TUMA MAOMBI YA MIKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018
MNATANGAZIWA KUWA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU IMEANZA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018. MCHAKATO WA
MAOMBI UMEANZA TAREHE 06 AGOSTI, 2017 HADI TAREHE 4 SEPTEMBA, 2017.
KWA YEYOTE MWENYE NIA YA KUOMBA MKOPO UTARATIBU NI KAMA IFUATAVYO:
1.ZINGATIA MIONGOZO, VIGEZO NA HATUA ZOTE ZA KUOMBA MIKOPO KAMA ZINAVYO AINISHWA KATIKA TOVUTI YA BODI YA MIKOPO. BOFYA HAPA: http://www.heslb.go.tz
2.BAADA YA KUKAMILISHA MCHAKATO WOTE (YAANI UMESHATUMA MAOMBI YAKO BODI) UTAHITAJIKA KUTOA TAARIFA CHUONI KUPITIA KWA WAZIRI WA MIKOPO. TUTAHITAJI TAARIFA ZIFUATAZO:
I.NAMBARI YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (MFANO: S0329.0001.2016)
II.JINA KAMILI III. JINSIA
IV. NAMBARI YAKO YA USAJILI CHUONI (MFANO: TUMA/BAED/16/072976)
V.PROGRAMU UNAYOSOMA (MFANO: BAED)
VI. MWAKA WA MASOMO ULIOPO KWA SASA (MFANO: MWAKA 1 AU 2) VII. MWAKA WA MASOMO UNAOTARAJIA KUINGIA (MFANO: MWAKA 2 AU 3) VIII. BENKI UNAYOTUMIA (MFANO: CRDB)
IX. NAMBARI YA AKAUNTI YA BENKI YAKO (MFANO: 0152407397500)
3.TUTAPOKEA TAARIFA HIZI HADI TAREHE 11 SEPTEMBA, 2017. BAADA YA HAPO CHUO KITAANDIKA NA KUTUMA BODI, BARUA MOJA YA PAMOJA, KUWATAMBULISHA WANAFUNZI WETU WOTE WALIOOMBA MIKOPO.
DAWATI LA MIKOPO – TUMA
AUGUST 9, 2017
See also