KNEC KCSE Kiswahili Paper 2 Question Paper / 2015 KCSE Meru South Form 4 Joint Examination
2015 KCSE Meru South Form 4 Joint Examination
Kiswahili Paper 2
1. UFAHAMU (Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho ujibu maswali:
KARATASI YA 2
Tunapoakisi hatua ambayo mfumo wa kiteknohama umepiga misamba, kizazi cha vichakazi (facebook) kimetoweka na kupisha kile cha kututumiwa (GMO). Sidhalilishi hivi vikembe na vijikembe vya kututumuliwa japo kunao wenye falfasa hasi kuhusu vikembe hivi. Vijetegemeo mji wao ja waso haya.Hivi vya kutitimuliwa vina mitindo anuai ya kujinakia.Kama wewe si kufu au lahiki yao basi wewe jua bayana kuwa umepitwa na wakati. Utembeapo katika vitongoji vya janibu hizi si Gitau hadi Kaanwa, si Thuchi hadi Mutuati…sisemi Mukothima, utapatana na vikembe HIVI VYA KUTUTUMULIWA. Barobaro hujivika magwanda yanayoonekana kama yatabambuka wakati wowote na kuacha wazi sehemu tunazotegemea.
Vijembe navyo huwa vimejisetiri nusu kwa vijigwanda ambavyo vimeundwa kutoka kwenye shashi. Wafahamu shashi?Kile kitambaa kidogo cha kupangusia pua. Japo mimi vizazi hivi huviona maridadi na anisi, ni yakini kwamba maadili yamewapaa kabisa. Maghulamu wa kukutumuliwa hutembea kwa miondoko au kwa kudakia ukipenda. Zamani nikiwa mdogo tulivaa kaptura na shati za kawaida.Tulijinakia kuchezea matope huku tukivaa nguo safi siku ya Dominika pekee.
Vikembe vya kututumuliwa daima vina vidubwasha maskioni vikiburudika kwa mahadhi ya miziki kutoka kwenye simu zao za ruhunu. Hata kikutane na nani au nani sharti ampishe njia.Enzi zetu mwalimu hakuwa akifanya mambo mengine kama vile kula aina fulani ya chakula sisemi hata kwenda haja. Ukipatana naye njiani wee! Sharti utafute mahali ujifiche mpaka mwalimu apite.Vikembe vya kututumuliwa huwa tunaviheshimu sana.
Mara nyingi vitakuona vipi na huku vikembe na vijikembe hutembea huku vimepatikana kama mwanakima na mamake. Waso haya wana mji wao.Ukikutana nvyo njiani utatamani kurudisha saa yako ya maisha nyuma kidogo. Lakini ndugu, ujajani moshi, ukienda .. Hubagui baina ya vikembe na vijikembe kwani wote vipuli vimebanwa katika sikio moja na kama si moja kijikembe cha kututumuliwa huwa na kipuli kirefu kifikiapo hadi begani.Kijikembe hutembea huku kimesetiri miguu yake kwa jumu yake kwa jumu ambazo zimefika hadi kwenye goti. Na visigino je? Yuatembeahuku akihofu ardhi isibonyee au kuseteka.
/Enzi zetu kila baada ya shughuli za shule jioni tulikuta faradhi za kila nui zatusubiri. Mojawapoilikuwa kuwapeleka mifugo malishoni. Kizungumkuti kilikuwa pale ambapo katika michezo yetu ya vijana, ng’ombe wataishia katika shamba la jirani. Jioni hiyo sharti uyatayarishe sisemi makalio kwa utovu wa tafsida Lakini mijeledi itazuru hapo si katiyi.
Vile vikembe vyetu vya kututumuliwa vitakuwa pengine kwenye runinga au kwenye simu zao za rununu na wakati mwingine vimepakata vipakatalishi huku vikibovya vidude hapa na pale. Kila shughuli yao huwa ya mwendo wa pole pole havina mchapuo. Vinyonge hivi si kama vya enzi ya mababu zetu ambao walikuwa wakichapa mpira juu na kuketi kunusa ugoro huku wakisubiri mpira urudi ndiposa waendelee na mchezo wao.
Vikembe vya kutumuliwa huupisha tu na kikiteleza na kuanguka kidogo basi, mchezo umekoma hadi kipelekwe si zahanatini Lakini katika hospitali kuu ya daraja latano.
