Welcome to Ugfacts.net/ke. On this page you will find details on the following topics

KUCCPS Admission Letters KUCCPS Student Portal KUCCPS Admission Lists
FREE KNEC KCSE Past Papers FREE KNEC KCPE Past Papers List of All Past Papers 
Fees Structure for 2024-2025 KNEC KCPE KNEC KCSE
Intakes and Admissions 2024-2025 List of Courses Offered Latest Jobs in Kenya 2024-2025
TVET Applications 2024-2025 TSC KNUT
KDF Recruitment Kenya Police Recruitment Kenya Prisons Service Recruitment

Your Opinions and Questions Matter. Kindly leave your comments below and we shall attend to you promptly.

KNEC KCPE Past Papers Kiswahili 2011

KNEC KCPE Past Papers Kiswahili 2011

 

 

Kenya National Examination Council

K.C.P.E 2011

Sehemu ya pili

Insha

Namba yako ya mtihani

Jina lako

Jina la shule yako

Soma Maagizo Haya Kwa Makini

1. Kwenye nafasi zilizoachwa hapo juu andika Namba yako kamili ya mtihmi, Jina lako na Jina La Shule yako.

2. Sasa fungua karatasi hii, soma kichwa cha insha kwa makini na uandike insha yako kwenye nafasi ulizoachiwa

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa. Mwandikie rafiki yako barua kuhusu namna ya kujiandaa vyema kwa mtihani wa K.C.P.E.

 

 

Kenya National Examination Council

K.C.P.E 2011

Kiswahili

Paper

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Wakazi wa vitongoji duni -1 na matatizo mengi. Asilimia kubwa ya waja hapa -2 -3 aila. 4_, katika mitaa ya mabwanyenye -5 na vitongoji hivi, hali ni tofauti; majumba yenye kuvutia yamepamba mazingira humo. Maisha ya makundi haya mawili _6. Wana wa matajiri hupata mahitaji _7 huku maskini -8 kwa ukosefu. Ama kwa kweli _9.

1. A wametwaliwa B. wamekabiclhiwa C. wametengwa D wametingwa

2. A haiwezi B. hawawezi C. haziwezi D hamuwezi

3. A kumkimu B. kuzikimu C. kujikimu D kuwakimu

4. A Labda B.Kwa hivyo C. Hata hivyo D Ingawa

5. A waliyopakana B.iliyopakana C. uliyopakana D. yaliyopakana

6. A yamebaidika kama ardhi na mbingu. B. yamcadimika kama wali wa daku.

C. yameingia kati kama mchuzi wa ugali. D. yamejikaukia kama ukuni.

7. A zote B. yme C. nyote D. sote

8. A wakila mwata B. wakila mwande C. wakila yamini D. wakila hasara

9. A dua la kuku halimpati mwewe B. bidii ya mja haioudoi kudura

C. dau la mnyonge haliendi joshi D. mtegemea nundu haachi kunona

Tina alijua kwamba alihitaji kutia bidii masomoni asije -10 shule. Kijijini mwao ilikuwa kawaida wasichana _11 nafasi katika elimu. Palipotokea uhaba _12 karo. masomo ya msichana _13 huku mvulana akiendelea na elimu. Mara hii Tina aliamua kulia bidii ili angaa Mwalimu Mkuu amtafutie mhisani _14. Kwa njia hii Tina -15 namna fulani ya kuliokoa tabaka lake.

10 A. akaachishwa B. akaachiwa C. akaachilia D. akaachia

11. A. kunyanyaswa B. kubadilishiwa C. kudhulumiwa D. kupunguzwa

12. A. ya B. kwa C. wa D na

13. A. yangekatizwa B. yanakatizwa C. yakikatizwa D. yakakatizwa

14. A. ayathamini masomo yake B. amthamini masomo yake

C.amdhamini masomo yake D. ayadhamini masomo yake

15. A. alitarajia alipata B. alijihimu alipata C. alijihimu kupata D. alitarajia kupata

Kutoku swali la 16 mpaka 30. chagua jibu lililo sahihi.

