KNEC KCSE Kiswahili Paper 3 Question Paper / 2015 KCSE Kajiado County Joint Examination
2015 KCSE Kajiado County Joint Examination
Kiswahili Paper 3
1.USHAIRI (Alama 20)
LAZIMA:
Ah! siambile ovyo, samba ah! kupuuzwa
Ah! hii niambavyo, si kwaamba nimependezwa
Ah! moyo wamba hivyo, kwayo niliyofanyizwa
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.
Ah! si mimi nilivyo, mawazo yametatizwa
Ah! tata za magovyo, fikira zimeshangazwa
Ah! naviwe viwavyo, sioni pa kutulizwa
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.
Ah! sililii yavyo, kwa kutaka kunyamazwa
Ah! sipendezwi navyo, sipendezwi kebezwa
Ah! ni hivi ambavyo, mkata heshi kutezwa?
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.
Ah! kukicha ya vivyo, na uchao yajalizwa
Ah! havishi viishavyo, na matayo kuambizwa
Ah! sivyo hivi sivyo, vyakanywa na kukatazwa
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.
Ah! lau hata ndivyo, basi hata kulekezwa
Ah! wayatenda kwayo, kwamba ndiko kutukuzwa
Ah! tenda utendavyo, ni kuwa watendekezwa
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.
Ah! ni vile wambwayo, togo upate tangazwa
Ah! kila upendwavyo, mwisho ‘we utatukizwa
Ah! pendo lianzwavyo, sivyo vya kuishilizwa
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.
Ah! kila lenye govyo, halikawii kuvizwa
Ah! nalende lendavyo, ukomo litagotezwa
Ah! ni vipi kulivyo, kukadumu kutulizwa?
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.
Ah! dunia ni kyovyo, kizamacho chaibuzwa
Ah! ni mangapi ja’vyo, hayako metokomezwa
Ah! jaa lijaavyo, mwishilio lapunguzwa
Ah! namba nionavyo, vipasavyo kuelezwa.
Ah! kaa ukaavyo, hatimayo yasogezwa
Ah! nauwe uwavyo, atende hulipizwa
Ah! hakuna lilivyo, gumu lisilolegezwa
Ah! namba nionavyo, vipasyo kuelezwa.
a) Taja mambo matatu ambayo mshairi analalamikia. (alama 3)
b) Shairi hili liko katika bahari gani? Toa sababu. (alama 2)
c) Taja na utolee mifano tamathali mbili za lugha zilizotumiwa na mshairi. (alama 4)
d) Huku ukitoa mifano kutoka shairi, eleza matumizi yoyote matatu ya uhuru wa ushairi. (alama 3)
e) Andika ubeti wa kwanza katika lugha ya nadharia. (alama 4)
f) Tambua toni ya mshairi. (alama 2)
g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa kwenye shairi. (alama 2)
i. Watendekezwa
ii. Togo
20 marks
2.RIWAYA (Alama 20)
Kidagaa Kimemwozea; Ken Walibora Jibu swali 2 au la 3
Thibitisha matumizi ya mbinu zifuatazo katika Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
i. Sitiari (alama 10)
ii. Taswira (alama 10)
20 marks
…..ilibidi kulipa hela nyingi za kadhongo, kuwalipa polisi, makarani wa mahakama, majaji, wajua tena mti hauendi ila kwa nyenzo.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Eleza tamathali ya usemi iliyo katika dondoo. (alama 2)
c) Fafanua maudhui yanayorejelewa katika dondoo hili kwa kutumia mifano saba (alama 14)
20 marks
3.TAMTHILIA: (Alama 20)
a) “…….Duniani kuna watu na viatu….” Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea Tamthilia ya Mstahiki Meya. (alama 16)
20 marks
4.HADITHI FUPI: (Alama 20)
Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine: K. Walibora na S.A Mohamed. Jibu swali la 5 au la 6
“……Usipoachana na mambo haya nitaacha kazi,”
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
b) Thibitisha kuwa mnenewa ni katili. (alama 16)
20 marks
Kwa kurejelea hadithi zifuatazo onyesha jinsi vijana walivyosawiriwa.
i. Gilasi ya mwisho makaburini. (alama 5)
ii. Kanda la usufi
iii. Shaka ya mambo
iv. Tazamana na mauti
20 marks
5.FASIHI SIMULIZI (Alama 20)
a) Mbali na kuapiza na kufukuza pepo taja miktadha mine mingine ambapo ulumbi hutumika. (alama 4)
b) Eleza sifa zozote tatu za ulumbi. (alama 6)
c) i) Maapizo ni nini? (alama 2)
ii) fafanua umuhimu wa maapizo katika jamii. (alama 8)
20 marks
Ndimi kisoi, dume la ukoo mtukufu
Ulojipambanua kwa mabingwa
Wachezaji hodari wa ngoma
Ndimi dume liloingia nyanjani.
a) Tambua aina ya maghani inayowasilishwa. (alama 2)
b) Fafanua sifa bainifu za aina hii ya utunzi. (alama 10)
c) Eleza umuhimu wa tungo hizi katika jamii. (alama 8)
20 marks