KNEC KCSE Kiswahili Paper 3 – 2015 – Machakos County Trial
2015 KCSE Machakos County Trial
Kiswahili Paper 3
SEHEMU YA A (Alama 20)
SHAIRI (Lazima)
Nimechoka
Nilivyofikisha hapa, na juu kupandishwa
Na kwa hila gani, au, zilipofungwa
Ncha za waya hii ngumu ya maisha, sijui.
Wanadamu wameinama.Wanasali kwa haraka sasa.
Utafikiri wanahesabu mchanga utakaojaza kaburi langu.
Vichwa vyeupe vinacheka.Kingine kinasema tena:
“Mnaliona Hilo! Joga !” Vichwa vinachela.Wanasali.
“Nyinyi nyote hamna akili!Mnaniudhi!
Hamwoni hali yangu!” Napiga kelele.Lakini vichwa
Havitishi,na wanadamu hawatingishiki.
Sauti ya baba inasema kwa msisitizo
“Najua utafika wakati itakulazimu kudondoka.
“Lakini unazo nguvu bado,na usikate tamaa,
Ila usitegemee kusifiwa au kusaidiwa;
Vichwa vyote hivi vilidondoka kutoka umbali huo,
Nawe kudondoka,utadondoka!
Ninaendelea kuning’inia.Nimechoka.Mikono
Inaniuma;hatari ya vitimbo.Vinacheka.Wanasali
Sasa wanaimba.Sitaki nyimbo zao;maana
Mimi bado nimeniong’inia na vitimbo having’oki.
Lakini pole pole ninaanza kutabasamu.
Sijafikia hatua ya kucheka;maana nimechoka,
Kichomi kimenipata na sijadondoka
Lakini najiona nimening’inia kama ndege
Aliyenaswa na mtego wa mtoto mdogo
Mimi,Lakini ni mwanadamu na akili zangu
Timamu.Ninaweza kudondoka, kama nikipenda.
Lakini ninaogopa chini yangu naona miti
Iliyochongwa ikifuata usawa wa waya hii,
Ikingoja kwa hamu,kama mshikaki kunichoma,
Kunitoboa na kufurahia kimya kimya,
Uzuri wa kupita katika mwili mwororo wa binadamu.
Lazima nishike kwa nguvu nisianguke kama kifurushi
Cha pamba cha mtoto mdogo kilichokwisha pimwa.
Mikono inaniuma, na waya imekwishanikata vidole.
Damu imetiririka hadi kwapani;kujipangusa siwezi.
Nimechoka.Kadiri niendeleavyo kunig’inia, ndivyo
Sura yangu ionyeshavyo vizuri alama za uchovu.
Ninatazama huku na huko kuwatafuta wenye huruma.
Lakini wanadamu wote wazima wanainamisha vichwa
Chini kama kwamba hawanijui;hata jamaa zangu!
Ninaendelea kuning’inia kama picha iliyotundikwa
Katika shamba la mawele, na mwenye shamba
Huvuta waya kutoka nyumbani,itingishike kuwatisha
ndege.
Machozi yananitoka,kuyapangua siwezi.
Ninajitahidi kutoa sauti kwa nguvu;
“Jamani e! Nisaidie! Ng’oeni hivyo vitimbo!”
Lakini wanadamu wameinama.Wanaanza sasa kusali.
Kati ya vitimbo, vichwa vinazuka ardhini
Ukweli wa maisha unakuwa kama ndoto ya uwongo.
Kichwa kimoja kinasema kwa sauti “Mnaliona Hilo!”
Halafu vichjwa vyote vyeupe vinacheka.Ninashangaa.
Ninashangaa zaidi kusikia sauti ya baba
Ikicheka miongoni mwa vichwa hivyo vyeupe.
Siyaamini macho,siyaamini masikio, sikiamini kichwa.
Maswali:
1. Shairi hili ni la “udhanaishi” Fafanua kauli hii. (alama 4)
2. Eleza kwa kutoa mifano miwili, jinsi msanii alivyotumia tamathali zifuatazo (alama 6)
(a) Jazanda
(b) Uhuishi
3. Andika ubeti wa saba kwa lugha tutumbi. (alama 4)
4. Eleza maana ya mishororo “vichwa vyote hivi vilidondoka kutoka umbali huo, nawe kudondoka
utadondoka”. (alama 2)
5. Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
20 marks
SEHEMU YA B (Alama 20)
RIWAYA: Kidagaa Kimemwozea
“….usiniweke pembeni kama tanbihi, mimi na wanawake wenzangu kama wanaume wengine
wafanyavyo waandikapo…”
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Fafanua mbinu mbili za uandishi zilizotumika hapa (alama 2)
c) Hakiki usawiri wa wahusika wa kike katika riwaya hii (alama 14)
20 marks
Wananchi wa Tomoko wamesalia katika ndoto ya uhuru.Dhibitisha ukweli wa kauli hii.
20 marks
SEHEMU YA C (Alama 20)
TAMTHILIA: Mstahiki Maya
“Si ninyi nd’o mjuao wanangu!..nilikiona afadhali”.
(a) Eleza muktadha wa maneno haya (alama 4)
(b) Taja na utolee mifano ya mbinu zozote mbili za uandishi zilizotumika katika kifungu hiki.
(alama 4)
(c) Fafanua maudhui yanayorejelewa na dondoo hili. (alama 12)
20 marks
“Mtu huvuna alichopanda.Ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
b) “Ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi” ina maana gani kulingana na muktadha huu. (Alama 6)
c) Taja na ueleze matendo mengine manne ya kuonyesha kuwa walipanda pojo na kuvuna pojo si
kunazi. (Alama 8)
d) Taja tamathali za usemi zilizotumiwa katika dondoo hili. (Alama 2)
20 marks
SEHEMU YA D (Alama 20)
HADITHI FUPI: Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine Ken Walibora na Said A.Mohaned
“Kama alivyoshinda nani Yule….nunez?”
a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake. (Alama 4)
b) Linganua sifa nne za msemaji na msemewa katika dondoo hili. (Alama 8)
c) Kwa kurejelea hadithi nzima eleza hisia za utamaduni ulipitwa na wakati. (Alama 6)
d) Ni mbinu zipi za lugha zilizotumika katika dondoo hili? (Alama 2)
20 marks
Mwanamke katika diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine amepewa nafasi finyu.
Fafanua kwa kuzingatia hadithi zozote nne.
20 marks
SEHEMU YA E (Alama 20)
FASIHI SIMULIZI
a) Eleza maana ya maghani (alama 2)
b) Fafanua sifa nne za maghani (alama 4)
c) Taja njia zozote nne za kuhifadhi kazi za fasihi simulizi katika jamii. (alama 4)
d) Fafanua hatua za ukusanyaji wa data katika fasihi simulizi (alama 5)
e) Eleza matatizo yanaokabili fasihi simulizi katika jamii ya sasa (alama 5)
20 marks