16. Sentensi inayounganisha sentensi: “Juma ni mzee. Juma anzsoma kitabu bila kisahihi ni:

A. Juma ni mzee maadamu anasoma kitabu bila miwani.

B. Juma anasoma kitabu bila miwani licha ya kuwa yeye ni mzee.

C. Juma ni mzee madhali anasoma kitabu bila miwani.

D. Juma anasoma kilabu bila miwani minghairi ya yeye m mzee.

17. Ki katika sentensi; “Mwanafunzi huyo akikuona atatembea kijeshi”, imetumiwa kuonyesha:

A. Masharti. nomino.

B. Wakati, nomino.

C. Masharti. namna.

D. Wakati, namna.

18. Chagua neno ambalo limetumia silabi changamano:

A. Mbuga.

B. Kituta.

C. Ziwa.

D. Utulivu.

19. Kamilisha, ‘Fahamikiana kama— ‘

A. sahani na kawa

B. kinu na mchi

C. pua na mdomo

D. tui na maziwa.

20. Chagua sentcnsi yenye vivumishi:

A Mwashi amcjcnga nyumba juu ya mlima.

B. Yule aliimba vizuri mno akatuzwa

C. Nokoa atafika hapa hivi punde.

D. Wanafunzi wengi walifaulu mtihani huo.

21. Ni sentensi ipi ambayo imetumia “kwa‘ kuonyesha sehemu ya kitu?

A. Alitembea moja kwa moja hadi shuleni.

B. Wazee kwa vijana walihudhuria sherehe hiyo.

C. Watu watatu kwa kumi huepuka mitego.

D. Mnnika alipongczcwa kwa wazazi wake.

22. Mkono wazi ni kwa ukarimu ilhali ni kwa inda.

A. jicho la nje

B. joka la mdimu

C. kifauongo

D. kisebusebu.

23. Chagua kifaa cha uhunzi A. fuawe

B. patasi

C. limazi

D. chetezo

24. Ni kundi Iipi lenye sauti ghuna pekee?

A. p, t, z

B. v, th, n

C. sh. l. w

D. b, d. g.

25. Wingi wa, ‘Kiduka hichu kilifunguliwa jana‘. ni:

A. Maduka hizo zilifunguliwa jana.

B. Viduka hizo zilifunguliwa jana.

C. Viduka hivyo vilifunguliwa jana.

D. Maduka hayo yalifunguliwa jana.

26. Ni sentensi ipi sahihi?

A. Hewala! Nitakusaidia.

B. Kefule! Naomba maji.

C. Oyee! Tumeshindwa.

D. Hamadi! Amekuja.

27. Miaka mia ni kwa kame ilhali vitu ishirini ni kwa

A. kikwi

B. korija

C. mwongo

D. lukuki.

28. Chagua sentensi yenye kiwakilishi cha idadi:

A. Mwanafunzi aliyefika kwanza alimpata mwalimu wa pili darasani.

B. Mwalimu aliyetufunza mwanzoni alituulira swali moja mara mbili.

C. Mwalimu aliyetufunza mwanzoni alitufafanulia mambo kadha ya kutufaa.

D. Mwanafunzi aliyefika kwanza alipewa medali na wa pili akapewa kitabu.

29. Ni sentensi ipi ambayo imetumia sitiari? A. Mwakio ni sungura siku hizi.

B. Moyo wake ulimwambia asirudi nyuma.

C. Muuguzi alisema atajifungua salama.

D. Nyaboke ni mpole kama njiwa.

30. lkiwajuzi ilikuwa Jumamtu. Jumamosi itakuwa: A. Kesho

B. Mtondo

C. Mtondogoo

D. Kceshokutwa.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 – 40.

Mfumo wa elimu nchini unatilia mkazo mafunzo mengine ambayo, japo yamo nje ya masomo ya kawaida, yanahusiana na kwenda sambamba na masomo hayo ya kawaida. Vyama vya wanafunzi shuleni vinachangia pakubwa kupitisha mafunzo hayo ya ziada

Vyama vya wanafunzi hutofautiana kulingana na majukumu. Mathalani, vipo vyama vya kidini, vya kitaaluma na vya michezo. Pia, kuna vyama vya kijamii kama vile Chama cha Kupambana na Matumizi Mabaya ya Dawa na vya kiuchumi kama vile Chama cha Wakulima Chipukizi.

