KNEC KCSE Kiswahili Paper 3 Question Paper / 2015 KCSE Gem Sub-County Joint Evaluation
KISWAHILI PAPER 3 QUESTION PAPER
2015 KCSE Gem Sub-County Joint Evaluation
Kiswahili Paper 3
1. LAZIMA (Alama 20)
Kutowajibika kwa viongozi barani kumesitishapakubwa maendeleo. Dhihirisha.
20 marks
2.RIWAYA (Alama 20)
Kidagaa Kimemwozea : Ken Walibora Jibu swali la 2 au la 3
“ ……Unaa … seema mimi sipakui? Wataka mimi nipike?
a) Eleza muktadha wa dondoo hii. (alama 4)
b) Kwa kutoa mifano mitatu. Eleza nafasi ya msemmewa na jinsia yake katika riwaya. (alama 6)
c) Eleza umuhimu wa msemaji kwa mujibu wa riwaya nzima. (alama 10)
20 marks
Eleza visababishi vya mafarakano katika ndoa kwa mujibu wa riwata “Kidagaa Kimemwozea”.
20 marks
3.HADITHI FUPI (Alama 20)
Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine Jibu swali la 4 au la 5
“Hapa huingii bila kuninyoshea mkono……….”
a) Eleza muktadha wa dondoo hii (alama 4)
b) Eleza sifa nne za mzungumziwa. (alama 4)
c) Kwa kurejerea muktadha wa hadithi nzima thibitisha ukweli kuwa mkono mtupu haulabwi.(alama12)
20 marks
Haki za watoto zimekiukwa pakubwa katika Diwani ya Damu Nyeusi. Dhihirisha kwa kurejerea.
i) Kanda lausufi
ii) Maskini Babu yangu
iii) Mwana wa Darubini
iv) Mizizi na matawi
20 marks
4.USHAIRI (Alama 20)
Jibu swali la 6 au la 7
Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali.
Maswali
i) Lipe shairi hili anwani mwafaka. (Alama 1)
ii) Kwa nini Utungo huu ni shairi? (alama 4)
iii) Kwa nini mshairi hataki kukumbushwa yaliyopita? (alama 2)
iv) Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari. (alama 4)
v) Taja na ueleze Mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika Utungo huu. (Alama 4)
vi) Fafanua umuhimu wa uhuru wa msahairi uliotumiwa. (alama 2)
vii) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika ushauri. (alama 2)
a)amesubutu
b)majinuni
20 marks
Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali
Maswali
a) Lipe shairi hili kichwa kifaacho. (Alama 1)
b) Fafanua jinsi idhini ya kishairi inayodhihirika katika shairi hili. (alama 4)
c) Mtunzi ametilia shaka masuala kadhaa. Yataje. (alama 5)
d) Andika ubeti wa tatau katika ligha ya kiriwaya. (alama 4)
e) Taja na ueleze mkondo wa shairi hili. (alama 4)
f) Eleza msamiati huu kama ulivyotumika katika shairi : (alama 2)
a) Anapakasa
b) Pakari
20 marks
5.FASIHI SIMULIZI (Alama 20)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Salimu alikumbana na mwanadada aliyejisikia sukari! Wacha aringiwe ile mbaya ! Alishindwa vya
Kuwaelezea marafikize waliomsubiri pembeni akaamua Kuingia mtini.
a) Tambulisha kipera hiki kwa mujibu wa sehemu zilizo pigiwa mstari. (Alama 2)
b) Ni nini maana yake ? (a) hapo juu (alama 2)
c) Eleza sifa zozote nne (4) za kipera hiki. (alama 8)
d) Eleza majukumu yoyote manne (4) ya kipera hiki katika jamii. (alama 8)
20 marks