Welcome to Ugfacts.net/ke. On this page you will find details on the following topics

KUCCPS Admission Letters KUCCPS Student Portal KUCCPS Admission Lists
FREE KNEC KCSE Past Papers FREE KNEC KCPE Past Papers List of All Past Papers 
Fees Structure for 2024-2025 KNEC KCPE KNEC KCSE
Intakes and Admissions 2024-2025 List of Courses Offered Latest Jobs in Kenya 2024-2025
TVET Applications 2024-2025 TSC KNUT
KDF Recruitment Kenya Police Recruitment Kenya Prisons Service Recruitment

Your Opinions and Questions Matter. Kindly leave your comments below and we shall attend to you promptly.

Free KNEC KCPE Past Papers Kiswahili 2014

Free KNEC KCPE Past Papers Kiswahili 2014

 

 

Free KNEC KCPE Past Papers Kiswahili 2014

Maswali 1 mpaka 15.

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Usalama ni jambo ————— kudumishwa kwa dhati; yaani —————–. Wizara husika L kiasi maalum cha fedha kwenye bajeti ya taifa ili kugharamia shughuli za usalama. shughuli hizi ni kuwapa askari——————- za kukabiliana na wakiuka sheria. ——————; uhifadhi wa usalama haupaswi kuachiwa polisi na Wanajeshi pekee. Kila mwananchi sharti awajibike kupalilia amani; si kwa heri, si kwa shari, si kwa fanaka, si kwa —————–; Wanajamii Wote —————kukabiliana kila Wakati na mtu yeyote anayezua vurugu.

1. A. Iinaostahili B. unaostahili C linalostahili D. unalostahili

2. A. kwa uaminifu B. kwa nia C kwa ustadi D. kwa hamu

3. A. ikitengewa B. ingetengewa C. inatengewa D. ikatengewa

4. A. Baadhi ya B. Kati ya C. Mkabala na D. Pamoja na

5. A. hekima B. mikakati C. ilhamu D. stadi

6. A. Papo kwa papo kamba hukata jiwe B. Chombo hakiendi ila kwa kafi

C. Bahari haivukwi kwa kuogclca D Kinga na kinga ndipo moto uwakapo

7. A. ukosefu B. shauku C.sikitiko D. uchungu

8. A. wapigc darubini B. wakae angc C.Wakae tutwe D. Wapige hema

Mweledi alipojiunga na shule ya chekechea walimu wake walitambua kuwa alikuwa na kipawa cha————— Baada ya muhula mmoja tu, aliweza kusimama jukwaani kukariri na kughani mashairi ya ————–10 , yaani ycnye mishororo mitatu katika kila ubeti; walimu na wanafunzi Wenzake Wakawa ndio —————– yake. Walimu Walimpa mazoezi zaidi ili————— 12 . Kadhalika, Mweledi ——————13 masomo kiasi kwamba katika darasa la tano aliweza kutambua aina za vivumishi kama vile: ————–14 , pamoja na akisami kama sudusi tatu ambayo kwa tarakimu ni —————————-15 .

9. A. kigeni B. kipekee C. kihalali D.. kiasili

10. A. tathnia B. tarbia C. tathlitha D.. takhmisa

11. A. halaiki B. msoa C.mashabiki D. hadhira

12. A. aimarike B. waimarishe C.aimarishe D.waimarike

13. A. aliuthamini B. alizithamini C.aliyathamini D. aliithamini

14. A. ajabu, mwelna,jepesi B. hodari, tano, matamu

C. kiasi, tena, vile D. lake, laini, mno

15. A. 6/3 B. 9/3 C.3/6 D. 3/20

swali la I6 mpaka 30, chagua jibu lililo sahihi.

16 Kukanusha kwa: ‘Mtumbwi ambao ulinunuliwa

umeanza safari‘, ni:

A. Mtumbwi ambao ulinunuliwa haukuanza safari.

B. Mtumbwi ambao haukununuliwa haujaanza safari.

C. Mtumbwi ambao ulimmuliwa haujaanza safari.

D. Mtumbwi ambao haukununuliwa haukuanza safari.

17 Chagua usemi halisi wa sentensi ifuatayo:

Mwenesi alimwambia ndugu yake kuwa Wangeenda Mombasa siku ambayo ingefuata.