lmedhihmka kwamba vyama vya wanafunzi vina . Hii ndiyo sababu shuleni, kila mwanafunzi anahimizwa kujiunga na angaa vyama viwili. Vyama vya wanafunzi huwasaidia kukuza vipawa na kuimarisha stadi za kujieleza. Haya hufikiwa kupitia kwa shughuli za vyama kama vile ukariri wa mashairi, mijadala, utegaji na uteguaji vitendawili, chemsha bongo na ulumbi. Aidha, vyama hivi huhimiza utangamano miongoni mwa wanachama kwani wao hujiona kuwa watu wenye mwelekeo mmoja. Vilevile utangamano wa kimifa na kimataifa hujengeka.

Mwanafunzi ambaye amejiunga na vyama vya wanafunzi huweza kukabiliana na changamoto za maisha kwa urahisi kuliko yule ambaye hajawahi kujiunga na chama chochote. Katika vyama hivi. wanafunzi hufunzana mikakati na maarifa ya kutatua matatizo na mbinu za kuepuka mitego ya ujana. Kupitia kwa‘ ushauri wa marika kwa mfano, mwanafunzi hushauriwa kuhusu masuala kama vile uteuzi wa marafiki, kuratibu muda, kujikubali na kuwakubali wenzake.

Hali kadhalika, mwanafunzi hujifunza maadili ya kijamii na kidini. Kupitia kwa vyama vya kidini na vinginevyo, yeye hujifunza kujistahi na teuwa na stahamala ya kidini, kiitikadi na kikabila. Kadhalika, majukumu ambayo mwanafiinzi huenda akapewa hupalilia uwajibikaj i. uaminifu na kipawa cha uongozi. Hata anapohitimu masomo yake, mwanafunzi huyu huendeleza sifa hizi.

Vijana wana nafasi kubwa katika kukabiliana na maovu ya kijamii kwani wao ndio wengi zaidi. Kupitia kwa vyama hivi, wanafunzi wanawcza kuwahamasisha wenzao dhidi ya labia hasi kama vile kushiriki mapenzi kiholela, ulanguzi wa dawa za kulevya na kujiingiza katika burudani zisizofaa. Pia, shughuli na miradi ya vyama hivi huwawezesha wanafunzi kutumia nishati zao kwa njia ya kujinufaisha na kuepuka maovu. Kwa mfano, wanaweza kwenda kukwea milima, kufanya matembezi ya kukusanya pesa za kuwafadhili wahitaji, kuendeleza shughuli za kunadhifisha mazingira na kutembelea vituo vya mayatima na wazee.

Kushiriki katika vyama vya michezo hakumwczeshi mwanafunzi kuimarisha afya na kujenga misuli li, bali pia huweza kuwa msingi wa kupata chanzo cha riziki baadayc. Wapo wachezaji maarufu ambao walitambua na kuviendeleza vipawa vyao kupitia kwa vyama vya aina hii. na hivi sasa wana uwezo wa kuyaendcsha maisha yao na ya familia zao.

Ifahamike kuwa vyama vya wanafunzi vinapaswa kuwa msingi wa mshikamano na maridhiano. Visitumiwe kama vyombo vya kuwagawa wanafunzi kitabaka. Mwanafunzi hana budi kusawazisha muda anaotumia. Atenge muda wa shughuli za vyama na wa kudurusu masomo yake.

31. Kulingana na kifungu, mwanafunzi akiwa shuleni:

A. Hufunzwa mfumo sambamba, hufunzwa kupirisha mafunzo ya ziada B. Hujiunga na vyama, hujifunzz mfumo sambamba C. Hufunzwa mfumo sambamba, hufunzwa laaluma ya vyama D. Hujiunga na vyarna, hujifunza taaluma mhalimbali.

