KNEC Kiswahili Paper 2 Question Paper / 2016 KCSE MOKASA Joint Examination
2016 KCSE MOKASA Joint Examination
Kiswahili Paper 2
1.UFAHAMU (Alama 15)
Idara ya polisi nchini imelaumiwa kwa muda mrefu kutokana na visa vya mauaji ya kiholela, utepetevu na ufisadi miongoni mwao.Ni kutokana na kilio cha mwananchi pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali ambapo serikali imejitolea sabili kubadili hali katika idara hiyo huku tume mbali mbali zilizobuniwa zikitoa mapendekezo muhimu ya kurekebisha idara hiyo. Matokeo ya hivi punde kutoka kwa shirika la Transparency International liliorodhesha idara ya polisi kama idara fisadi zaidi nchini,maoni ambayo yalisisitiziwa na shirika la kutetea haki za kibinadamu .Ufisadi bado umekita mizizi katika idara ya polisi tangu mabadiliko yaanze upande wa trafiki na hata ndani ya polisi,.
Serikali imejitolea kupambana na ufisadi unaonekana kuwa kidonda ndugu katika idara ya polisi. Wananchi wanasema kuwa polisi ni mafisadi na kusahau kuwa ufisadi unashirikisha watu wawili na wote wanapaswa kufunguliwa mashtaka,lazima raia na polisi wazingatie hili.Na ili kuleta mabadiliko muhimu katika idara ya polisi,mapendekezo yote pamoja na ya tume zingine za hapo awali lazima yatekelezwa na kwa mujibu wa katiba mpya.Lazima mabadiliko yaanze uanzia juu kwani maafisa wadogo hulazimiswa kuchukua hongo ili wapelekee wakubwa wao,ni lazima shughuli ya kuwachagua maafisa waliobora ifanyike kisheria ili mabadiliko yaanze kutoka kwa wakuu wa maafisa wa polisi.
Polisi kidogo wameweza kubadili ile lugha yao ya matusi na ukali kwa rai.Raia nao hawajabadilika,bado wana uwoga dhidi ya polisi na itachukua muda kwani wanadhania kuwa kikosi ni kile kile cha kitambo.Kwa upande wa polisi, hakuna mageuzi yamefanyika. Unaposafiri
kuja mjini polisi wangali wana chukua hongo kutoka kwa wenye matatu na kuwaruhusu kubeba kupita kiasi, pia usalama umedorora sana kwani kumekuwa na visa vingi vya mauaji hapa mjini.ukiangalia maafisa wa polisi hakuna mageuzi makubwa yameshuhudiwa haswa kwa upande wa maafisa wa trafiki bado ni wale wale na ufisadi ungali upo.
Mabadiliko ambayo tunataka ni ile polisi wasikae mahali kwa muda hadi wanajuana na mafisadi na majambazi.Maafisa wa polisi wanafaa kuhudumu katika kituo kimoja kwa muda usiozidi miaka mitatu.Kwa kufuata njia hiyo mabadiliko yatapatikana.Juhudi nyingi zikielekezwa katika kubadili kikosi cha polisi wananchi wanapaswa kuhamasishwa ili nao wawezakubadilikahaswa kuhusuiana na mtazamo wao kwa maafisa wa polisi .Na huku tukijaribu kubadili maafisa wa polisi wananchi pia wanapaswa kuelimishwa ili waweze kubadili mtazamo wao kuhusu maafisa hao.Ni bayana kuwa ili kuweza kuleta mabadiliko ya kutamanika katika kikosi cha polisi na haswa katika kupambana na ufisadi uliokita mizizi wananchi sawia na maafisa wa polisi wanajukumu la pamoja kuleta mabadiliko hayo yatakayopelekea kuwepo kwa mlahaka mzuri kati ya maafisa wa polisi na raia.Hatimaye kuwepo kwa huduma bora itakayochangia pakubwa kuboresha uchumi wa taifa na kuafikiwa kwa ruwaza ya mwaka 2030.
Maswali
a) Kipe kifungu hiki kichwa mwafaka. (alama 1)
…………………………………………………………………………………………………………………………………
b) Thibitisha kwamba ufisadi ni kidonda ndugu ukirejelea makala haya.. (alama2)
………………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
c) Ni vipi ufisadi katika idara ya polisi unaweza kuzikwa katika kaburi la sahau? (alama2)
………………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………….
(d) ‘Wananchi ndio wanapaswa kulaumiwa kwa ufisadi.”Thibitisha. (alama 3)
………………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………..……………………………………………
(e) “ Serikali imepiga hatua katika kuleta mabadiliko katika idara ya polisi”.Onyesha kinaya
cha usemi huu.(alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………..
