KNEC KCSE Kiswahili Paper 3 Question Paper / 2015 KCSE Starehe Boys Centre Mock
2015 KCSE Starehe Boys Centre Mock
Kiswahili Paper 3
SEHEMU A: (Alama 20)
FASIHI SIMULIZI
(a) Eleza tofauti kati ya ngoma na ngomezi. {alama 4}
b) Eleza umuhimu wa ukusanyaji wa data za Fasihi Simulizi. {alama 6}
c) Andika fani zilizounda methali zifuatazo:- {alama 3}
i) Chelewa chelewa utapata mwana si wako.
ii) Ujana ni moshi ukienda haurudi.
iii) Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza.
d) Onyesha jinsi methali ni utanzu tegemezi kwa kueleza miktadha ambapo hutumiwa.
{alama 6}
e) Eleza maana ya semi. {alama 1}
f) Eleza maana ya lakabu. {alama 2}
g) Taja sifa 5 za lakabu. {alama 5}
20 marks
SEHEMU B (Alama 20)
RIWAYA: KIDAGAA KIMEMWOZEA Ken Walibora
“Wachache hawa hawaogopi, ashakum si matusi, hata kutema mate au kumwaga
mkojo usoni mwa haki, usawa na uhuru uliopiganiwa na kumwagiwa damu…”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Tambua mbinu ya lugha iliyotumika katika dondoo hili. (alama 2)
c) Huku ukitoa mifano fafanua aina 7 za ukiukaji wa haki katika riwaya
ya Kidagaa Kimemwozea.
20 marks
Jadili kauli kwamba Kidagaa Kimemwozea ni riwaya tatizo.
20 marks
SEHEMU C (Alama 20)
TAMTHILIA: MSTAHIKI MEYA Timothy M. Arege
”………Naona unajaribu kutia kidole chako katika mzinga wa nyuki. Ni hatari!”
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Eleza sifa nne za mnenewa. (alama 4)
c) Bainisha tamathali moja ya usemi inayojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)
d) Fafanua mifano mingine mitano ya tamathali hii katika tamthilia. (alama 10)
20 marks
Mwandishi wa tamthilia ya Msitahiki Meya ameshughulikia maudhui ya Usaliti na Ukoloni maomboleo vilivyo. Jadili…
20 marks
MKE WANGU
“Lo! Ati mimi nikachome mihogo niuze! Si nitaonekana nina wazimu mie?”
a) Eleza muktadha wa usemi huu. {alama 4}
b) Jadili sifa za msimulizi kama zinavyojitokeza katika hadithi hii. {alama 16}
20 marks
DAMU NYEUSI
“Nasikia wasichana wenu wote mnawakeketa na kuwashona ili kuzuia ukware?”
a) Eleza muktadha wa usemi huu. {alama 4}
b) Thibitisha jinsi ubaguzi ulivyoendelezwa katika hadithi hii, kwa kurejelea mifano MINANE.
{alama 16}
20 marks
SEHEMU D (Alama 20)
HADITHI FUPI: DAMU NYEUSI NA HADITHI NYINGINE
SEHEMU E (Alama 20)
USHAIRI: Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
Kimya changu kimezidi, navunja yangu subira,
Merejeya kwa miradi, kuhitimisha dhamira,
Kukejeli sina budi, niwafunze utu bora,
Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?
Sirikali bila hadi, ndo kiini cha madhara,
Yanopiga kama radi, isokuwa na ishara,
Yamini kuwa gaidi, wakitupora mishahara,
Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?
Wamejifanya hasidi, wasopatana kifikra,
Wana yao maksuudi, kujizombea ujira,
Wakilenga kufaidi, tumbo zao za kichura,
Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?
Nchi yetu kufisidi, ni jambo linonikera,
Tangia siku za jadi, ufukara ndo king’ora,
Kutujazeni ahadi, nyie mkitia fora,
Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?
Maskini watozwa kodi, wapwani na walo bara,
Kwa uvumba na uudi, mwawalipa kwa hasara,
Hamudhamini miradi, mejihisi masogora,
Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?
Mesema kazi ni chudi, basi sirikali gura,
Nafsi zenu mzirudi, mkubali kuchakura,
Makondeni mkirudi, muondoe ufukara,
Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?
Ujanjenu umezidi, demokrasia bakora,
Debeni takaporudi, michirizi kwenye sura,
Kuwachuja a! muradi, kwa za mkizi hasira,
Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?
Maswali
(a) Toa anwani mwafaka kwa shairi hili. (alama 1)
(b) Ainisha shairi hili kwa jinsi tatu na kutoa sababu. (alama 3)
(c) Onyesha mbinu za lugha katika shairi hili. (alama 2)
(d) Bainisha matumizi matatu ya uhuru wa mshairi katika shairi hili. (alama 3)
(e) Andika ubeti wa nne katika mtindo tutumbi. (alama 4)
(f) Fafanua maudhui matatu yanayojitokeza katika shairi hili. (alama 3)
(g) Taja mpango mmoja unaotajwa kama njia ya kutatua matatizo ya nchi. (alama 1)
(h) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 3)
20 marks
Ajaye kisimani mbele,hunywa maji maenge
Asinywe yalo na vunju
Yakampa kigegezi
Yakamtibua roho akaona na kinyaa
Awali ndio awali awali mbovu hamna
Ikiwa utalimatia,
Utayaramba makombo
Uvidata viyu cheche
Kisoma aali kikupe kisogo
Inajuzu ujihimu
Mwanafuu darasani
Uraukapo bukrata
Katu hutayaramba makombo
Hutokosa kisebeho
Dereva nawe utingo
Natija ni asubuhi
Wateja utawawahi
Wasaa kuzingatia
Uwafikishe kazini
Kwa wasaa ufaao
Wasije wakateteshwa na
Bosi wao nao wakuapize
Nawe mwana zaraa
Mpini uukamate kabla
Jua kutiririsha majasho jasadini
Ushindwe kung’oa magugu
Kutoka kwa lako konde
Mhadimu mwenye zohali
Yajuzu ujihimu
Maziwa anunue majogoo
Usije ukayadata na hivyo
Ukaandaa chai mkandaa
Wateja wakuambae mithili ya ibilisi
MASWALI
a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka (alama 1)
b) Shairi hili ni la aina gani (alama 2)
c) Tambua tamathali zozote mbili za usemi zilizotumiwa na mtunzi. (alama 4)
d) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha nadhari. (alama 4)
e) Wafanyikazi waliolengwa wataathirika vipi endapo hawatafuata ushauri wanaopewa kwenye shairi? (alama 3)
f) Eleza maana ya maneno yafuatayo. (alama 2)
i) Wakuapize
ii) Jasadini
g) Eleza nasaha yoyote inayotolewa kwa wafanyikazi wowote watatu. (alama 4)
20 marks