A. “Kesho mtaenda Mombasa.“ Mwenesi

alimwambia ndugu yake.

B. “Siku iliyofuata mlienda Mombasa.” Mwenesi alimwambia ndugu yake.

C. “Kesho utaenda Mombasa.” Mwenesi alimwambia ndugu yake.

D. “Siku iliyofuata ulienda Mombasa.

“ 18. Mwenesi alimwambia ndugu yaks.

Chagua wingi wa sentensi ifuatayo: Mruka kiunzi alipongezwa aliponyakua nishani hiyo.

A. Waruka viunzi walipongczwa waliponyakua nishani hiyo.

B. Waruka viunzi walipongezwa Waliponyakua nishani hizo.

C. Mruka viunzi alipongezwa aliponyakua nishani hiyo.

D. Mruka viunzi alipongezwa aliponyakua nishani hizo.

19. Ikiwa mtondogoo itakuwa Jumanne, ko ni:

A. Jumamosi

B. Alhamisi

C. Ijumaa

D. Jumatano.

20. Chagua sentensi yenye kiwakilishi kimilikishi.

A. Mzazi wake alihudhuria sherehe Iakini wangu hakuhudhuria.

B. Mtoto wao aliamka mapema lakini huyu alichelewa.

C. Mfanyakazi wa tatu alistaafu lakini wengine walibakia.

D. Msafiri wa nne alipata kibali lakini waie hawakupata.

21. Natu ameolewa na John. Dada yake Natu ameolewa na Ken. Ken na John walaitana:

A. mwamu

B. mwanyumba

C. kivyere

D. mkwe.

22. Ni kundi lipi lenye viunganishi pekee?

A. maadamu, kama, kefule, hamadi

B. ijapokuwa, ila. wala, bali

C. labda. ingawa, ikiwa. hala

D. sembuse, tarigu, badala, basi.

23. Shehena ni ya mizigo ilhali ni la udongo.

A. tita

B. peto

C. shumbi

D. bumba.

24. Chagua scntensi ycnye maelczo sahihi.

A. Hijabu ni ugonjwa Wa kuvimba fizi.

B. Kinieta ni ugonjwa unaodhoofisha figo.

C. Tauni ni ugonjwa unaokatakata viungo.

D. Surua ni ugonjwa wa kutoa vipele.

25. Ni scntensi ipi yenye maturnizi sahihi ya koloni? A. Iumapili ni tarehe: 3.3.2012.

B. Mama alinunua matunda: yaani, chungwa, fenesi na embe.

C. Teknolojia imefanikisha maendeleo: akasema waziri.

D. Miji niliyotembelea ni hii: Kisurnu, Nairobi, Voi na Einbu.

26. Gugu ni nyasi ndefu zinazomea katika sehemu Lambarare, gugu pia ni D

A. mmea unaotambaa kote shambani;

B. mmca unaobana minginc shambani;

C. mmea unaomea pale pasipopaliliwa;

D. mmea unaomea mahali usipotakikana.

27. Chaguajibu lenye maelezo sahihi.

A. Mjumu ni fimdi wa kufua visu.

B. Sogora ni bingwa wa kuimba mashairi ngomani.

C. Dalali hushindania bidhaa mnadani.

D. Mkalimani hutafsiri maandishi vitabuni.

28. Sentensi, ‘Jedi ni ninga’ imetumia tamathali gani?

A. Msemo

B. Tashbihi

C. Sitiari

D. Nahau.

29. Arbuni ni

A. sehemu ya bei ya kitu inayotolewa mwanzoni;

B. sehemu ya ujira Wa kumsaidia mtu mwanzoni;

C. sehemu ya fidia anayolipwa mtu mwanzoni;

D. sehemu ya malipo ya kukopea kitu

30. Methali, ‘Kamba ya mbali haifungi kuni’, ni kwa wanaotegemea msaada wa walio mbali.

‘Maji ya kifuu bahari ya chungu’. ni kwa

A. anayciona hadhi ya vitu kuwa ya chini;

B. anayeyaona matatizo ya wengine kuwa madogo;

C. anayeziona hali za wengine kuwa Za kawaida;