32. Katika aya ya pili, wazo kuu analozungumzia mwandishi ni:

A. Aina za vyama vya kijamii

B. Majukumu ya vyama vya wanafunzi

C. Aina za vyama vya wanafunzi

D. Majukumu ya vyama vya kijamii.

33. Chagua jibu lisilo sahihi kwa mujibu wa taarifa. A. Vyama vya wanafunzi huchangia kukuza ubunifu wa wanafunzi.

B. Vyama vya wanafunzi huchangia kukuza uzalcndo wa kimataifa.

C. Vyama vya wanafunzi huwasaidia kuimarisha uzalendo na mahusiano mema.

D. Vyama vya wanafunzi huwasaidia kuimarisha uhusiano na nchi nyingine.

34. Kifungu kinaonyesha kuwa ushauri na uelekezaji:

A. Ilumwezesha mwanafunzi kujithamini.

B. Humsaidia mwanafunzi kupata marafiki.

C. Humwandalia mwanafunzi mipango ya kazi

D. Humwondolea mwanafunzi mitego.

35. Kwa mujibu wa taarifa_ jibu linalodhihirisha maana ya melhali, “Ukiona vyaelea vimeundwa,” ni:

A. Wanafunzi wakipewa nafasi ya uongozi huheshimu mielekeo ya wengine.

B. Wanafunzi wakipewa nafasi ya uongozi hujislahikj na kustahimili wcngine.

C. Wanafunzi wakipewa nafasi ya uongozi huhimiza stahamala ya kidini baadaye.

D. Wanafunzi wakipewa nafasi ya uongozi huwa wa kutegemewa baadaye.

36. Kulingana na kifungu, vijana wanaweza kudhihirisha uwajibikaji katika jamii kupitia:

A. Kuwapinga walanguzi wa dawa za kulevya na kuepuka burudani.

B. Kufanya matembezi anuwai ya kukusanya pesa.

C. Kushikiki katika miradi ya kuwaauni wanyonge.

D. Kuendeleza shughuli za kuhifadhi mazingira na kutembea milimani.

37. Kifungu kimebainisha kuwa: A. Vijana ndio wanaoweza kushiriki mapenzi kiholela.

kuslawisha vituo vya wahitaji.

C. Vijana wanaweza kulumiwa kama msingi wa kuadilisha jamii pana.

D. Vijana ndio wanaoweza kukabiliana na matatizo ya kijamii.

38. Chagua jibu sahihi kulingana na kifungu A. Michezo huweza kumjengea mtu jina na kumwimarisha kiuchumi.

B. Wachezaji maarufu walianza kucheza walipojiunga na vyama.

C. Wachezaji maarufu walianza kugundua vipawa vyao walipojiunga na vyama.

D. Michezo huweza kumjengea mtu uwezo na kumwimarisha kiuchumi

39. Maoni ya mwandishi katika aya ya mwisho ni kwamba:

A. Vyama vya wanafunzi vinaweza kuvuruga usawa katika jamii.

B. Vyama vya wanafunzi ndio msingi wa kumsaidia mwanafunzi kutumia muda wake darasani.

C. Vyama vya wanafunzi vinaweza kuvuruga masomo katika darasa.

D. Vyama vya wanafunzi ndio msingi wa kuimarisha umoja na maelewano katika jamii

40. Kulingana na kifungu, ‘manufaa ya kuhusudiwa ni:

A. manufaa yanayowafaidi wengi

B. manufaa yanayowavutia wengi

C. manufaa yasiyosahaulika kwa urahisi

D. manufaa yasiyopatikana kwa urahisi.

 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.

Naikumbuka siku hiyu vizuri. Niliamka alfajiri mbichi tayari kuanza safari kutoka kijijini mwetu hadi Mji Mkuu. Hii ndiyo iliyokuwa mara yangu ya kwanza kuuzu mji huu. Moyoni nilikuwa na bashasha isiyokuwa ya kawaida kwa sababu siku hiyo ningcuona mji ambao sifa lake nilikuwa nikizisikia tu kutoka kwa wenzangu waliobahatika kuulcmbelea. Hamu ya kuona majengo marefu, barabara zilizosakifiwa, magari mengi, watu wa asili mbalimbali na mabustani ya starehe ilinigubika. uikawa sijifai kwa matumaini.

