KNEC KCSE Kiswahili Paper 1 Question Paper / 2015 KCSE Kericho West Joint Examination
2015 KCSE Kericho West Joint Examination
Kiswahili Paper 1
Lazima
Kumekuwa na ongezeko la visa vya ubakaji nchini katika siku za hivi karibuni. Wewe umeteuliwa na waziri wa usalama wa jamii kuwa katibu wa jopo linalochunguza chanzo cha visa hivi na kupendekeza njia za kusitisha uovu huu. Andika ripoti yako.
20 marks
“Ulevi wa pombe haramu umeleta madhara mengi katika jamii ya leo.” Thibitisha ukweli wa usemi huu huku ukipendekeza hatua zitakazochukuliwa na serikali na jamii kutatua tatizo hili.
20 marks
Andika insha itakayodhihirisha ukweli wa methali hii.
Sikio la kufa halisikii dawa.
20 marks
Tunga kisa kitakachoisha kwa maneno yafuatayo:
… Hapo ndipo nilipogutuka kutoka usingizini. Mwili wangu ulikuwa umeloa jasho, nao moyo ulinipapa. Ndipo nilipong’amua kuwa yote hayo yalikuwa ruiya tu.
20 marks