KNEC KCSE Kiswahili Paper 1 Question Paper / 2015 KCSE Tharaka South Joint Examination
2015 KCSE Tharaka South Joint Examination
Kiswahili Paper 1
LAZIMA
Wewe ni Mwalimu Mkuu. Mwandikie barua ya mapendekezo mwanafunzi wako anayanuia kujiunga na Chuo Kikuu nje ya nchi.
20 marks
Ni hatua zipi zinahitaji kuchukuliwa ili kukubaliana na tisho la ukame nchini.
20 marks
Mwenda juu kipungu hafikii mbinguni.
20 marks
Malizia kwa
…….Tangu siku hiyo niliamini kwamba ukuukuu wa kamba si upya wa ukambaa.
20 marks
KISWAHILI PAPER 1 MARKING SCHEME
2015 KCSE Tharaka South Joint Examination
Kiswahili Paper 1
Lazima
– Barua hii iwe na anwani tu:
Anayeandika
Jina la shule
S.L.P
– pawe na tarehe chini ya anwani
– upande wa atakayeipokea iwe ni : kwa anayehusika
– mint: itaje majina na nambari ya usajili ya unayependekezea
– piga mstari chini ya mintarafu
– maudhui- eleza wasifu kuhusu huyo mwanafunzi, masomo, utendakazi n.k. sifa ziwe nzuri ili apate nafasi
– tamati- ichukue muundo wa barua rasmi
– akifisha
– andika cheo cha aliyeandika mapendekezo
– utangulizi- ianze kwa ujumbe mkuu ulio kwenye mada ya barua
20 marks
Ukame ni hali ya nchi kuwa kavu kiasi cha kutowezesha kupata mavuno ya kutosha Hatua
– Kunyunyuzia mashamba maji hasa sehemu kame
– Kupanda miti ili kisaidia kuvutia mvua
– Kuhifadhi miti ili kuzuia mmomonyoko wa udongo
– Kutolima kandokando ya mito ili kuhifadhi chemichemi za maji
– Viwanda vinavyotoa kemikali zinazochangia kuharibika kwa hewa kuwekewa sheria za kufuata
– Kutochoma makaa
– Kupunguza idadi kubwa ya mifugo wanaolishwa katika maeneo mbalimbali nchini
– Adhabu ya kisheria kupatiwa wanaoharibu mazingira kama vile kukata miti na kuchoma makaa
20 marks
Mwenda juu kipungu hafiki mbinguni
– insha ya methali
– kichwa kinaweza kunukuu methali nzima
– maelezo ya methali si lazima yatolewe
– kisa kiwe na maudhui ya kudhihirisha maana ya methali
– kisa kitiririke na kuwa na mwanzo, upeo na mwisho
20 marks
Insha ya kumalizia, mtahiniwa ajieleze kwa kutungia kisa kinachosimulia kuwa kitu kipya duni na kinachovutia si kizuri kuliko cha zamani chenye kukufaa.
– malizia kwa maneno uliyopewa bila kuongeza chochote/ (neno) la kibinafsi lolote
– asianze kwa kifungu alochopewa- akifanya hivyo amejitungia swali
20 marks