Kufungwa Rasmi kwa Zoezi la Udahili kwa waombaji wa Shahada ya kwanza kwa mwaka 2016/17 (CAS)

Kufungwa Rasmi kwa Zoezi la Udahili kwa waombaji wa Shahada ya kwanza kwa mwaka 2016/17 (CAS)

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa zoezi la kupokea maombi ya kujiunga na masomo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017 limefungwa rasmi. Orodha ya majina ya waliochaguliwa ilishatangazwa na vyuo husika. Wote waliochaguliwa wanaweza kuona vyuo na programu walizochaguliwa kupitia tovuti ya tume www.tcu.go.tz (view provisional results for 2016/17).

Hivyo Tume inapenda kuwatangazia wote waliodahiliwa na Umma kwa ujumla kwamba:

Mfumo wa pamoja wa udahili (CAS) kwa mwaka wa masomo 2016/17 sasa umefungwa rasmi.

Waombaji wote waliopangiwa vyuo wanatakiwa wawe wamesharipoti kwenye vyuo husika kwa usajili na taratibu nyingine kabla ya muda wa usajili kuisha

Taratibu zote za kuhama chuo au programu zitafanyika vyuoni na kuthibitishwa na Tume. Mwisho wa kupokea maombi ya uhamisho ni tarehe 18 Novemba, 2016 na hakuna maombi yatakayopokelewa baada ya muda huo kuisha.

Imetolewa na

Katibu Mtendaji

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania

15/11/2016

Sponsored Links

Leave a Comment