BODI YAONGEZA SIKU 7 KUTUMA MAOMBI YA MKOPO HADI SEPT. 11, 2017

BODI YAONGEZA SIKU 7 KUTUMA MAOMBI YA MKOPO HADI SEPT. 11, 2017

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu i(HESLB) meongeza muda wa siku saba wa kutuma maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 ili kutoa nafasi kwa waombaji mikopo ambao hawajakamilisha baadhi ya hatua za kujaza fomu za maombi kukamilisha na kutuma.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Bodi ya Mikopo zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji Bw. Abdul-Razaq Badru amesema kuwa maombi ya mikopo yaliyokuwa yafungwe Septemba 4, yataendelea hadi Septemba 11, 2017.

Aidha, Badru amewasisitiza waombaji wa mikopo kuzingatia mwongozo uliotolewa na Bodi unaowataka kuambatanisha nyaraka zote zilizothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamimi (RITA), makamishina wa viapo, mawakili na serikali za mtaa na kuziwasilisha kwenye mtandao wa Bodi.
Maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018, yanayofanyika kwa njia ya mtandao olas.heslb.go.tz  yalifunguliwa Agosti 6, 2017.
Mpaka kufikia Agosti 29, 2017, maombi ya mkopo zaidi ya 50,000 yalikuwa yametumwa Bodi ya Mikopo kwa ajili ya uhakiki na baadaye kupangiwa mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

See also

HESLB | Higher Education Students Loan Board |

Fisheries Education and Training Agency | FETA |

TCU | Tanzania Commission for Universities |

National Council for Technical Education | NACTE |

Admissions for Universities in Tanzania

Examination Results for Universities in Tanzania

Selected Candidates / Applicants

Necta Examination Results

International Scholarships for Tanzanians to Study Abroad

Sponsored Links

2 thoughts on “BODI YAONGEZA SIKU 7 KUTUMA MAOMBI YA MKOPO HADI SEPT. 11, 2017”

  1. I don’t understand when you said we must print again after printing the first and signed it

    Reply
  2. u did da best 2 extent da time but more than that,make sure you work upon all applicants because by so doing the meaning of your extra time will be recognised.

    Reply

Leave a Comment