SEKOMU Diploma and Certificate Admissions 2016 / 2017

SEKOMU Diploma and Certificate Admissions

Sebastian Kolowa Memorial University Diploma and Certificate Applications 2016 / 2017

 

CLINICAL OFFICERS’ TRAINING CENTRE BUMBULI

Telephone: +255 27 2640353

P. O. Box 9, BUMBULI.

Fax: + 255 27 2640360

TANZANIA.

Kumb.Na. COTC/BK/1/2016

Tarehe: 26 Julai 2016

JINA LA MWANAFUNZI: ……………………….

 

ANUANI: ………………………………………………..

 

Yah: MAFUNZO YA KUJIENDELEZA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Napenda kukuarifu kuwa umechaguliwa kujiunga na mafunzo ya Clinical Officer/Assistant Clinical Officer hapa Clinical Officers’ Training Centre (C.O.T.C) Bumbuli. Pongezi!

Mafunzo haya ni ya miaka mitatu (3) kwa Clinical Officer (Ordinary Diploma in Clinical Medicine) na miaka miwili (2) kwa Assistant Clinical Officer (Technician Certificate in Clinical Medicine).

Unatakiwa uripoti Chuoni tarehe 26 Septemba 2016. Endapo utakuwa na maswali, tafadhali piga simu au tuma ujumbe kwa namba zifuatazo: 0787-337872 au 0754-382819.

Kuhusu gharama ya mafunzo, unatakiwa kulipa ada kiasi cha shilingi Millioni Moja, Laki Saba na Elfu Tano tu (TZS. 1,705,000.00) kwa mwaka. Unaweza kulipa ada hii kama ilivyoonyeshwa kwenye utaratibu wa malipo hapo chini. Malipo yote ya Ada yanapaswa kufanywa benki kwa kupitia akaunti ifuatayo: NMB Lushoto, ELCT NED CLINICAL OFFICERS TRAINING CENTRE: A/C NO. 4161300005.

Utaratibu wa malipo ni kama ifuatavyo:

Wakati wa kuripoti, unatakiwa uwe umelipa TZS. 550,000/= kwenye Akaunti (NMB Lushoto, ELCT NED CLINICAL OFFICERS TRAINING CENTRE A/C No. 4161300005).

Ada kwa ajili ya serikali ya wanafunzi ni 18,000/= (SEKOMU-SO A/C No. 4162301220 NMB)

Kiasi kilichobaki kitalipwa kwenye awamu tatu kama ifuatavyo:-

1.Shilingi 380.,000/= kabla ya kufanya mitihani ya kumaliza muhula wa kwanza

2.Shilingi 380,000/= mwanzoni mwa muhula wa pili

3.Shilingi 377,000/= kabla ya kufanya mitihani ya kumaliza muhula wa pili

Malipo yanaweza kufanywa kwenye benki huko uliko.

Mara ufikapo chuoni, utatakiwa kupimwa afya yako hapa Munbuli Hospital.

Wakati wote uwapo chuoni, utatakiwa kutii sheria za nchi na za Chuo. Masuala yote ya mwanafunzi Chuoni yatashughulikiwa na Uongozi wa Chuo. Endapo patakuwa na haja ya suala la mwanafunzi kushughulikiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (Makao Makuu), jambo hilo litatakiwa kuwasilishwa kwanza kwa Mkuu wa Chuo kabla ya kupelekwa Wizarani.

All correspondence should be addressed to the Vice Chancellor

1

Gharama zote za usafiri wa kwenda na kurudi chuoni ni jukumu la mwanafunzi kwa kipindi chote anapokuwa chuoni. Hakikisha unakuwa na fedha za kutosha kwa ajili ya matumizi binafsi kwa kipindi chote utakapokuwa chuoni.

UNATAKIWA KUFIKA CHUONI NA VIFAA VIFUATAVYO:

1.SARE ZA CHUO KWA MWANAMKE:

Magauni mawili (2) meupe ya mikono mifupi na urefu usiopungua sentimita kumi (10 cm) chini ya magoti

Viatu vyeupe, vyeusi au kahawia vyenye visigino vifupi

Makoti mawili meupe ya mikono mirefu, na yawe na urefu usiopungua sentimita kumu (10 cm) chini ya magoti.

2.SARE ZA CHUO KWA MWANAMUME:

Suruali mbili (2) za rangi ya khaki

Mashati mawili rangi nyeupe ya mikono mifupi

Viatu vya ngozi vyeusi au kahawia

Makoti mawili meupe ya mikono mirefu, na yawe na urefu usiopungua sentimenta kumi (10 cm) chini ya magoti.

