaka S0.
Siku hiyo jua lilichomoza mapema kuliko kawaida. Niliitazama miale yake kupitia kwenye dirisha la chumba changu. Rangi ya mialc hii iliibua rnjadala moyoni mwangu.
“Sijui kama macho yangu ndiyo yanayonipiga chenga, ila naona leo miale hii ina mabaka meusi yaliyolwaa wekundu wa damu,” moyo Wangu ukasema. “Ingawa mimi si mnajimu wala mshirikina, nadhani rangi hii imefumbata kitendawili fulani,” moyo ulirudia kusema. Baada ya mawazo haya nilishusha pumzi ndefu na kusema, “Siku njema huonekana asubuhi, huenda hii ni dalili ya wema wenyewe.
Juu ya hayo mustakabali wa siku umo mikononi mwake aliyciamrisha siku yenyewe kuwepo, bindamu ana hiari au usemi gani kuhusu yatakayokuwa au yatakayokosa kuwepo? Nilijikokota kutoka kitandani mwangu.
Siku hii nilikuwa na miadi na rafiki yangu Tindi ambayc alihitaji kununua vifaa vya nyumbani.
Rafiki huyu alikuwa kapata kazi ya uhasibu katika Shirika Ia Utozaji Ushuru baada ya kipindi cha kuhangaishwa na ulaji rushwa. Alikuwa anagura alikoishi na wazazi wake.
Kama alivyosema, alitaka kuishi peke yake ili ajifunze kujitegemea, Tulikuwa tumepanga kukutana katikajcngo moja la kibiashara ambamo mliuzwa aina nyingi za vifaa vya nyumbani.
Nilifika kwenye jengo hilo baada ya saa moja na nusu. Nilirnngojea rafiki yangu kwa takriban saa mbili ingawa alikuwa ameahidi kufika mapema.
Hata hivyo, kuchelewa huku hakukuwa ibra kwangu. “Vipi Bwana? Leo umczidi?” Nifimuuliza Tindi. “Samahani sana ndugu, ila wewe unajua katika mji wa Selea methali, ‘Chelewa chclcwa utampala mwana si wako’, haiwezi kuafiki.
Hata mm ukataka kuchapuka vipi, msongamano wa magari umkutilia vizingiti,” alijibu kama kawaida yaks. Tulijitoma katika shughuli ya ununuzi. Mara, “Leta hiki,” mara, “Rudisha, hiki ni ghali mno,” mara, “Punguza bei.” Hata baadaya muda usiopungua saa tano na nusu, tulikuwa tumenunua vyote vilivyokuwa kwenye orodha yetu ya bidhaa. Ghafla taa za umeme zilizimika, mlio wajenereta ukasikika, kisha mlipuko, na kiza cha kutisha. Mara nilisikia ukemi mkubwa uliopasua dari ya jengo hili. Ukemi huu ulifuatwa na sauti nenc ya kiume, “Fungeni vishubaka vya pesa! Nenda kafunge mlango wa mbele na wa nyuma!” Wakati hayo yote yakijiri, jumba lilikuwa limekumbatiwa na moto wa tanuri.
Joshi jeusi lilitanda kila mahali, vilio vya wateja waliokuwa wanatapatapa huku na huko kama kuku aliyedenguliwa shingo viliyaremba mandhari haya. Nilimshika Tindi mkono na kukimbilia mlango wa nyuma ambamo alisimama mlinda lango mmoja kuhakikisha hatubebi bidhaa yoyote; hata zile tulizokuwa tumelipia.
Nilijaribu kumsihi atufungulie tutoke lakini akakataa katakata. Amri ya Bwana Mkubwa ilimzuia hata kuona hatari iliyomkabili yeye. Hatimaye nilifanikiwa kutumia misuli yangu kumwondoa, nikajishukuru kwa mazoezi ya viungo ambayo mimi hufanya kila siku.