Kila jumapili jirani yangu alikuwa na zamu ya kushughulikia kichwa change kwa wembe wake. Hakuwa na shufaka au huruma ukipenda. Kichwa kilibaki kama kupe. Usishtuke kuviona vikembe vya kututumuliwa vichwa vyao vina ukwasi wa nywele si kipilipili bali kama za Bob Marley. Naona kana kwamba siku hizi kunz uhaba wa vinyoleo
.
Sisemi kizazi kimetukinai, hata chembe. Ni kwa kiteule kwa hivyo tusikipurukushe au kukinyanyapaa. Kila uchao lawana zaradidiwa kuhusu kizazi hiki. Haya ni mambo mazito ja jabali na hivyo basi kinachobaki ni kukihusisha katika ushaui na nasaha. La sivyo sisi wenyewe ndio tutakuja kulio kilio cha mbwa mdomo juu.
Maswali
a) Ipe taarifa hii anwani mwafaka. (alama 2)
b) ‘Kizazi chetu kimekosa maadili.’ (alama 3)
Thibitisha kwa mujibu wa taarifa hii.
c) Eleza tofauti nne ambazo mwandishi ameangazia kati ya kizazi cha zamani na kile cha kisasa. (alama 4)
d) Mwandishi anamaanisha nini kwa : (alama 3)
i. …umepitwa na wakati
ii. …vimeundwa kutoka kwenye shashi
iii. mijiledi itazuru hapo si katiti
e) Eleza maana za maneno haya kama yalivyotumiwa katika taarifa. (alama 3)
i. kujinaki
ii. faradhi
iii. tusikipurukushe
15 marks
2. MUHTASARI/UFUPISHO (Alama 15)
Soma taarifa ifuatyo kasha ujibu maswali kulingana na maagizo:
Inaridhisha kuyasikia mengi kuhusu mikakati ambayo serikali imeanzisha kuimarisha maendeleo ya nchi.Ni kweli kuwa maendeleo huhitajika kuonyesha mafanikio ya nchi ili kumaliza umaskini nchini.Ni juzi tu serikali imeanzisha ujenzi wa reli ambao umeibua malumbano mengi pamoja na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta ukiwa miongoni mwa miradi mengine mingi.
Kuna mipango kabambe ya kuwezesha usafiri wa maji uimarike zaidi katika mto Nile ili manufaa yake pia yaonekane katika eneo la Afrika mashariki sio tu Misri.
Ustawi wa taifa pia umelengwa kwa kupigia debe swala la pesa mashinani ili serikali za gatuzi ziweze
kufadhili miradi moja kwa moja bila kutegemea serikali kuu.Na Ikiwa ugatuzi huu utafaulu basi vijana na wanawake washugulikiwe kwa kuwapa mikopo ya kuanzisha biashara ndogo ndogo.
Maendeleo hayawezi kuimarika bila ujenzi na upanuzi a barabara ili kukuza teknolojia ya mawasiliano.Jambo hili litarahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Elimu pia ni kigezo muhimu na msingi thabiti wa kuega uchumi kwa kila nchi.Katika mabara yalioendelea asilimia kubwa ya wnanchi huwa na kiwango cha juu cha elimu.Kwa hivyo ni jambo muhimu kwa serikali kutoa elimu ya bure katika shule za msingi hadi shule za upili.Pia kilimo kipanuliwe kwa kutumia mbinu za kisasa na teknolojia mpya iwezeshe kwa hali na mali mashambani ili kuwaajiri watu wengi katika sekta hiyo.
Azma na matumaini ya kila nchi kuendelea hukabwq na matatizo kwa kuwa Fedha zinazohitajika zinashinda hata bajeti y mwaka mzima ya nchi hizo.Kuna uhaba mkubwa wa wataalamu mbalimbali wenye ujuzi wa kufaa katika sekta nyingi hapa nchini.
Pamoja na kuweko kwa viongozi wenye matumbo makubwa ambao humimina Fedha zenye manufaa kwa wananchi,kuna ukosefu wa vifaa vya kisasa vinavyorahisisha utenda kazi.Vikiwepo huwa duni kulingana na viwango vya maendeleo.