Ni muhimu kuhakikisha kwamba mavazi yanatunza heshima yako na ya Chuo, hivyo mavazi yasibane wala kuangaza kwa namna inavyoonyesha maumbile ya mwili. Unatakiwa kuvaa nguo za heshima wakati wote unapokuwa chuoni.

NB: ENDAPO HUTAFANIKIWA KUTAFUTA VIFAA HIVI kabla ya kuripoti chuoni, unaweza kuvitafuta baada ya kuripoti chuoni.

A.AINISHO LA ADA NA GHARAMA NYINGINE:

S/N

ITEM

COST

1.

Tuition fee

1,090,000.00

2.

NACTE Examination fee

150,000.00

3.

Identity card

12,000.00

4.

Practical procedure book

50,000.00

5.

Practicum guide book

30,000.00

6.

Caution money

10,000.00

7.

NACTE Students Registration fee

15,000.00

8.

Computer Facilities & Services

60,000.00

9.

Student Activity fee (to be paid to SEKOMU-SO A/C

18,000.00

 

No. 4162301220 NMB)

 

10.

Quality Assurance fee

20,000.00

11.

Internal Examinations’ fee

100,000.00

12.

Field work

150,000.00

Total Amount

1,705,000.00

*Endapo tayari unayo bima ya Afya basi utahitajika kufika na kitambulisho cha bima au kulipia shilingi 50,400/= kwa mwaka.

PIA UNATAKIWA KUJA NA VIFAA VIFUATAVYO:

Nguo za michezo rangi ya buluu au nyeusi

Ndoo ya maji aina ya “Plastic”

Picha nne (4) passport size kwa ajili ya kumbukumbu

Cheti halisi (original) cha kuhitimu kidato cha Nne. Ikiwa vyeti vitakuwa havijatoka unaporipoti Chuoni, utatakiwa kufuatilia wakati wa likizo.

Vitabu katika kozi husika inapowezekana

Vifaa vya kuandikia kwa mfano madaftari, kalamu, rula n.k.

Mwavuli au koti la mvua na buti za mvua

Shuka 4, mto 1, blanketi 1, chandarua 1, taulo na foronya

2

Blood pressure machine

Stethoscope

NB: Endapo hutafanikiwa kupata vifaa kabla ya kuripoti k.m. blood pressure machine, stethoscope, vitabu, n.k., uongozi wa Chuo utaweka utaratibu wa kukusaidia kuvipata lakini utapaswa kuvilipia.

B.MALAZI

Gharama ya mahali pa kuishi ni ya mwanafunzi

Utapewa mahali pa kuishi ndani eneo la Chuo. Gharama kwa muhula ni shilingi laki mbili tu (TShs.200,000/=) na kwa mwaka wote wa masomo (miezi 10) ni shilingi laki nne tu (Tsh. 400,000/=).

Fedha hizo zaweza kulipwa kwa mara moja au awamu mbili kupitia akaunti ya chuo (NMB Lushoto, ELCT NED CLINICAL OFFICERS TRAINING CENTRE A/C No. 4161300005). Malipo yanaweza kufanywa kwenye benki huko uliko.

Malazi yanapatikana pia nje ya eneo la Chuo.

C.CHAKULA

Chakula kwa kipindi chote cha mafunzo ni gharama ya mwanafunzi

Chakula kitapatikana katika mgahawa wa chuo kwa fedha taslimu. Unashauriwa kuandaa kiasi kisichopungua Tshs. 90,000/= kwa mwezi kwa ajili ya chakula.

D.

MAELEKEZO KUHUSU MAHALI CHUO KILIPO

Chuo kipo Bumbuli katika Halmashauri ya Bumbuli, Wilaya ya Lushoto, Mkoa wa Tanga.

Ukitokea upande wa kaskazini (k.m. Arusha/Moshi/Tanga) au upande wa mashariki (k.m. Dar es Salaam) panda basi liendalo moja kwa moja Bumbuli.

Endapo hutapata basi liendalo moja kwa moja Bumbuli, waweza kupanda mabasi yaendayo Mombo au Soni kisha upande mabasi yaendayo Bumbuli.

Nakutakia kila la kheri katika mafunzo yako.

Dr. Wilson William

NAIBU MAKAMU MKUU WA CHUO (TAALUMA)

 

About SEKOMU

SEKOMU Courses Offered

SEKOMU Entry Requirements

SEKOMU Application Forms

SEKOMU Prospectus

SEKOMU Fees Structure

SEKOMU Contact Details

SEKOMU Joining Instructions

SEKOMU Basic Tech Certificate in Community Health Admissions

SEKOMU Registration

SEKOMU Accommodation

SEKOMU Library

SEKOMU Grading System

 

Sponsored Links

Leave a Comment