Mimi na Tindi tulifanikiwa kutoka nje bila majeraha ya haja. Ndani kule vilio vya roho zilizokuwa zikibanania kwenye mlango wa nyuma vilihanikiza. Bwana Mkubwa alikataa katakata kufimgua mlango Wa mbele; anahofia mali yake kukwepuliwa na wafu! Wapo walionusurika, wakapitia kwenye mlango huu, wapo waliosalimu amri ya moto, moshi, hewa yenye sumu na kubanwa na wenzao.
Hata Shirika la Zimamoto lilipowasili baada ya saa nne, jengo hilo lilikuwa majivu pamoja na vyote vilivyokuwcmo.
Runinga ya Taifa usiku huo iliarifu kwamba hata mwenye jengo aliyesimama wenye mlango wa mbele kulinda mali yake dhidi ya roho zilizokuwa zinateketea aliaga dunia.
41.Miale ya jua asubuhi hii:
A. Ilionyesha hali ya kuamini uchawi.
B. llimfanya Msimulizi kufikiri zaidi.
C.Ilikuwa kinyume na matarajio ya unajimu.
D.Ilisababisha upuuzaj i moyoni mwa mtazamaji.
42.Aya ya kwanza imedhihirisha kwamba:
A. Jambo huweza kutisha hata kama linaonekana zuri.
B. Ishara ya yanayotokea huonyesha mafanikio hapo mbeleni.
C. Binadamu hana mamlaka kuhusu hali inayoyaathiri maisha yake.
D. Mtu hukosa hakika ya mafumbo anayotoa akilini mwake.
43.Chagua jibu lisilo sahihi kwa mujibu wa kifungu.
A. Msimulizi anajua hii ni mara ya pili Tindi kuchelewa.
B. Ufisadi huathiri utoaji wa ajira nchini. C. Kuwepo kwa magari mengi barabarani hutatiza shughuli.
D. Pesa humpa mm nafasi ya kufiurahia uhuru wa kibinafsi.
44.Kauli, “Hata hivyo kuchelewa huku hakukuwa ibra kwangu”, inamaanisha:
A. Aghalabu Tindi hazingatii muda waliokubaliana kuanza shughuli.
B. Tindi ana hulka ya kuchelewa anaponunua bidhaa.
C. Msimulizi amezoea kutotimiza miadi ya Tindi.
D. Ni kawaida kwa Msimulizi kumwona Tindi baada ya kuchelewa.
45.Chagua mfuatano ufaao wa matukio kulingana na taarifa.
A. kuagiza bidhaa, kujadiliana bei, kupotea kwa umeme, mpasuko, giza nene;
B. kuagiza bidhaa, kukagua bidhaa, kuagiza nyingine, kupotea kwa umeme, sauti, giza nene;
C. kuagiza bidhaa, klmunua vyote, kupotea kwa umeme, moshi, giza nene;
D. kuagiza bidhaa, muda kuyoyoma, vilio, kupotea kwa umeme, giza nene.
46.Chagua sifa kuu za mwenye jengo kulingana na kifungu.
A. mwenye pupa, mwoga
B. mwenye tamaa, asiyewajibika
C. mwenye wivu, katili
D. mwenye dharau, asiyeamini
47.Chagua jibu ambalo si sahihi kwa mujibu wa kifungu.
A. Maafa mengi husababishwa na kutowazia hatirna za matendo yetu.
B. Utiifu huweza kurnletea rntu madhara.
C Desturi katika maisha yetu huweza kutuletea neema.
D.Sheria zitolewazo wanapoiba huweza kudhibiti waokoaji.
48.Aya ya mwisho imebainisha kwamba:
A.Msimulizi na Tindi walinusurika lcuumizwa.
B.Watu wengi walikufa kwa sababu ya kulinda mali zao.
C.Uharibifu mkubwa ulisababishwa na kutochukua hatua haraka.
D.Kufinyana kwenye moto kulileta moshi na sumu
49.Chagua kisawe cha kumsihi.
A. kumrai
B. lcumwelekeza
C. kumtahadharisha
D. kumshauri
50.“Hata mwenye jengo aliyesimama kwenye mlango wa mbele kulinda mali yake dhidi ya roho zilizokuwa ziuateketea aliaga dunia.”