Kuna pengo kubwa sana kati ya matajiri na maskini hivi kwamba itachukua muda kuyashawishi matabaka haya mawili.Takwimu sahihi ya mahitaji ya watu katika maeneo fulani yahitajika ili serikali iweze kusambaza miradi kulingana na jinsi eneo lilivyo.Wamiliki ardhi kubwa wamekuwa na mzizi iliyokita kwenye ulingo wakisiasa hivi kwamba ni vugumu na hatari kugusia suala la umiliki wa ardhi.
a) Ni juhudi zipi zilitiliwa maanani kuimarisha uchumi? (maneno 55) (alama 6,1 ya utiririko)
Matayarisho
jibu
b) Kwa maneno yasiyozidi 55 fupisha aya tatu za mwisho. (alama 7, 1 ya utiririko)
Matayarisho
Jibu
15 marks
3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
Jibe maswali yafuatayo.
Andika mifano minne ya vitenzi vya silabi moja katika ya kutendesha.
2 marks
Unda sentesi yenye muundo ufuatao :
KN(N+V),KT(t+ V+E)
2 marks
Taja sifa inayotofautisha sauti / ny/na/ng/
2 marks
Ainisha vihusishi katika sentensihii :
Tulichakura tarakilishi ya mwalimu iliyokuwa kando ya dawati baada ya mtihani kukamilika.
3 marks
Tumia kiunganishi seuze / sembuse katika sentensi.
2 marks
Eleza maana tatu za sentensi hii.
Chakula kingine kimeliwa na wageni.
2 marks
Ainisha vitenzi katika sentensi hii.
Hawa ndio wageni tuliokuwa tukingojea kwa hamu.
2 marks
Hizi ni mofimu za aina gani?
Kiwavi
Miwani
Karatasi
3 marks
Akifisha
Toka nje au niku nyanya akaamuru murithi
3 marks
Changanua kwa kutumia vishale.
Swali hilo lilikuwa rahisi sana.
5 marks
Yakinisha
Chakula hakiko tayari hivyo wageni wasinawe mikono.
2 marks
Ainisha vishazi katika sentensi hii.
Kama nitamkuta nyumbani nitamshauri asome kwa bidii.
3 marks
Tunga sentensi ya neno moja yenye sehemu zifuatazo :
Kikanushi
Hali timilifu
Mtendewa
Kitenzi cha silabi moja
Kauli ya kutendesha
Kiishio
3 marks
Andika katika usemi wa taarifa :
“Mkishinda timu hii leo nitamtuza.”Mkufunzi akatwambia.
3 marks
Tambua yambwa na ueleze ni za aina gani.
Wazazi waliwanunulia wanafunzi bora zawadi nyingi kwa hundi.
2 marks
Nyambua neno hili katika kauli ya kutendesha.
1 marks
4. ISIMU JAMII (Alama 10)
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali
Anachukua ile ngoma kijana Rooney,
Kwake chicharito…anaachenga moja , mbili
Hatari! Hatari! Hatari kwenye lango..
a) Hii ni sajili gani? (alama 2)
b) Eleza sifa nane za sajilli hii. (alama 8)
10 marks
KISWAHILI PAPER 2 MARKING SCHEME
2015 KCSE Meru South Form 4 Joint Examination
Kiswahili Paper 2
1. UFAHAMU (Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho ujibu maswali:
a) Kizazi cha kisasa
Kizazi cha kututumiliwa
(anwani ioane na taarifa)
b) i) kuvaa mavazi ambayo hayasetiri miili yao kabisa
ii) hawawapishi njia/ hawaheshimu wakubwa wao
iii) hutembea njiani wameshikana bila haya
c) i) kizazi cha zamani kilivaa mavazi ya kawaida lakini cha kisasa huvaa mavazi ambayo huziacha sehemu nyingine zikiwa wazi
iii) kizazi cha zamani kiliheshimu wakubwa hawa walimu lakini cha kisasa hawawaheshimu hata kuwapisha njia
iv) kizazi cha zamani kilikuwa na kazi kama kupeleka ng’ombe malishoni lakini cha kisasa hushinda
kutazama runinga na kuchakura katika vipakatalishi au rununu
iv) vizazi vya zamani vilikuwa na nguvu lakini vya kisasa huwa dhaifu
