KCSE Kiswahili Paper 3 – 2015 KCSE Ikutha Sub-County Joint Examination
2015 KCSE Ikutha Sub-County Joint Examination
Kiswahili Paper 3
1.SEHEMU YA A: USHAIRI (Alama 20)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo.
Vile lelo walalama, kwa yale ulotendewa,
Huyakumbuki ya nyuma, pindi ulipochachawa,
Ulipotenda unyama, uliona ndiyo sawa,
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!
Ulizusha uhasama, leo wewe wapagawa,
Walia bila kukoma, tungadhani umefiwa,
Sasa huna usalama, huwezi kujiopowa
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!
Tenda mambo kwa kupima, usiruke huna mbawa,
Una macho kutazama, na akili umepewa,
Matendo hurudi nyuma, atendaye hurudiwa,
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!
Dunia haishi njama, sijione umepewa,
Ukadhani usalama, binadamu kuwagawa,
Ukahisi ni wanyama, waso hali kama ngawa,
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!
Unapotenda zahama, siku yako itakuwa,
Ambapo utaungama, useme umechachiwa,
Na uanze kutetema, ulie umeonewa,
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa.
Maswali
a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 2)
b) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu. (alama 2)
c) Eleza muundo wa ubeti wa pili. (alama 4)
d) Ni kaida zipi za utunzi zilizozingatiwa na mshairi? (alama 2)
e) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya mjazo. (alama 4)
f) Toa mifano miwili ya idhini ya mshairi. (alama 2)
g) Kwa nini msemewa hafai kulalamika ? (alama 2)
h) Eleza maana ya maneno yafuatayo.
i) Uhasama (alama 1)
ii) Umepowa (alama 1)
20 marks
2. SEHEMU YA B: RIWAYA (Alama 20)
Kidagaa Kimemwozea: Ken Walibora
…unaa…seema mimiiii sipakui?…wataka mimi nipike? Ehee? Ati mimi nalaza damu? Wewe
unaiamsha damu?
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Eleza mbinu zozote tatu za lugha zilizotumika katika dondoo hili. (alama 6)
c) Jadili ufaafu wa anwani kwa kurejelea mnenaji. (alama 10)
20 marks
Eleza jinsi mbinu ya tabaini inavyojitokeza katika riwaya ya kidagaa kimemwozea.
20 marks
3.SEHEMU YA C: TAMTHILIA (Alama 20)
Mstahiki Meya:Timothy Arege. Jibu swali la 4 au 5
“Hawa ndio watu muhimu katika ulimwengu wa sasa”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Fafanua mchango wa mrejelewa katika kusambaratisha baraza la Cheneo. (alama 4)
c) Cheneo imekandamizwa kutokana na wakazi wake kutotumia akili. Fafanua kauli hii kwa kurejelea
tamthilia nzima. (alama 12)
20 marks
Tamthilia ya Mstahiki Meya ni taswira kamili ya mataifa mengi barani Afrika. Thibitisha kauli hii.
20 marks
4.SEHEMU D: HADITHI FUPI (Alama 20)
Ken Walibora na Said A. Mohamed: Damu Nyeusi
“Hapa huingii bila kuninyoshea mkono…”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Eleza sifa nne za mzungumziwa. (alama 4)
c) Kwa kurejelea muktadha wa hadithi nzima. Thibisha ukweli wa kauli kuwa mkono mtupu haulambwi
(alama 12)
20 marks
Kwa kurejelea hadithi ya Mke Wangu eleza mambo yanayochangia kuimarika kwa ndoa.
20 marks
5. SEHEMU YA E: (Alama 20)
FASIHI SIMULIZI
a) Nini maana ya maghani ? (alama 2)
b) Eleza aina za maghani zifuatazo. (alama 10)
i) Vivugo
ii) Tondozi
iii) Sifo
iv) Tendi
v) Rara
c) Eleza sifa nne za maghani. (alama 4)
d) Taja umuhimu wa maghani. (alama 4)
20 marks