Chagua tamathali mbili za usemi zilizotumiwa katika kauli hii.
A. tashbihi,sitiari
B. kinaya,nahau
C.ishara, tashihisi
D.chuku,majazi
Maswali na Majabu
Kiswahili
Sehemu ya Kwanza
Mazugumzo_1.C. huzingatiakanuni fulani ili 2.C. kuyafanikia_Lugha3.A. anayotumiamsemaji lazima 4.D. ielewekena msikilizaji 5.A. lau sivyo kuwasiliana hakutapatikana.Mtu 6.A akijifunza kuzugumza huanza qwa kutamka sauti 7.A. Baadhi ya _sauti hizi huwa ghuna.Mfano wa sauti ghuna ni 8.B. v,z,dh,w Sherehe ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwangu9.A Itakuwa ikiwadia . Niliamka alfajiri na mapema 10.D. kujitayarishaNilikuwa na hamu kuu ya kuona dada na kaka zangu wa toka nitoke yaani;11.C Maumbuwangu. Baada ya kupata kiamshakinywa, 12.C. nilishika tariki kuelekea sokoni 13.D ambako nilinunua mboga za kila aina, si kabeji, si mchicha, si 14.A. kicha cha sukumawiki15.C. … alimradi nilikuwa na vingi vya kununua.
Kutoka swali la 16 mpaka 30, chaguaj ibu sahihi.
16.Wingi wa, “Ua wa nyumba yaks umejengwa
na fundi mwenye bidii,” ni:
B. Nyua za nyumba yao zimjengwa na mafundi wenye bidii.
17.Neno, “kiliundiwa” lina silabi ngapi?
D.5
18.Chagua jibu lenye nomino zilizo katika ngeli ya I-ZI pekee.
D. Pamba, Taa
19.Nijibu lipi lenye maelezo sahihi?
B. Kiwiko huunganisha kiganja na sehemu ya juu ya mkono.
20.Chagua ukanusho Wa:
Maembe yalitiwa kapuni yakaiva.
B. Maembe hayakutiwa kapuni wala hayakuiva.
21.Chagua jibu lenye nomino iliyoundwa kutokana na nomino.
D. mpishi — mapishi.
22.Usemi wa taarifa wa, “Mtavihifadhi vitabu
vyenu kwenye kabati,” mwalimu akatuambia, ni
B. Mwalimu alituambia kwamba tungevihifadhi vitabu vyetu kwenye kabati.
23.Chagua aina za maneno yaliyopigiwa mstari.
Wageni file walialikwa tilakini wengjug hawakualikwa.
A. kivumishi, kielezi, kiwakilishi
24.Kauli zilizopigiwa mstari zimetumia tamathali gani za usemi?
Tui ni chiriku anaweza kutamka maneno mia moja kwa sekunde.
C. sitiari, chuku
25.Chagua jibu Iisilolingana na mengine.
D. imara —- thabili
26.Chagua sentensi yenye “ki” ya wakati.
A. Wachezaji wanaimba wakishangilia.
27.Onyesha kauli ya kutendea ya sentensi zifuatazo: Munga alitengeneza gari. Munga alikuwa kiwandani.
A.Munga alitengenezea gad kiwandani.
28.Chagua sentensi yenye maelezo sahihi.
C. Kusuka ni kutikisa kitu ilhali kuzuka ni kutokea kwa jambo.
29.Chagua sentensi iliyoakifishwa ipasavyo.
C. Mugou (yule mtangazaji hodari) amepata,
Tuzo ya Mtangazaji Bora.
30.Chagua semensi ambayo inaunganisha sentensi zifizatazo ipasavyo.
Gari Iilikuwa jipya. Gari halikumpendeza.
B. Licha ya gari kuwa jipya, halikumpendeza.
Soma kzfimgu kzfimtacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.
