KNEC KCSE Kiswahili Paper 3 Question Paper / 2015 KCSE Tharaka South Joint Examination
2015 KCSE Tharaka South Joint Examination
Kiswahili Paper 3
1.LAZIMA : (Alama 20)
USHAIRI
Kiatu umepasuka, mwenyeo ni masikini
Nakuona wararuka, ukanyagapo njiani
Hivyo ngozi kichunjuka, ‘takusaidia nani?
Uvawavyo miguuni,utazidi kutoboka.
Awali ulisifika, ulipotoka dukani
Mwenyeo aliudhika, upitapo matopeni
Rangi aliyokupaka, kwa leo ungepakwani?
Uvawavyo miguuni, utazidi kutoboka.
Urembo umekutoka, si kama vile zamani
Weupe ulimemeka, mwenyeo ‘kikuthamini
Sasa amefilisika, japo enenda kazini
Uvawavyo miguuni, utazidi kutoboka.
Yakaa umekenuka, wangaliapo usoni
Kama kwamba unacheka, una kicheko kinywani
Tena ulivyopanuka, bila shaka u ta’bani
Uvawavyo miguuni, utazidi kutoboka.
Vidole vinaoneka, vimekunyata humoni
Wayo unadhihirika, kwani soli mashakani
Wafanya nyingi dhihaka, upitapo sakafuni
Uvawavyo miguuni, utazidi kutoboka.
Kwa kweli utatoboka, jinsi hali ya Fulani
Kila unaponyanyuka, ana wewe miguuni
Miezi tele yapita, pasi kulipwa kipeni
Uvawavyo miguuni, utazidi kutoboka.
Mwenyeo yalimfika, kwanzia mwezi wa juni
‘Ngawa kazini afika, tajiriye amhini
Hivo huwezi tunzika, kiatu cha mokasini
Uvawavyo miguuni, utazidi kutoboka.
Ijapo amekuchoka, hangekutupa pipani
Kwani unahitaji, kutembea ofisini
Tena inadhihirika, si mzaha si utani
Uvawavyo miguuni, utazidi kutoboka.
Takubidi kutumika, kutuliza wayoni
Kwani huwezi tunzika, wala kulipia deni
Tena umeshadunika, kupelekwa kwa rahani
Uvawavyo miguuni, kupelekwa kutoboka.
MASWALI
a) Ni anwani gani inayofaa shairi hili? (alama 1)
b) Taja na ueleze tamathali ya usemi iliyotumika katika ubeti wan ne wa shairi hili. (alama 2)
c) Kwa kutoa mifano mitatu, onyesha jinsi inkisari ilivyotumika katika shairi hili. (alama 3)
d) Taja bahari mbili zinazodhihirisha katika shairi hili. (alama 1)
e) Ni mambo gani yanayodhihirisha kwamba kiatu kimetokwa na uembo? (alama 3)
f) Ni sababu gani zinazomfanya mwenye kiatu kuendelea kukitumia? (alama 2)
g) Huku ukitoa mifano mwafaka, taja mambo yanayoonyesha kwamba hili ni shairi la arudhi. (alama 6)
h) Taja maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi. (alama 2)
i) Kenuka
ii) Rahani
20 marks
2.RIWAYA: (Alama 20)
Fafanua matumizi ya majazi kama fani ukirejea riwaya la Kidagaa kimemwozea.
20 marks
“….Mwenda juu kipungu hafikii mbinguni!…”
a) Eleza muktatha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Eleza ukweli wa dondoo ulilolisoma kwa mujibu wa riwaya Kidagaa kimemwozea. .(alama 16)
20 marks
3.TAMTHILIA: (Alama 20)
Msthaki Meya: Timothy M. Arege
…..Dawa tulizonazo ni pain killers tu!…..wawashie taa ya tumaini. Ganga ganga za mganga huleta tumaini.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Onyesha mbinu tatu zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 6)
c) Kando na ukosefu wa dawa na matibabu mazuri, eleza matatizo mengine matano wanayokumbana nayo wanacheneo. (alama 10)
20 marks
Jadili jinsi maudhui yafutayo yanavyojitokeza katika tamthilia ya Mstahiki Meya.
i) Unafiki
ii) Umaskini
20 marks
4.HADITHI FUPI (Alama 20)
Jibu swali la 6 au 7
Damu Nyeusi na Hadithi nyingine Ken Walibora na Said A. Mohamed
a) Onyesha jinsi maudhui ya utamaduni yanavyojitokeza kwa mujibu wa hadithi ya Mke wangu. (alama 10)
b) Eleza sifa za Mhusika Aziza katika hadithi hii. (alama 10)
20 marks
Ndoa ya samani
a) “Fahami twe’zetu nyumbani”
i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
ii) Fafanua sifa zozote nne za msemaji wa dondoo hili. (alama4)
b) Fafanua dhana ya fadhaa iliyobainishwa katika hadithi hii. (alama 2)
c) Dhihirisha maana ya ‘Kanda la usufi’ kwa kurejelea hadithi kanda la usufi ya Rhoda Nyaga. (alama 10)
20 marks
5.FASIHI SIMULIZI (Alama 20)
a) Eleza maana ya Fasihi Simulizi. (alama 2)
b) Eleza matatizo matano yanayokabili fasihi simulizi katika jamii ya sasa. (alama 10)
c) Tofautisha vipera vifuatavyo vya fasihi simulizi (alama 4)
i) Maghani na mighani
ii) Ngoma na ngomezi
d) Taja sifa nne za mwigizaji bora. (alama 4)
20 marks