SEKOMU Joining Instructions for 2016 / 2017
Yah: MAFUNZO YA KUJIENDELEZA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017
Napenda kukuarifu kuwa umechaguliwa kujiunga na mafunzo ya Clinical Officer/Assistant Clinical Officer hapa Clinical Officers’ Training Centre (C.O.T.C) Bumbuli. Pongezi!
Mafunzo haya ni ya miaka mitatu (3) kwa Clinical Officer (Ordinary Diploma in Clinical Medicine) na miaka miwili (2) kwa Assistant Clinical Officer (Technician Certificate in Clinical Medicine).
Unatakiwa uripoti Chuoni tarehe 26 Septemba 2016. Endapo utakuwa na maswali, tafadhali piga simu au tuma ujumbe kwa namba zifuatazo: 0787-337872 au 0754-382819.
Kuhusu gharama ya mafunzo, unatakiwa kulipa ada kiasi cha shilingi Millioni Moja, Laki Saba na Elfu Tano tu (TZS. 1,705,000.00) kwa mwaka. Unaweza kulipa ada hii kama ilivyoonyeshwa kwenye utaratibu wa malipo hapo chini. Malipo yote ya Ada yanapaswa kufanywa benki kwa kupitia akaunti ifuatayo: NMB Lushoto, ELCT NED CLINICAL OFFICERS TRAINING CENTRE: A/C NO. 4161300005.
Utaratibu wa malipo ni kama ifuatavyo:
∙Wakati wa kuripoti, unatakiwa uwe umelipa TZS. 550,000/= kwenye Akaunti (NMB Lushoto, ELCT NED CLINICAL OFFICERS TRAINING CENTRE A/C No. 4161300005).
∙Ada kwa ajili ya serikali ya wanafunzi ni 18,000/= (SEKOMU-SO A/C No. 4162301220 NMB)
∙Kiasi kilichobaki kitalipwa kwenye awamu tatu kama ifuatavyo:-
1.Shilingi 380.,000/= kabla ya kufanya mitihani ya kumaliza muhula wa kwanza
2.Shilingi 380,000/= mwanzoni mwa muhula wa pili
3.Shilingi 377,000/= kabla ya kufanya mitihani ya kumaliza muhula wa pili
Malipo yanaweza kufanywa kwenye benki huko uliko.
Mara ufikapo chuoni, utatakiwa kupimwa afya yako hapa Munbuli Hospital.
Wakati wote uwapo chuoni, utatakiwa kutii sheria za nchi na za Chuo. Masuala yote ya mwanafunzi Chuoni yatashughulikiwa na Uongozi wa Chuo. Endapo patakuwa na haja ya suala la mwanafunzi kushughulikiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (Makao Makuu), jambo hilo litatakiwa kuwasilishwa kwanza kwa Mkuu wa Chuo kabla ya kupelekwa Wizarani.
All correspondence should be addressed to the Vice Chancellor |
1 |
Gharama zote za usafiri wa kwenda na kurudi chuoni ni jukumu la mwanafunzi kwa kipindi chote anapokuwa chuoni. Hakikisha unakuwa na fedha za kutosha kwa ajili ya matumizi binafsi kwa kipindi chote utakapokuwa chuoni.
UNATAKIWA KUFIKA CHUONI NA VIFAA VIFUATAVYO:
1.SARE ZA CHUO KWA MWANAMKE:
∙Magauni mawili (2) meupe ya mikono mifupi na urefu usiopungua sentimita kumi (10 cm) chini ya magoti
∙Viatu vyeupe, vyeusi au kahawia vyenye visigino vifupi
∙Makoti mawili meupe ya mikono mirefu, na yawe na urefu usiopungua sentimita kumu (10 cm) chini ya magoti.
2.SARE ZA CHUO KWA MWANAMUME:
∙Suruali mbili (2) za rangi ya khaki
∙Mashati mawili rangi nyeupe ya mikono mifupi
∙Viatu vya ngozi vyeusi au kahawia
∙Makoti mawili meupe ya mikono mirefu, na yawe na urefu usiopungua sentimenta kumi (10 cm) chini ya magoti.