Usalama ni moj awapo ya mahitaji ya kimsingi katika maisha ya binadamu. Nchi isiyowahakikisha raia wake usalama hujidhalilisha; ni sawa na kuku ambaye aonapo mwewe kukimbiza roho yake hukubakiwaacha vifaranga Wake kuwa kitoweo cha mwewe. Ukosefu Wa usalama hauathiri lu mtu binafsi, bali pia huathiri nchi na majirani wake.
Mathalani, vita vya kikabila vinapozuka nchini, raia, kwa kuhofia usalarna wao, hukimbilia kwa makabila mengine na hata nchi jirani. Wakimbizi hawa, licha ya kuwa wategemezi wa wafadhili wao, hupoteza hadhi yao kama binadamu, kwani daima mhitaji huwa mtumwa.
Isitoshe, katika nchi ambamo ukosefu wa usalama urneshamiri, uchumi hutetereka. Shughuli nyingi za uzalishaji mali na uwekezaji hugonga mwamba.
Wawekezaji wa ndani na nje huhofia kupoteza mali na roho zao. Hali hii hupalilia zaidi makali ya ukosefu wa nafasi za kazi na umaskini.
Maeneo mengi kalika nchi zilizo na tatizo la ukosefu wa usalama hukabiliwa na uchechefu wa wafanyakazi. Raia kindakindaki wa sehemu hizi hupungua.
Si ajabu kupata kwamba katika baadhi ya maeneo, wenyeji hawadiriki kujenga humo, kisa na maana; wanahofia kuchomewa nyumba zao na magaidi wanaodai asilimia kubwa ya fedha ili wasitekeleze uhalifu huu.
Matokeo ya haya ni kwamba shughuli za kiuchumi kama vile ufugaji zimeachiwa wachache, hususan wazee ambao hawana hamu ya kuhamia mijini.
Hali kadhalika, jamii isiyo na usalama huvuruga misingi ya mshikamano wa kijamii. Ni dhahiri kwamba wanajamii ambao Wanaendeleza vitendo kama vile wizi wa mifiigo, unyakuzi Wa ardhi, ubakaji, na ulawiti hupalilia zaidi utengano miongoni mwao.
Vitendo hivi huzua chuki, kisasi, kutoaminiana na mara nyingine husababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe. Katika hali hii baadhi ya raia huumizwa, wengine hufa n’a Wengine kuachiwa majei-aha ya moyo.
Tatizo la ukosefu wa usalama linapozungumziwa, watu moja kwa moja huwanyooshea vidole polisi na walinda usalama wengine.
Raia kwajumla huwa wepesi kusema,“Tunai sihi serikali imhakikishie usalama.” Jambo la kusikitisha ni kwamba wanaoiomba serikali kuwahakikishia usalama ndio kwa mfano, wanaojenga kando ya mito na kujifia katika hatari ya kusombwa na maji. Wengine wanatarajia serikali kuwahakikishia usalama huku wakiabiri magari yaliyojaa watu pomoni bila kuwazia hatari inayowakabili.
Wapo wengine ambao huhatarisha usalama wao kwa kunywa pombe haramu na kuambulia upofu. Wengine nao hula vyakula vyenye kemikali zinazoathiri afya zao. Wapo Wengine wanaojitia hatarini kwa kupuuza wito wa serikali wa kuhakikisha kuwa wamcjua anayeishi karibu nao, na kwamba wamewaangaza Wale ambao wanashukiwa kuwa pingamizi kwa usalama.
Isitoshe, kuna Wale ambao huhatarisha usalama wao kwa kutumia njia za kijadi za matibabu kama vile akjna mama kujifungulia nyumbani bila Wakunga maalum; jambo ambalo huhatarisha maisha ya Inzazi na mtoto pia.
Wengine hushiriki, vitendo viovu kama vile utunguaji mimba na kujisababishia vifo. Ni dhahiri kwamba kudumishwa kwa usalama kunahitaji mchango wa kila mwanajarnii.
Kama kila mtu angejifunga masombo kushughulikia usalama wake na wajirani, huenda hakungekuwa na haja ya polisi na hata walinda lango.
