SUZA yakabidhiwa rasmi taasisi za Elimu Zanzibar
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar tarehe 16 Januari, 2017 ilikabidhiwa rasmi Chuo cha Utawala wa Fedha Zanzibar (ZIFA), Chuo cha Sayansi za Afya (CHS), na Taasisi ya Maendeleo ya Utalii Zanzibar (ZIToD) ambazo zote kwa pamoja sasa zinakuwa chini ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).
Makabidhiano hayo yalifanywa na Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Afya ambaye aliikabidhi CHS, Mheshimiwa Rashid Ali Juma, Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo aliyeikabidhi ZIToD na Mheshimiwa Dkt. Khalid Salum Mohamed, Waziri wa Fedha na Mipango ambaye aliwakilishwa na Bwana Iddi Haji Makame, Kaimu Mkuu wa ZIFA
Makabidhiano hayo yalifanyika kufuatia Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mnamo tarehe 16 Oktoba, 2016 kuidhinisha kuunganishwa kwa taasisi hizo kwa kusaini Sheria namba 7 ya mwaka 2016 iliyopitishwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na kufuta Sheria zilizoanzisha taasisi hizo. Aidha Sheria hiyo iliyosainiwa na Dkt. Shein kuunganisha taasisi hizi imeifanyia marekebisho Sheria Namba 11 ya mwaka 2009 ambayo nayo iliirekebisha Sheria Namba 8 ya 1999 ambayo ndio
ilianzisha Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.
Taasisi zilizounganishwa na SUZA zitaendesha shughuli zake kama kawaida lakini zikiwa na majina mengine ambapo iliyokuwa ZIFA sasa itakuwa ni Skuli ya Biashara, CHS itakuwa chini ya Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ambapo ZIToD itakuwa ni Taasisi ya Maendelo ya Utalii.
1 thought on “SUZA yakabidhiwa rasmi taasisi za Elimu Zanzibar”