Kamati ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Wanawake ya BLW ziarani SUZA
Visit Admissions for Universities in Tanzania for More Details on Admissions
Ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Wanawake ya Baraza la Wawakilishi iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Dkt. Mwinyihaji Makame katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) iliyofanyika tarehe 24 Januari, 2017. Lengo la ziara hiyo ni kuangalia utekelezaji wa majukumu ya Serikali yanayofanywa na Wizara mbalimbali. Wakiwa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, ambacho kiko chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali walifanya mazungumzo na Baraza la Chuo chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Said Bakari Jecha. Mheshimiwa Mmanga Mjengo Mjawiri, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali pia alishiriki katika ziara hiyo.
Sponsored Links
1 thought on “Kamati ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Wanawake ya BLW ziarani SUZA”