D. anayeviona vilu vidogo kuwa na Faida

Soma kifimgu kifizatacho kisha ujibu maswuli 31 mpaka 40,

Afya au siha ni hali ya kutokuwa na maradhi. Hali hii humwezesha mtu kuhifadhi nguvu zake Za mwili na kufanikisha utendakazi katika nyanja tofautitofauti. Mtu mwenye afya bora huweza kutekeleza mengi bila udhia. Mathalani, yeye huweza kujirausha na kujishughulisha hadi jioni bila kuhisi uchovu mwingi.

Mti hauendi ila kwa nyenzo, nayo afya nzuri haimjii tu mtu. Afya hustahili kupaliliwa na kutunzwa kwa namna anuwai kama vile kula vyakula vyenye viinilishe, kufanya mazoezi na kuandama niienendo miadilifu. Usafi wa mwili na mazingira pia huchangia katika kuimarisha afya. Ni wazi kwamba mazingira yakiwa machafu hukosa kuvulia na kusababisha kuhanikiza kwa harufu inayokirihisha. Isitoshe, uchafu huwa hali mufti ya kuzaana kwa wadudu kama vile chawa, kunguni, nzi na mbu ambao ni maadui Wakuu Wa afya.

Tabia ya mja huathiri afya yake. Wapo Watu ambao Wameambulia magonjwa kama vile saratani ya ini na rnapafu, na kifua kikuu kutokana na uraibu wa pombe, sigara na dawa za kulevya. Wengine hujiponza kwa kuingilia vitendo viovu kama vile kushiriki mapenzi kiholela na kujisababishia magonjwa. Magonjwa haya ni kama vile kaswende na ukimwi ambao umewapukutisha wengi. Hali kadhalika, Watu hujiharibia afya kwa kufanya kazi mfillulizo bila kupumzika. Licha ya kwamba bidii ni muhimu katika maendeleo yajamii yoyole ile, utendaji kazi kidindia huweza kuwa na athari hasi. Kuna baadhi ya watu ambao Wamewahi kupata maradhi ya moyo, ya kiakili na hata shinikizo la damu kutokana na hali kama hii. Wengine hujihasiri kwa kula vyakula vingi kupindukia.

Kadhalika, Wapo Wcngine ambao hupata magonjwa kwa kula vyakula visivyofaa. Katika kundi hili kuna wale ambao hawadiriki kufanya kazi wala mazoezi. Hawa hujinenepea na kudhoofisha utendakazi wao. Pia kuna wengine ambao hawali chakula cha kutosha. Hawa nao huweza kupata magonjwa kama vile safura na vidonda vya tumbo.

Hall ya umaskini pia huchochea kuzoroteka kwa afya. Asilimia kubwa ya watu nchini humu haimudu huduma bora za afya na lishe bora kutokana na hali ya ufukara. Wengine, kwa kukosa fedha, hawapati elimu ya kimsingi kuhusu afya. Hawa huweza kujizulia magonjwa kwa kutojua na kutofuata kanuni Za afya. Pamoja na haya, kuna Wale ambao Wanarithi magonjwa ya kiukoo kama vile bolisukari kutoka kwa wazee Wao.

Umuhimu Wa afya hauwezi kupuuzwa. Taifa lenye kizazi chenye afya hustawi kiuchumi. Afya ikidumishwa wanajamii huweza kutumia fedha Z210 kuwekeza katika miradi badala ya kuzitumia kujiuguza au kuwauguza Wenzao. Ni jukumu la kila raia kuhakikisha kwamba ameilinda afya yake na ya Wengine kwa vyovyote vile. Walio na mazoea ya kupuuza ushauri wa wanaotoa huduma za afya na lishe wajiase, la sivyo watakuja kujiuma vidole.

