MASHINDANO YA USHAIRI KUMBUKIZI YA KIFO CHA BABA WA TAIFA, MWALIMU NYERERE KWA SHULE ZA SEKONDARI
TAARIFA KWA UMMA
MASHINDANO YA USHAIRI KUMBUKIZI YA KIFO CHA BABA WA
TAIFA, MWALIMU NYERERE KWA SHULE ZA SEKONDARI
14 OKTOBA, 2016
Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Julius Nyerere-Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimeandaa mashindano ya ushairi kwa shule za sekondari zenye klabu za Jukwaa la Fikra za Mwalimu Nyerere zilizoko jijini Dar es Salaam na Bukoba.
Mashindano haya yatafanyika mnamo tarehe 14 Oktoba, 2016 kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana, ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CKD).
Mada kuu ya mashindano ni “MWALIMU JULIUS NYERERE NA
MAENDELEO YA WATU MASHINANI�?
Zawadi zitatolewa kwa washindi.
WOTE MNAKARIBISHWA
Sponsored Links