RUCU : Awamu ya pili ya Kuomba nafasi za chuo

RUCU : Awamu ya pili ya Kuomba nafasi za chuo

TAARIFA KWA UMMA

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeuntangazia Umma kuwa imefungua maombi ya kuomba chuo kwa awamu ya pili kuanzia tarehe 4 hadi 10 Octoba 2017 ili kuruhusu makundi mbalimbali ya waombaji ambao kwa sababu moja au nyingine hawakuweza kufanya maombi katika awamu ya kwanza:

Sambamba na Tangazo hilo, Chuo Kikuu cha Ruaha kinapenda kuwatangazia umma kuwa nafasi za kuomba katika shahada (degree) mbalimbali bado zinapatikana.

Tembelea Online Admission System kufanya maombi ya kudahiliwa au njoo chuoni kwetu Iringa mjini kufanya maombi yako.

Aidha, uongozi wa chuo unawakumbusha wanafunzi wote waliochaguliwa RUCU pamoja na vyuo vingine wathibitishe kujiunga na RUCU mapema. Ikumbukwe kwamba wale waliochaguliwa vyuo viwili au zaidi wanapaswa kuthibitisha tu kwa simu au email, hawana haja ya kufanya maombi ya udahili kwa mara ya pili.

Kwa wale ambao walikuwa wameshatuma maombi lakini hawakuwa wamepata AVN kutoka NACTE lakini sasa wameshapata, wanapaswa tu kuwasiliana tena na chuo pasipo kutuma tena maombi kwa mara ya pili.

Karibuni sana, Ruaha Catholic University.

See also

International Scholarships for Tanzanians to Study Abroad

HESLB | Higher Education Students Loan Board |

Fisheries Education and Training Agency | FETA |

TCU | Tanzania Commission for Universities |

National Council for Technical Education | NACTE |

Admissions for Universities in Tanzania

Examination Results for Universities in Tanzania

Selected Candidates / Applicants

Necta Examination Results

 

Sponsored Links

Leave a Comment