31. Kulingana na aya ya kwanza, afya:

A. huimarisha matokeo ya utendakazi;

B. humwondolea mtu matatizo mwilini;

C. humpunguzia rntu mazoea ya uchovu;

D. hukuza maendeleo katika maeneo Mbalimbali.

32. Ni muhimu kutunza mazingira kwani:

A. tutarudisha hali ya kupendeza;

B. tutaepuka kuenea kwa harufu;

C. tutamaliza vikwazo tofautitofauti vya afya;

D. tutazuia ongezeko la wadudu waharibifu.

33. Mwandishi anapinga hali gani hasa katika aya ya tatu?

A. vifo vya watu wengi;

B. kuhusiana bila mpango;

C. matumizi mabaya ya vileo;

D. uambukizaji wa magonjwa.

34. Chaguajibu ambalo si sahihi kulingana na aya ya nne,

A. Jambojema huweza kusababisha madhara.

B. Kazi nyingi husababisha ugonjwa Wa mayo.

C. Mazoezi hudhibiti ukubwa wa mwili.

D. Mapumziko huimarisha hali ya mtu kiakili.

35. Chakula huwadhuru:

A. Wanaokula mara zote na kunenepajinsi isivyostahili;

B. wasiofanyajuhudi kuongeza hamu ya kazi;

C. Wasiopanga njia nyingi za kutumia lishe;

D.wanaokula kiasi kisicholingana na mahitaji yao kimwili.

36. Chagua jibu sahihi kulingana na kifungu.

a.Watu Wengi nchini hupata magonjwa kutoka kwajamaa zao.

B.Walu wengi nchini hudhoofika kiafya kwa kukosa pesa.

C.Watu wengi nchini hawajui hali ya afya zao.

D.Watu wengi nchini hupuuza onyo kuhusu afya.

37 Umuhimu wa afya hauwezi kupuuzwa kwa vile:

A. Magonjwa husababisha kuzorota kwa maendeleo.

B.Watu Wagonjwa hawawezi kuizalisha mali.

C.Pesa nyingi hutumiwa kuwatunza Walio hospitalini.

D.Mipango nchini hukwama wahudumu wakikosekana.

38. Chagua funzo linalojitokeza katika aya ya mwisho.

A. Taifa haliwezi kuimarisha afya bila raia wote kuhusika‘

B. Wanaodharau watu wenye busara hupata maradhi.

C. Mtu hawezi kufaidika kiafya bila kupata ushauri.

D. Wanaokosa kujikanya hupata majuto baadaye.

39 Maana ya, ‘mti hauendi ila kwa nyenzo’ imejitokeza vipi katika kifungu?

A.Wanaokula vyakula vyenye viinilishe huzuia kunenepa.

B.Wanaoepuka kazi hawapati shinikizo la damu.

C.Wanaozingatia miencndo mizuri hudumisha afya,

D.Wanaonyoosha viungo vyao huwa wakakamavu.

40. Maana ya ‘inay0kirihisha‘ ni:

A. inayodhuru;

B. inayoenea;

C. inayoaibisha;

D. inayochukiza.

 

Soma kifungu kzfualachu kisha ujibu maswali 41 mpaka 50,

Shawe alizaliwa katika familia iliyojiweza. Malezi yake basi yangeweza kutabiriwa. Alilelewa kwa tunu na tamasha, asij ue maana ya msamiati wa kukosa. Wazazi wake walikuwa Wafanyabiashara maarufu ambao walisafiri nchini na ng’amb0 kwa shughuli hizo. Hata hivyo, hawakukosa muda wa kutangamana na mwanao. Walimwelekeza na kumfunza maadili na kanuni za kijamii, si kwa maneno tu, bali pia kwa vitendo.

Miongoni mwa mambo ambayo wazazi wa Shawe walitilia maanani ni umoja na mshikamano Wa kijamii. Pamoja na kwamba Walikuwa kiguu na njia katika kujiinua kiuchumi, hakuna sherehe ya kijijini, iwe harusi au matanga waliyokosa kuhudhuria. Wakali ambao mmoja wao alikuwa safarini, mwenzake alimwakilisha. Wanakijiji waliwapenda na kuwastahi, nao wakawa hawaishi kumsifia Shawe ukarimu na uchangamfu wa wanakijiji. Walimshauri kuhusu umuhimu wa kushirikiana na Wengine na kumtahadharisha kuwa mm pweke ni uvundo.