Nilitembea hatua chache hadi kituo cha mabasi, nikapata daladala moja iliyotoza nauli nafuu, nikaiabiria mpaka mji uliokuwa pua na mdomo kutoka kitongojini mwetu. Hapo nilirumainia kupata matwana ya kusafiria hadi Mji Mkuu. Kwenye stcsheni kulikuwa na msongarnano wa matwana na harakati za utingo waliokuwa waking’ang‘ania abiria. Nikaingia katika marwana moja iliyoitwa Upcpo. Nilikuwa abiria wa kumi na mbili kuingia. Buada ya dakika tano hivi, gari lilijaa abiria, Wore kumi na wanne. Tukang’oa nanga. Mandhari ya kupendeza yalijikunjua mbele yangu. Upepo mwanana kupilia dirishani. mpito wa kasi wa miti. mazigazi ….vyote vilishirikiana kunipumbaza kiasi cha kunisahaulisha kufunga mkanda wa usalama.

Baada ya robo saa utingo alidai nauli. Nikapeleka mkono kwa tahadhari kwenye kibindo changu ambamo nilikuwa nimezifutika hela za usafiri na masurufu. Nikaloa noti ya shilingi mia mbili na kumkabidhi utingo huku nikitarajia baki. Utingo alinikazia macho, akanyoosha mkono na kusema, “Mia midi!“ Nikarudi tena kwenye kibindo, nikama noti mbili za shilingi hamsini na kumpa. Safari ikaendelea.

Tulipofika mji mdogo wa Pilia, matwana ilisimama. Utingo aliinama chini ya viti, akaloa vibao na kuviweka baina ya viti vya kawaida. Kisha akaanza kutangaza. “Wa Jiji na mia; mia hamsini”. Abiria walioonekana kuwa wachovu kwa kungojea na kupigwa na mzizimo wa kipupwe walipigana vikumbo kuingia. huku utingo akiwaelekeza kwenye vile vibao. Vili vilivyotcngenezewa abiria watatu vikaishia kubeba abiria Watano Matwana nayo ikawa haina budi kuslahimili uzito wa abiria ishirini na watalu. Tukawa tunabanana kweli kweli. Utingo naye alining’inia mlangoni. shati lake lapeperushwa na upepo. Nilipojaribu kulalamikia hali hii nilinyamazishwa hata na abiria wenzangu.

Gari Iikaanza mwcndo tena huku likicndctshwa kwa kasi ya umeme. Abiria waliokuwa wakizungumza sasa walinyamaza. kila mmoja roho i mkononi. Kimya cha kaburi kikatawala hadi pale utingo alifiomwambia dereva. “Weka ngoma.“ Muziki ukahanikiza hewani kwa fujo. Baadhi ya abiria wakaanza kuyumbisha vichwa kwa kufuata mdundo wa muziki ambao ulitishia kuvipasua viwambo vya masikio yangu.

Njiani tulikutana na waiinda usalama ambao walilusimamisha. Utingo alishuka na kwenda chemba na mmojawapo wa hao maafisa kisha akarudi huku kipaji chake kimenawiri kwa tabasamu. Akasema, “Nimempaka mafuta viganjani.” Baadhi ya abiria walitikisa vichwa, wengine wakacheka kama kwamba wameona kinyago. Mimi nilibaki kuduwaa tu. Gari liliongeza mwendo na baada ya muda mfupi lukafika kwenye mji mmoja ambao ulikuwa na majcngo makubwa makubwa. Nikadhani tumcfika Mji Mkuu. Nilipomuuliza abiria jirani aliniambia kuwa huu ulikuwa tu mji mkuu wa Jimbo la Buraha. Tukazidi kuyakunja rnasafa ya safari hii kwa kasi ya kuogofya huku dercva akitafuna majani aliyokuwa akiyatoa mfukoni mwa shati lake. Kadiri alivyoyatafima ndivyo alivyozidisha kasi. Nikahisi kama gari linapaa juu angani. Nikataka kumwambia dereva jambo, lakini nikajiasa, “Ikiwa wengine wamenyamaza sembuse mimi?“

Baada ya kitambo kidogo mvua ilianza kunyesha. Kukawa na ukungu na utelezi barabarani. Abiria mmoja alimsihi dereva kupunguza mwendu Haya hayakumgusa dereva mshipa. Aliongeza kasi kana kwamba hajasikia lolote. Gari Iilifika kwenye kuruba. dereva akawa haoni vizuri. Ghafla nikasikia, “Kirrr..!“ Kisha_“Mungu wangu!” Halafu, ‘ngu!’

Kiza cha kaniki kitanda.