(f) Taja manufaa yoyote mawili yanayotokana na mabadiliko katika idara ya polisi (alama2)
………………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………………….
(g) Eleza maana ya:
(i)Mlahaka……………………………………………………………………………………….
(ii)Utepetevu………………………………………………………………………………………
(iii) Kujitolea sabili………………………………………………………………………(alama 3)
20 marks
2.UFUPISHO (Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata
Kwa miaka na dahari, nchi nyingi za Asia, Amerika Kusini na Afrika, zimekuwa na mamilioni
ya watoto wanaoteseka. Matatizo huwakumba kwenye hali nyingi. Si kielemu, si kiafya, si
kiutamaduni na kimakuzi tu, bali hata kiuchumi. Nguvu zao na uwezo wao hufujwa kwa njia
zinazokirihisha nyoyo. Wale wanaopenda maendeleo na kutilia nguvu haki za kibinadamu
huudhiwa kupindukia.
Wazazi wengi wa sehemu hizo wamekuwa wakiamini mambo kipuuzi. Wamekuwa wakidhani
kuwa wingi ni hoja, lakini wazazi hawa huwapata watoto wengi wasioweza kuwatunza. Isitoshe,
huwachukulia watoto kama sehemu ya mali yao badala ya kuwachukulia kuwa ni binadamu
wenzao. Akili haziwapigi na kutambua kuwa, hata nao ‘vinyang’arika’, wakitunzwa vizuri na
kupewa nafasi mwafaka za kuwainua kimaendeleo, wataweza kuwa watu wa kutajika katika
jamii. Wazazi kama hao wanadhania ya leo ni leo tu, msema kesho ni mwongo. Dhana hizo
finyu na potovu zimewapelekea kuthamini uzaaji wa watoto wengi ili watoto hawa wawe punda
wa dobi. Wazazi hawa wanajihisi matajiri wa kupindukia wanaopata vijana wengi wa
kuwasaidia katika kazi zao bure bilashi.
Baadhi ya watoto hunyimwa nafasi ya kwenda shule. Wale wanaonjeshwa masomo kidogo,
huachishwa kisomo hicho mapema. Sababu za kuhinishwa huko kwa kisomo zinafahamika
vizuri na wahusika hao. Mara nyingi, huachishwa shule ili wawe mayaya wa watoto wenzao au
wakafunge mifugo, kulima shambani, kusaidia biasharani na katika sekta za juakali. Watoto
hawana nguvu za kukataa kwani ni kinyume cha utamaduni kuwapinga wazazi. Isitoshe, watoto
hawa wanawategemea wazazi hao kwa kila kitu. Utiifu huu, ingawa una uzuri wake
unazorotesha maendeleo kupindukia.
Unyonge wa aina hii umefanya mashirika ya viwanda, ya mashamba kama ya chai, kahawa, ya
pamba na ya juakali kuwatumia watoto vibaya bila ya kujali maslahi ya watoto hao. Baadhi ya
watu wameanzisha mashirika ya uasherati na utumwa. Watoto wanateswa na kuingizwa kwenye
majanga yanayotokana na ukimwi na mengine ya uzinifu. Kutokana na dhuluma hizi, watoto
hukandamizwa na kupewa posho duni ya kuwapa uhai tu. Matajiri wamezidi kufutuka kiuchumi
kutokana na jasho la watoto hao. Watoto hawapewi kinga zozote za kemikali wala kuonyeshwa
jinsi ya kuzitumia kemikali hizo. Wakuu wao hutumia saikolojia duni za watoto kuwawezesha
kujikuza kiuchumi. Huwapa viperemende hafifu na viungo ovyo ili watoto waimbe na kucheza
ngoma za watu hao. Watoto, kwa kutojua, huwasifu wakuu wao badala ya kuwalaani kwa
kuwanyonya hadi mifupani na kupewa vijipesa tu. Kwa kuwa ni watoto hawatambui kuwa
wanahiniwa.
Matajiri nao husahau kuwa watoto hao wakisoma vizuri hadi mwisho, wanaweza kutoa huduma
bora nchini. Inadhihirika kuwa lengo potovu la watu hao ni kukwepa kulipa mishahara mikubwa
kwa watu wazima. Lakini nasema si sawa kuwanyonya watoto. Matajiri hawa wangehisi vipi
kama watoto wao nao wangefanyiwa hivyo? Ama ni yule ya mkuki kwa nguruwe, kwa
mwanadamu uchungu? Serikali zina mikono mirefu. Inafaa ziwachukulia hatua kali wazazi na
maafisa wanaotumia watoto kama matambara mabovu. Watoto nao wanafaa kuzinduka na
kutaka kusoma kinyuki. Inafaa wajue kuwa vipesa vya ujakazi ni sumu.