Shawe aliendelea kukua, akarithi labia ya wazazi wake ya kuinamia cha mvunguni; akawa mwanafunzi hora masomoni, tena mtiifu kwa walimu na hata majirani. Bidii yake ilizaa matunda, akapanda ngazi moja hadi nyingine kielimu, akafikia kilele cha elimu yake chuoni alipohitimu shahada ya tatu. Baadaye alipata kazi nzuri na kupanda madaraka kutokana na bidii yakc. Baada ya kudunduliza pesa za kulosha za kuikimu familia, Shawe aliamua kuoa. Hapa ndipo maisha yake yalipochukua mkondo mwingine.

Shawe alijikuta amekabiliwa na mabadiliko ya kihali ambayo hakuyawazia. Awali alikuwa akiwategemca Wazazi kwa ushauri na maelekezo, sasa ndiye aliyetarajiwa kuwa mshauri na mwelekezi wa familia yake. Majukumu mengine ya kijamii pia yalimtumbulia macho. Pamoja na shughuli nyingi za kikazi, desturi zajamii yake zilimhitaji kushirikiana na wanajamii wenzake kwa hali na mali. Ingawa Shawe alikuwa mkono Wazi, alihisi kuwa hakuwa na muda Wa kutosha kutangamana na wanajamii Wcnzakc katika shughuli kama vile kudumisha usalama, sherchc za posa na hafla za kuchangia elimu ya watolo maskini.

Mkewe Shawe alijaribu kumrai atenge muda, hasa mwishoni mwa wiki, kuingiliana na Wanajamii Wengine lakini kila mara Shawe alilalamikia hili na lilé akisema kwamba ametingwa na kazi. Palipotokca haja ya kifedha, Shawe hakuchelewa kutoa mchango Wake. Hakika hata alitoa pesa kila mwezi kukuza hazina ya Chama Cha Masilahi Ya Mtaa alikoishi. Mkewe alikerwa mno na hali hii na kumkumbusha kila mara kuwa pesa hununua; hazitumwi. Wanakijiji nao, pamoja na kwamba Walitambua na kuienzi michango yake ya kifedha, Walihisi kwamba Shawe anajitenga nao. Kulingana nao, Shawe aliwanyima fursa ya kufaidika kwa kipawa chake cha uongozi. Walimtumia mjumbe, si mara moja, si mara mbili kuhusu hali hii. Shawn: ambaye alikuwa amedidimia zaidi katika kazi yake alikiona kitendo cha wanakijiji kama usumbufu. “Mimi hutuma michango yangu kila mara wanapoihitaji, wanataka nini zaidi?” alisema Shawe.

Siku moja Shawe alikuja kutambua maana ya methali, ‘Kinyozi hajinyoi’. Kifungua mimba wake aliamua kuuasi ukapera, akamtaka babake kupeleka posa kwa mchumba wake. Kama ilivyokuwa desturi, Shawe alihitaji kuandamana na wazee na akina mama katika shughuli hii. Alimtuma mkewe kumjuza kinara Wa baraza la ukoo pamoja na mwenyekiti Wa Chama Cha Masilahi Ya Mtaani.

Viongozi hawa walipopata ujumbe huo, Walitabasamu tu, wakawakusanya wanachama Wao kuwapasha habari, wanachama wakafurahi kwamba mtoto anapata jiko. Walikusanya pesa na kumtumia Shawe kupitia kwa mkewe huku kila mmoja wao akituma udhuru wa kutohudhuria. Shawe alipokea bahasha iliyosetiri kibunda cha pesa kutoka kwa mkewe, akazitazama kwa masikitiko makuu huku amejiinamia kwa fedheha. Lilikuwa pigo lililohitaji moyo wajiwe kulikabili.