31.Kulingana na aya ya kwanza:
A. Mzazi asiyewalinda wanawe hupoteza hadhi yake kama mlezi.
32.Vita vya kikabila:
C. huwafanya watu hupoteza heshima yao;
33.Aya ya tatu imeonyesha kwamba:
B. Tamaa inasababisha ukosefu wa usalama katika j amii.
34.Kulingana na kifungu, athari za ukosefu wa usalama ni:
C. kushuldana, uharibifu wa mali;
35.Mwandishi amedhihirisha kwarnba:
A. Walinda usalama huelekezewa lawama baada ya uhalifu kutokea.
36.“Wanaoiomba serlkali kuwahakikishia usalama ndio kwa mfano, wanaojenga kando ya mito na kujitia katika hatari ya kusombwa na maji.”
Onyesha methali inayoweza kutumiwa kuwaonya watu hawa.
C.Ukibebwa usilevyelevye miguu.
37.Ni wazi kwamba kudumisha usalama kunahitaji:
C. uwajibikaji Wa mtu binafsi katika shughuli zake;
38.Kulingana na kifimgu serikali:
D. inawahimiza watu kujua mienendo ya majirani wao.
39.Wazo kuu linalojitokeza katika aya ya mwisho, ni:
C. Ni muhimu mtu kujitahidi kuhakikisha usalama kwake na katika mazingira yake.
40.Chagua maana ya kindakindaki kwa mujibu wa kifilngu.
A. waliozaliwa hapo
Somu kifungu kwmtacho kisha ujibu maswali 41 mpaka S0.
Siku hiyo jua lilichomoza mapema kuliko kawaida. Niliitazama miale yake kupitia kwenye dirisha la chumba changu. Rangi ya mialc hii iliibua rnjadala moyoni mwangu.
“Sijui kama macho yangu ndiyo yanayonipiga chenga, ila naona leo miale hii ina mabaka meusi yaliyolwaa wekundu wa damu,” moyo Wangu ukasema. “Ingawa mimi si mnajimu wala mshirikina, nadhani rangi hii imefumbata kitendawili fulani,” moyo ulirudia kusema. Baada ya mawazo haya nilishusha pumzi ndefu na kusema, “Siku njema huonekana asubuhi, huenda hii ni dalili ya wema wenyewe.
Juu ya hayo mustakabali wa siku umo mikononi mwake aliyciamrisha siku yenyewe kuwepo, bindamu ana hiari au usemi gani kuhusu yatakayokuwa au yatakayokosa kuwepo? Nilijikokota kutoka kitandani mwangu.
Siku hii nilikuwa na miadi na rafiki yangu Tindi ambayc alihitaji kununua vifaa vya nyumbani.
Rafiki huyu alikuwa kapata kazi ya uhasibu katika Shirika Ia Utozaji Ushuru baada ya kipindi cha kuhangaishwa na ulaji rushwa. Alikuwa anagura alikoishi na wazazi wake.
Kama alivyosema, alitaka kuishi peke yake ili ajifunze kujitegemea, Tulikuwa tumepanga kukutana katikajcngo moja la kibiashara ambamo mliuzwa aina nyingi za vifaa vya nyumbani.
Nilifika kwenye jengo hilo baada ya saa moja na nusu. Nilirnngojea rafiki yangu kwa takriban saa mbili ingawa alikuwa ameahidi kufika mapema.
Hata hivyo, kuchelewa huku hakukuwa ibra kwangu. “Vipi Bwana? Leo umczidi?” Nifimuuliza Tindi. “Samahani sana ndugu, ila wewe unajua katika mji wa Selea methali, ‘Chelewa chclcwa utampala mwana si wako’, haiwezi kuafiki.