41. Kulingana na kifungu;

A. Wcnzake Msimulizi waliwahi kfipata fursa ya kuishi kalika Mji Mkuu.

B. Barabara za Mji Mkuu hazina mashimo.

C. Mji Mkuu una majumba mengi marefu.

D. Msimulizi ana mwao na hali ilivyo katika Mji Mkuu.

42. Chagua jibu sahihi kuhusu vituo vya magari kwa mujibu wa aya ya pili:

A. Wasafiri wengi kushindania nafasi

B. Magari mengi kushindania wasafiri

C. Misongamano mingi ya kumngazia wasafari

D. Shughuli nyingi za kunadia nafasi.

43. Mazingira ya kuvutia yalimwathiri Msimulizi kwani: A. Aliduwaa na kujisahau.

B. Alifurahia upepo na kujisahau.

C. Alizubaa na kupuuza sheria za usafiri.

D. Alipumbaa na kupinga sheria za usafiri.

44. Msimulizi alikuwa amehifadhi pesa katika:

A. Mfuko mdogo ndani ya suruali.

B. Mfuko mdogo mbclc ya suruali.

C. Mkuko wa nguo iliyoshonwa kiunoni.

D. Mkunjo wa nguo uliofimgwa kiunoni.

45. Katika mji wa Pitia abiria walipigana vikumbo kuingia garini kwa sababu:

A. Kulikuwa na uhaba wa magari.

B. Kulikuwa na uhaba wa viti.

C. Walikuwa wamechoka kungojea matwana

Upepo.

D. Walikuwa wamepigwa na baridi na mvua.

46. Kulingana na kifungu. ajali barabarani husababishwa na:

A. ukosefu wa magari, kubeba abiria wengi.

B. kiburi cha madereva. kutozingatia maelekezo barabarani.

C. ukosefu wa mikanda ya usalarna, madereva kutowajibika.

D. muziki wa kupasua viwambo. madereva kutoona vizuri.

47. Msimulizi ni mkakamavu kwa vile:

A. Alishutumu hali ya gari kubeba abiria kuliko kiasi.

B. Alishutumu hali ya shati na utingo kuning‘inia nje.

C. Alinyarnaza alipoona dereva akikaribia kuruba kwa kasi.

D. Alinyamam alipoona utingo akienda chemba na afisa.

48. Chagua jibu lisilo sahihi kulingana na kifungu:

A. Abiria wengine waliufurahia muziki garini.

B. Ufisadi unaweza kusababisha ajali barabamni.

C. Abiria wanaweza kuzuia ajali barabarani.

D. Kuruba ndiyo iliyosababisha ajali garini.

49. Ni mfuatano upi wa matukio ufaao kwa mujibu wa kifungu? ‘

A. Kucheza muziki, kukutana na polisi, kufikia kuruba, mvua kunyesha, kupata ajali

B. Kukutana na polisi, kuhonga, kucheza muziki, kufikia kuruba, kupata ajali

C. Kuchezz muziki, kukutana na polisi. kuhonga, kufikia kuruba, kupata ajali.

D. Kukutana na polisi, gari kupaa juu. mvua kunyesha, kufikia kuruba, kupata ajali.

50. ‘Kiza cha kaniki kitandani’; kulingana na kifungu ina maana:

A. Msimulizi akapoteza fahamu.

B. Msimuiizi akapoteza uwezo wa kuona.

C. Kukawa na weusi mkubwa.

D. Kukawa na giza totoro.

 

 

Free KNEC KCPE Past Papers Kiswahili 2011 Marking Scheme/Answers

KCPE 2011 ANSWERS

# Kiswahili

1 D

2 A

3 B

4 C

5 B

6 A

7 B

8 A

9 C

10 A

11 C

12 C

13 A

14 D

15 D

16 B

17 C

18 A

19 B

20 D

21 C

22 B

23 A

24 D

25 C

26 A

27 B

28 D

29 A

30 B

31 D

32 C

33 B

34 A

35 D

36 C

37 C

38 A

39 A

40 B

41 D

42 B

43 C

44 D

45 A

46 B

47 A

48 D

49 C

50 A

2 thoughts on “KNEC KCPE Past Papers Kiswahili 2011”

Leave a Comment