KNEC KCSE Kiswahili Paper 3 – 2014 Gatundu Mock
2014 Gatundu Mock
Kiswahili Paper 3
SEHEMU A: (Alama 20)
TAMTHILIA Timothy M. Arege: Mstahiki Meya. (Swali la Lazima)
“Wapo sana. Lakini tuliopo ndio tuliochaguliwa…………..kwa nini basi kulalamika?”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili? (alama 4)
b) Fafanua kwa kutoa mifano sifa tatu za mzungumzaji? (alama 6)
c) Usaliti na ukengeushi ni miongoni mwa mambo muhimu yanayojitokeza katika tamthilia ya
mstahiki meya. Thibitisha. (alama 10)
20 marks
SEHEMU B: (Alama 20)
RIWAYA (Jibu swali la 2 au 3) Ken Walibora: Kidagaa kimewozea.
Kwa kutumia riwaya ya kidagaa kimemwozea jadili jinsi swala la ukoloni mamboleo na ulitima
limefafanuliwa.
20 marks
“alisimama jadidi na kuwatazama hawa watu wawili waliosimama wima kutetemeka kama
waliokuwa wamepigwa na dhoruba ya theluji”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Eleza hulka ya yule ‘alisimama dadidi na kuwatazama hawa watu wawili.” (alama 6)
c) Jadili mchango wa wanawake katika riwaya ya kidagaa. (alama 10)
20 marks
SEHEMU C: (Alama 20)
USHAIRI (Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata)
RABI HUMLIPIZIA
Pungueni uonezi, wanyonge kuwaonea
Kuwafanya wao mbuzi, mazizini kuwatia.
Muogopeni Mwenyezi, haki mkiwapatia.
Rabi humlipizia, Mnyonge mkosa haki.
Rabi kumeza hawezi, dhuluma isiyo njia,
Atatoa uamuzi, haki inayopotea,
Daima kwake machozi, kuna kilio kulia,
Rabi humlipizia, Mnyonge mkosa haki.
Niyanenayo sadiki, alikilini kuyatia,
Aloshikilia haki, hatafikwa na hatia,
Punguzeni unafiki, kuzua mkichelea
Rabi humlipizia, Mnyonge mkosa haki.
Haki haifichamiki, japo iwe myaka mia,
Mwenyezi Mungu mwehaki, haki ataifichua
Awatenge wanafiki, haki mnaoumbua,
Rabi humlipizia, Mnyonge mkosa haki.
Kuna kundi lake laki, limekaa langojea,
Kukalia unafiki, mwashibota kuwania,
Punguzeni mwabonaki, mumde mola jalia
Rabi humlipizia, Mnyonge mkosa haki.
Rabi atawafedhehi, haki wanayoumbuwa,
Na mwisho awakebehi, avunje wenu uluwa,
Mwenzi wenu nimewahi, Mungu ameniokowa,
Rabi humlipizia, Mnyonge mkosa haki.
(kutoka: Diwani ya Akilimali, Akilimali, S.E.AL.B; Uk 54)
Maswali
a) Taja umuhimu ya kutenda haki. (alama 4)
b) Taja mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi hili. (alama 2)
c) Shairi hili linaweza kuwa katika bahari mbili. Zitaje (alama 2)
d) Taja na ueleze mifano miwili tofauti ya uhuru wa kishairi uliotumika. (alama 2)
e) Mshairi alikuwa na dhamira ipi alipotunga shairi ili. (alama 2)
f) Andika ubeti wa 3 kwa lugha ya nathari. (alama 4)
g) Eleza muundo wa ubeti 2 (alama 2)
h) Fafanua maana ya :
(i) Awatenge wanafiki, haki mnaoumbua.(alama 2)
20 marks
SEHEMU D: (Alama 20)
FASIHI SIMULIZI
(i) Misimu ni nini (alama 2)
(ii) Eleza sifa tano za misimu. (alama 10)
(iii) Fafanua majukumu yoyote manne yanayotekelezwa na misimu. (alama 8)
20 marks
a) Maghani ni nini? (alama 2)
b) Eleza fani zifuatazo za maghani. (alama 8)
(i) Tondozi
(ii) Pembezi
(iii) Tendi
(iv) Rara
c) Eleza sifa tatu za maghani. (alama 6)
d) Taja dhima nne za maghani. (alama 4)
20 marks
SEHEMU E: (Alama 20)
Hadhithi Fupi. Ken walibora na Said A. Mohammed: Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine.
Tukio lililowaleta hapa ni la kawaida kwetu. Ingawa sisi hufanya tuwezayo kuwalinda wanetu, mara
nyingi tabia zao hutupiga chenga……………………..”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Eleza sifa nne za mzungumzaji. (alama 8)
c) Jadili matatizo manne yanayojitokeza katika hadithi hii. (alama 8)
20 marks