Hata mm ukataka kuchapuka vipi, msongamano wa magari umkutilia vizingiti,” alijibu kama kawaida yaks. Tulijitoma katika shughuli ya ununuzi. Mara, “Leta hiki,” mara, “Rudisha, hiki ni ghali mno,” mara, “Punguza bei.” Hata baadaya muda usiopungua saa tano na nusu, tulikuwa tumenunua vyote vilivyokuwa kwenye orodha yetu ya bidhaa. Ghafla taa za umeme zilizimika, mlio wajenereta ukasikika, kisha mlipuko, na kiza cha kutisha. Mara nilisikia ukemi mkubwa uliopasua dari ya jengo hili. Ukemi huu ulifuatwa na sauti nenc ya kiume, “Fungeni vishubaka vya pesa! Nenda kafunge mlango wa mbele na wa nyuma!” Wakati hayo yote yakijiri, jumba lilikuwa limekumbatiwa na moto wa tanuri.
Joshi jeusi lilitanda kila mahali, vilio vya wateja waliokuwa wanatapatapa huku na huko kama kuku aliyedenguliwa shingo viliyaremba mandhari haya. Nilimshika Tindi mkono na kukimbilia mlango wa nyuma ambamo alisimama mlinda lango mmoja kuhakikisha hatubebi bidhaa yoyote; hata zile tulizokuwa tumelipia.
Nilijaribu kumsihi atufungulie tutoke lakini akakataa katakata. Amri ya Bwana Mkubwa ilimzuia hata kuona hatari iliyomkabili yeye. Hatimaye nilifanikiwa kutumia misuli yangu kumwondoa, nikajishukuru kwa mazoezi ya viungo ambayo mimi hufanya kila siku.
Mimi na Tindi tulifanikiwa kutoka nje bila majeraha ya haja. Ndani kule vilio vya roho zilizokuwa zikibanania kwenye mlango wa nyuma vilihanikiza. Bwana Mkubwa alikataa katakata kufimgua mlango Wa mbele; anahofia mali yake kukwepuliwa na wafu! Wapo walionusurika, wakapitia kwenye mlango huu, wapo waliosalimu amri ya moto, moshi, hewa yenye sumu na kubanwa na wenzao.
Hata Shirika la Zimamoto lilipowasili baada ya saa nne, jengo hilo lilikuwa majivu pamoja na vyote vilivyokuwcmo.
Runinga ya Taifa usiku huo iliarifu kwamba hata mwenye jengo aliyesimama wenye mlango wa mbele kulinda mali yake dhidi ya roho zilizokuwa zinateketea aliaga dunia.
41.Miale ya jua asubuhi hii:
B. llimfanya Msimulizi kufikiri zaidi.
42.Aya ya kwanza imedhihirisha kwamba:
C. Binadamu hana mamlaka kuhusu hali inayoyaathiri maisha yake.
43.Chagua jibu lisilo sahihi kwa mujibu wa kifungu.
A. Msimulizi anajua hii ni mara ya pili Tindi kuchelewa.
44.Kauli, “Hata hivyo kuchelewa huku hakukuwa ibra kwangu”, inamaanisha:
A. Aghalabu Tindi hazingatii muda waliokubaliana kuanza shughuli.
45.Chagua mfuatano ufaao wa matukio kulingana na taarifa.
A. kuagiza bidhaa, kujadiliana bei, kupotea kwa umeme, mpasuko, giza nene;
46.Chagua sifa kuu za mwenye jengo kulingana na kifungu.
B. mwenye tamaa, asiyewajibika
47.Chagua jibu ambalo si sahihi kwa mujibu wa kifungu.
D.Sheria zitolewazo wanapoiba huweza kudhibiti waokoaji.
48.Aya ya mwisho imebainisha kwamba:
C.Uharibifu mkubwa ulisababishwa na kutochukua hatua haraka.
49.Chagua kisawe cha kumsihi.
A. kumrai
50.“Hata mwenye jengo aliyesimama kwenye mlango wa mbele kulinda mali yake dhidi ya roho zilizokuwa ziuateketea aliaga dunia.”
Chagua tamathali mbili za usemi zilizotumiwa katika kauli hii.
B. kinaya,nahau
I wish to get the marking scheme
I wish to get the macking scheme
Making scheme please