KNEC KCSE Kiswahili Paper 3 Question Paper / 2016 Pre KCSE
2016 Pre KCSE
Kiswahili Paper 3
SEHEMU A: RIWAYA (Alama 20)
Ken Walibora: Kidagaa Kimemwozea.
LAZIMA
Kuvunjwa kwa haki na sheria lilikua jambo la kawaida chini ya uongozi wa mtemi Nasaba
bora.Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejarelea riwaya.
20 marks
SEHEMU B: TAMTHILIA (Alama 20)
Timothy M. Arege: Mstahiki Meya
Hatua tuchukuazo maishaini mwetu zaweza kutuathiri na kuathiri nchi pakubwa. Fafanua kauli hii
ukimrejerelea Meya Sosi.
20 marks
Mwafulani I: Tulipoitwa kuhudumu tuliitika na hakuna kurudi nyuma..
Mwafulani II:Mara mbili hivi karibu niache kazi hii
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Fafanua maudhui yanayojitokeza katika mazungumzo hayo (alama 8)
c) Fafanua tabia za mwafulani wa kwanza na wa pili (alama 8)
20 marks
SEHEMU C: HADITHI FUPI (Alama 20)
Ken Walibora na Said A.mohamed: Damu Nyeusi
Maudhui ya ubaguzi na utabaka yamepewa uzito na waandishi wa Diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi nyingine. Kwa kurejelea hadithi zozote tano onyesha ukweli wa kauli hii.
20 marks
SEHEMU D: FASIHI SIMULIZI (Alama 20)
a) Maigizo ni nini (alama 2)
b) Andika sifa za maigizo (alama 4)
c) Ngomezi ni nini (alama 2)
d) Taja aina mbili za ujumbe ambazo zinaweza kuwasilishwa na ngomezi (alama 2)
e) Andika sifa za ngomezi (alama 4)
f) Miviga ni nini (alama 2)
g) Miviga ina umuhimu gani? (alama 4)
20 marks
SEHEMU E: USHAIRI (Alama 20)
Jibu swali la 6 au la 7
Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali
1. Tunda la elimu zote, wanasema wanazuoni
Ni kwamba mtu apate, kumtambua manani
Ndipo hadhi apate, akumbukwe duniani.
2. Elimu bila ukweli, haizidi asilani
Giza na nuru muhali, katu havitangamani
Uwongo ufe kweli, itue nuru moyoni
3. Elimu ni kama mali, haichoshi kutamani
Ni bora yashinda mali, taji la wanazuoni
Elimu njoma miali,langazayo gizani.
4. Mtu hachomwi na mwiba, na viatu miguuni
Ulimwengu una miiba, tele tele majiani
Elimu ukiishiba, u salama duniani.
5. Wafu ni wasiosoma, watazikwa ardhini
Hai ndio maulana,wapaao maangani
Elimu jambo adhima, aso nayo maskini.
6. Toa wakfu ujana, elimu ukitamani
Na uwe mzee sana, kujua usijihini
Elimu ni jambo adhima, aso nayo maskini
7. Elimu ina malipo, utoyalipwa mwishoni
Pale uitafutapo, ujira usitamani
Mwanachuoni afapo, mbingu huwa na huzuni.
8. Haki ya kuheshimiwa, ni yao wanachuoni
Wao wameongolewa, na ni taa duniani
Kweli wanapoijua, watoe bila kuhuni.
9. Elimu bila amali, mti usio majani
Haumtii kivuli, aukaliaye chini
Inakuwa mashkeli, wa kughuri insane.
Maswali
a) Toa kichwa mwafaka kwa shairi hili (alama 2)
b) Taja aina na bahari ya shairi (alama 3)
c) Eleza umbo la shairi (alama 6)
d) Fafanua maudhui katika ubeti wa tatu na wa saba (alama 6)
e) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya tutumbi/nathari. (alama 3)
20 marks
MASWALI
a) Andika anwani mwafaka ya shairi hili (alama 1)
b) Eleza muundo wa shairi hili (alama 4)
c) Taja vinyume kumi vinavyorejelewa katika shairi (alama 5)
d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari (alama 4)
e) Onyesha jinsi mwandishi ametumia idhini ya ushauri (alama 4)
f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi (alama 2)
(i) Pakari
(ii) Apakasa
20 marks
Nice job we need more papers