v) vizazi vya zamani vilikuwa na nywele fupi lakini vya kisasa vinaweka nywele kubwa na husokotwa
d) i) wewe si wa kisasaa/ hujazinduka
ii) nguo ndogo sana
iii) utachapwa/ utapigwa
e) i) kujinakia- kujisifu/ kujigamba/ kujibondoa/ kujifaragua
ii) faradhi- wajibu/ jambe la lazima / sharti
15 marks
2. MUHTASARI/UFUPISHO (Alama 15)
Soma taarifa ifuatyo kasha ujibu maswali kulingana na maagizo:
A
− serikali imeanzisha ujenzi wa reli
− upanuzi wa uwanja wa ndege
− kuwezesha usafiri wa maji kuwa bora zaidi katika mto Nile
− kupigia debe mipango ya pesa mashinani
− mikopo kwa vijana na wanawake
− ujenzi na upanuzi wa barabara
− kutoa elimu ya bure kwa shule za msingi na upili
− kuinua kilimo kwa wananchi
b
− pesa zinazohotajika zinashinda hata bajeti ya mwaka
− kuna uhaba wa wataalamu wenye ujuzi
− viongozi wenye matumbo makubwa ambao umimina pesa
− ukosefu wa vifaa vya kisasa
− hakuna takwimu sahihi ya mahitaji ya maneno mbalimbali
− kuwa na pengo kubwa kati ya matajiri ya maeneo mbalimbali
− wanaomiliki ardhi kubwa kuwa na mzizi uliokita kwenye ulingo wa kisiasa
− ni vigumu na hatari kugusia suala la umiliki wa ardhi
15 marks
3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
Jibe maswali yafuatayo.
Fisha/ lisha/ nywisha au nywesha/ chisha/ fisha
2 marks
Kitabu hicho kilikuwa kizuri sana
2 marks
/ny/ hutamkiwa katika kaakaa gumu lakini sauti /ng’/ hutamkiwa katika kaakaa gumu
2 marks
Baba alinunua gari seuze/ sembuse baiskeli. (shartisentensi ionyeshe kitu kimoja kikiwa kikubwa au na uwezo kuliko kingine)
3 marks
Chakula zaidi ya……
Baadhi ya chakula
Chakula tofauti na
2 marks
Ya- kihusishi cha la’ unganifu
Kando ya- kihushishi cha mahali
Baada ya- kihusishi cha wakati
2 marks
Ndio- kitenzi kishirikishi kipungufu
Tuliokuwa- kitenzi kisaidizi
Tukingojea- litenzi kikuu
Tuikuwa tukingojea- vitenzi sambamba
2 marks
Kiwavi- mofimu tegemezi
Miwani- mofimu huru
Karatasi- vitenzi sambamba
3 marks
“toka nje na niku…..!” Nyanya akaamuru Murithi
3 marks
S- KN + KT
KN- N+ V
N- swali
V- hili
KT- t+ V+ E
t- lilikuwa
V- rahisi
E- sana
5 marks
Chakula kiko tayari kwa hivyo wageni wanawe mikono.
2 marks
Ikiwa nitamkuta- kishanzi kitegemezi
Nitamshauri asome kwa bidii- kishazi huru
3 marks
Mfano: sijakulisha
3 marks
Mfukunzi alitwambia tungeshinda timu hivo siku hivo angetutuza
3 marks
Wanafunzi bora- yambwa tendewa
Azawadi nyingi- yambwa tendwa
Hundi- yambwa ala
2 marks
Jua- juza/ juvya
1 marks
4. ISIMU JAMII (Alama 10)
Sajili ya michezo
− Kuchanganya ndimi
− Kubadili ndimi
− Matumizi ya msamiati maalum wa michezo
− Hukiuka kanuni za kisarufi/ kuiboronga sarufi
− Hutumia mbinu ya utohozi
− Matumizi ya lugha ya mkato
− Matumizi ya uradidi wa maneno au kauli Fulani
− Matumizi ya misimu
− Matumizi ya lugha ya taharuki
− Matumizi ya majisifu mengi
− Kuna kutajataja majina ya wachezaji
Kila hoja sharti iandamane na mfano hai
Kama hoja haina mfano hai mtahiniwa atoe sababu za kutumiia aina hiyo ya lugha
Asipotumia mfano au sabbabu atuzwe nusu alamaMfukunzi alitwambia tungeshinda timu hivo siku hivo angetutuzaAzawadi nyingi- yambwa tendwa
Hundi- yambwa ala
10 marks