KNEC KCSE Kiswahili Paper 1 Question Paper / 2015 KCSE Gem Sub-County Joint Evaluation
KISWAHILI PAPER 1 QUESTION PAPER
2015 KCSE Gem Sub-County Joint Evaluation
Kiswahili Paper 1
Unataka kuwania Ugavana. Andika tawasifu watakayoisoma wapigakura ili wavutiwe kukuchagua.
20 marks
Tatizo la usalama nchini Kenya ni janga la kujitakia Jadili.
20 marks
Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti.
20 marks
Andika kisa kitakachoishia maneno haya : …nilitambua kwamba si vizuri kumtegemea mtu mmoja kwa hali na mali.
20 marks
KISWAHILI PAPER 1 MARKING SCHEME
2015 KCSE Gem Sub-County Joint Evaluation
Kiswahili Paper 1
TAWASIFU YA KUWANIA UGAVANA
Mtindo
a) Tawasifu- mtu binafsi anajielezea kwa nathari/ mfululizo
b) Maelezo yawe katika nafsi ya kwanza- umoja
1) Mada – TAWASIFU YANGU
2) Utangulizi:
− kujitambulisha
− jina
− mwaka wa kuzaliwa
− mahali pa kuzaliwa
− wazazi
− nafasi katika mzao/ familia
− familia yenu kimuhtasari
3) Mwili
a) Masomo
− chekechea
− msingi
− sekondari
− chuo
b) Kazi/ ujuzi
Mahali na muda
c) Mchango wako
Katika jamii
Katika vyama na shule
Uwezo wako kimaendeleo
d) Uanachama
Vyama mbalimbali na nafasi yako (vyeo)
e) Uraibu
Shughuli mbalimbali za ziada unazoshiriki
Shughuli unazopenda nje ya kazi yako rasmi
f) Hitimisho
Kuwaomba/ kuwahimiza wampigie kura
Tanbihi
i) Shughuli ulizojihusisha nazo katika taasisi za elimu na katika jamii zihusiane na zituelekezee kwenye msukumo
wa kutaka ugavana kama vile:
− vyeo/ nyadhifa za uongozi masomoni
− juhudi za maendeleo katika jamii
− juhudi za kusaidia wanajamii
− juhudi za kutetea haki za wanajamii
− utawafanyia nini
− Watarajie nini kutokka kwako
− Eleza uwezo wako
20 marks
SWALI LA PILI: USALAMA NCHINI
MTINDO
i) Insha ya mjadala
ii) Mtahiniwa atoe hoja za pande mbili
iii) Mtahiniwa ahitimishe kwa msimamo wake. Asimame upande wenye hoja nyingi au katikati iwapo hoja zitatoshana kiidadi
Maudhui
a) Kuunga mkono
i) Utepetevu wa walinda- usalama
ii) Ufisa wa Kenya kuingia Somali na al-shaabab
iii) Kutosomesha watoto
iv) Raia kutowajibika kuwafichua wahalifu
v) Mihadarati
vi) Tama
vii) Malipo duni kwa walinda usalama
viii) Umaskini
ix) ukabila
b) kupinga
i) uchache wa walinda
ii) ni tatizo la kimataifa- makundi ya kigaidi
iii) ni tatizo la kimaumbile kama vile mafuriko, radi,maporomoko ya ardhi
iv) umaskini
v) n.k
20 marks
SWALI LA TATU
Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti
Insha ya methali
Maana
Tusihadaiwe na uzuri wan je kutokana na mapambo ya kitu au mtu bali ni mihimu kuchunguza undani wake kwa
makini ili tubainishe uzuri wake
Mtindo
a) andika kinathari
b) kisa kiunge mkono baada na matumizi ya methali
c) kisa kikuze pande zote mbili kikamilifu
d) si lazima aeleze maana na matumizi ya methali
mielekeo
i) kufurahia uzuri wan je wa mtu au kitu baadaye kugundua ubovu au kasoro zilizofichika
ii) mtu aliyewahadaa watu kwa matendo mazuri hadharini (mbele ya watu) badaye akagunduliwa kuwa mtenda
maovu kisirisiri
iii) kiongozi wa kidini au mahali popote aliyehubiri maji na kunywa divai
iv) msichana mrembo sana ambaye alimvutia mwanamume aliyemuoa kumbe akagundua kasoro kubwa kwake
baadaye
v) na kadhalika
20 marks
SWALI LA NNE: MDOKEZO
MTINDO
a) mdokezo wa kumalizia kwa maneno ya mwisho uliyopewa
b) lazima maneno ya mwisho yawe yayo hayo
c) maudhui yahusu
i) mtahini aliyetegemea mtu mmoja kwa kila mahitaji yake na mtu huyo alipoondoka akawa hajiwezi tena
ii) mtahini aweze kuwa alishuhudia mume aliyeoa wake wengi akifa halafu wake na watoto wake kuzozana au
kukosa mahitaji yao/ kuwa katika hali duni
iii) mtahini kushuhudia raia waliomtegemea kiongozi au tajiri Fulani mmoja kwa mahitaji yao yote kasha
wakaishia ukosefu/ uhitaji mkuu kiongozi huyo alipoondoka.
20 marks