41. Wazazi wa Shawe walikuwa walezi Wema kwa vile:

A. walikuwa kielelezo chema kwa Shawe;

B. waliweza kuzingatia dcsturi za kijamii;

walifanya bidii katika biashara yao;

Walisema na Shawe bila shida.

5 Q 42. Kifungu kinaonyesha kwamba:

A. Shawe alibainisha umuhimu na uwezo wa wanakijiji.

B. Wazazi Wa Shawe waliungana na wanakijiji katika hali zote.

C. Wazazi wa Shawe walifurahia kutangamana kwa wanakijiji.

D. Shawe alijifunza maana ya ushirikiano kwa namna zotE.

43. Shawe alifanana vipi na Wazazi wake?

A. Aliwaheshimu walimu na majirani.

B. Alipiga hatua moja hadi nyingine maishani.

C. Aliweka akiba hadi akaoa kwao kijijini.

D. Alijitahidi masomoni na kazini.

44. Kulingana na aya ya nne, jamii:

 

A. lnamhitaji kila mmoja kukumbuka maendeleo ya kijamii.

B. Inamhitaji kila mmoja kushiriki kuendeleza elimu ya kijamii.

C. lnamhitaji kila mmoja kuhusika katika kanuni za kijamii.

D. lnamhitaji kila mmoja kuzipenda shughuli za kijamii.

45. Chagua maoni ya wanakijiji kumhusu Shawe.

A. anayeweza kuboresha uendeshaji wa kijiji;

B. aliyejaliwa mali pamoja na utu;

C. aliyependa kutoa usaidizi wake haraka;

D. anayejua kuangazia masuala yajamii.

 

46 “Mimi hutuma michango yangu kila mara wanapoihitaji, wanataka nini zaidi?”, inannyesha kuwa:

A. Wanakijiji walimtarajia Shawe kuwafikiria ipasavyo.

B. Wanakijiji waliutarajia ushirika kamili wa Shawe.

 

C. Wanakijiji walimtarajia Shawe kuwaandama vilivyo.

D. Wanakijiji waliutarajia uelekezi ufaao wa Shawe.

47. Wanakijiji wanajaliana masilahi hasa kwa

A. Walimwonya Shawe kuhusu upuuzaji wa ushirikiano.

B. Walimpa mkewe Shawe pesa ashughulikie ndoa.

C. Walizingatia ubora wa hazina ya chama.

D. Walichangamkia vyema ndoa ya mwanawe Shawe.

48 Wazo kuu linalojitokeza katika aya ya mwisho ni kwamba;

A. Wanakijiji walikuwa wamenuia kumpuuza Shawe. B. Wanakijiji walikuwa wameudhika na ujumbe wa Shawc. C. Wanakijiji walikuwa wamechoshwa na kupotoshwa kWa Shawe.

D. Wanakijiji walikuwa wameamua kumrekebisha Shawe.

49 Kwa nini hasa Shawc alijitcnga na wa.na.kijiji?

A. kukerwa;

B. kutosheka;

C. kiburi;

D. kisomo.

50 Chagua maana ya kifungu kifuatachoz ‘Alilelewa kwa tunu na tamasha, asijue maana ya msamiati wa kukosa.’

A. alipcndwa na kushauriwa kuhusu hali yakE.

B. alipendwa na kutimiziwa mahitaji yake yote;

C. alipendwa na kurithishwa yote aliyoyataka;

D. alipendwa na kuonyeshwa yaliyomfaa kwao;

 

 

Free KNEC KCPE Past Papers Kiswahili 2014 Marking Scheme/Answers

1.C 2.A 3.C 4.B 5.B 6.D 7.A 8.B 9.B 10.C 11.D 12.A 13.C 14.B 15.C 16.C 17. A 18.B 19.C 20.A 21.B 22.B 23.C 24.A 25.D 26.D 27.A 28.C 29.A 30.B 31.A 32.D 33.C 34.B 35.D 36.B 37.A 38.A 39.C 40.D 41.A 42.B 43.D 44.C 45.A 46.B 47.A 48.D 49.C 50.A

Leave a Comment