Mashirika ya aina hiyo, inafaa yakipatikana na hatia, yapewe adhabu kali. Yalazimishwe
kuwasomesha na kuwakimu watoto hao vilivyo, bila kuwanyanyasa ndipo wasome, kadri ya
uwezo wao.
Maswali
(a) Bila kupoteza maana iliyokusudiwa fupisha aya mbili za mwanzo kwa maneno (45-50)
(al. 6, 1 utiririko)
Maandalizi
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
Jibu
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………………………………
(b) Kwa kuzingatia taarifa hii eleza namna maonevu dhidi ya watoto yameendelezwa.. tumia
maneno (50-55) al. 9, 1 utiririko)
Matayarisho
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
Jibu
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
15 marks
3.MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
Kutokana na kigezo cha jinsi hewa inavyozuliwa,taja aina mbili za konsonanti na utolee
mifano kila moja
…………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
2 marks
Bainisha muundo wa silabi katika neno
Gongwa
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
2 marks
Eleza maana ya mofimu funge na kutoa mfano mwafaka
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
1 marks
(i)Eleza maana ya kiarifu. (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(ii)Onyesha kiarifu katika sentensi ifuatayo (alama 1)
Mtoto aliyezungumza na nyanyake ameingia darasa lililochafuliwa na watundu.
………………………………………………………………………………………………………
2 marks
Bainisha shamirisho katika tungo lifuatalo.
Mwanafunzi alipewa dawati na mwalimu jana jioni
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
2 marks
Bainisha matumizi ya kiambishi ‘ku’ katika sentensi hii
Naomi atakupikia chai halafu aende kule uwanjani
………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
2 marks
Tambua aina ya kivumishi na kihusishi katika sentensi ifuatayo
Kijana mgeni amekaribishwa na mgeni
………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………..
2 marks
Tunga sentensi ukitumia kitenzi ‘-nywa’ katika kauli ya kutendeka.
………………………………………………………………………………………………………
1 marks
Tunga sentensi iliyo na kitenzi kishirikishi kilicho na kiambishi nafsi na wakati
………………………………………………………………………………………………
1 marks
i) Eleza dhana ya kishazi. (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
ii) Onyesha aina za vishazi kwa kutumia sentensi moja. (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
2 marks
Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia vishale
Alimwona mamba majini alipopiga mbizi.
4 marks
Yakinisha
Mgonjwa huyo hakupona wala kurejea nyumbani
………………………………………………………………………………………………………
2 marks
Sahihisha sentensi ifuatayo
Mgeni ambaye aliyekuja atarudi jana.
………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………….
2 marks
Akifisha sentensi ifuatayo
Juma Maria ulimwona Farida Maria la hakuwepo jana
………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
2 marks
Andika sentensi ifuatayo katika wingi.
Ua unaozunguka nyumba una ua lililopandwa.
……………………………………………………………………………………………
1 marks
Weka nomino hizi katika ngeli zake
(i)Mbalungi……………………………………….
(ii)Mturuki………………………………………
1 marks
Andika katika hali ya udogo
Alishikwa na jipu ambalo lilivimbisha kidole chake cha mguu mithili ya pera.
…………………………………………………………………………………………………
2 marks
Andika katika usemi wa taarifa
“Lo! Kumbe wazuri hawajazaliwa,” Omari alisema baada ya kumwona kisura huyo.
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
2 marks
Andika misemo inayoafiki hali zifuatazo
(i)Kubahatika………………………………………………………………………………………
(ii)Ubahaili………………………………………………………………………………………
2 marks
Eleza maana tatu za sentensi ifuatayo
Mama alimwimbia mwanawe.
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
3 marks
Tunga sentensi moja kutofautisha maana mbili ya neno ziwa
………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………..
2 marks
4.ISIMU JAMII (Alama 10)
(a) Eleza maana ya istilahi hizi;(alama 2)
(i) Usanifishaji…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………….
(ii) Lahaja………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………….
(b) Taja sifa zozote nne za lugha yoyote ile. (alama 4)
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………..
(c) Eleza mambo yanayochangia makosa ya kisarufi na ya kimatamshi katika lugha ya Kiswahili
(alama4)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
10 marks