Ni muhimu kuhakikisha kwamba mavazi yanatunza heshima yako na ya Chuo, hivyo mavazi yasibane wala kuangaza kwa namna inavyoonyesha maumbile ya mwili. Unatakiwa kuvaa nguo za heshima wakati wote unapokuwa chuoni.
NB: ENDAPO HUTAFANIKIWA KUTAFUTA VIFAA HIVI kabla ya kuripoti chuoni, unaweza kuvitafuta baada ya kuripoti chuoni.
A.AINISHO LA ADA NA GHARAMA NYINGINE:
S/N |
ITEM |
COST |
1. |
Tuition fee |
1,090,000.00 |
2. |
NACTE Examination fee |
150,000.00 |
3. |
Identity card |
12,000.00 |
4. |
Practical procedure book |
50,000.00 |
5. |
Practicum guide book |
30,000.00 |
6. |
Caution money |
10,000.00 |
7. |
NACTE Students Registration fee |
15,000.00 |
8. |
Computer Facilities & Services |
60,000.00 |
9. |
Student Activity fee (to be paid to SEKOMU-SO A/C |
18,000.00 |
|
No. 4162301220 NMB) |
|
10. |
Quality Assurance fee |
20,000.00 |
11. |
Internal Examinations’ fee |
100,000.00 |
12. |
Field work |
150,000.00 |
Total Amount |
1,705,000.00 |
*Endapo tayari unayo bima ya Afya basi utahitajika kufika na kitambulisho cha bima au kulipia shilingi 50,400/= kwa mwaka.
PIA UNATAKIWA KUJA NA VIFAA VIFUATAVYO:
∙Nguo za michezo rangi ya buluu au nyeusi
∙Ndoo ya maji aina ya “Plastic”
∙Picha nne (4) passport size kwa ajili ya kumbukumbu
∙Cheti halisi (original) cha kuhitimu kidato cha Nne. Ikiwa vyeti vitakuwa havijatoka unaporipoti Chuoni, utatakiwa kufuatilia wakati wa likizo.
∙Vitabu katika kozi husika inapowezekana
∙Vifaa vya kuandikia kwa mfano madaftari, kalamu, rula n.k.
∙Mwavuli au koti la mvua na buti za mvua
∙Shuka 4, mto 1, blanketi 1, chandarua 1, taulo na foronya
2
∙Blood pressure machine
∙Stethoscope
∙NB: Endapo hutafanikiwa kupata vifaa kabla ya kuripoti k.m. blood pressure machine, stethoscope, vitabu, n.k., uongozi wa Chuo utaweka utaratibu wa kukusaidia kuvipata lakini utapaswa kuvilipia.
B.MALAZI
∙Gharama ya mahali pa kuishi ni ya mwanafunzi
∙Utapewa mahali pa kuishi ndani eneo la Chuo. Gharama kwa muhula ni shilingi laki mbili tu (TShs.200,000/=) na kwa mwaka wote wa masomo (miezi 10) ni shilingi laki nne tu (Tsh. 400,000/=).
∙Fedha hizo zaweza kulipwa kwa mara moja au awamu mbili kupitia akaunti ya chuo (NMB Lushoto, ELCT NED CLINICAL OFFICERS TRAINING CENTRE A/C No. 4161300005). Malipo yanaweza kufanywa kwenye benki huko uliko.
∙Malazi yanapatikana pia nje ya eneo la Chuo.
C.CHAKULA
∙Chakula kwa kipindi chote cha mafunzo ni gharama ya mwanafunzi
∙Chakula kitapatikana katika mgahawa wa chuo kwa fedha taslimu. Unashauriwa kuandaa kiasi kisichopungua Tshs. 90,000/= kwa mwezi kwa ajili ya chakula.
D. |
MAELEKEZO KUHUSU MAHALI CHUO KILIPO |
∙Chuo kipo Bumbuli katika Halmashauri ya Bumbuli, Wilaya ya Lushoto, Mkoa wa Tanga.
∙Ukitokea upande wa kaskazini (k.m. Arusha/Moshi/Tanga) au upande wa mashariki (k.m. Dar es Salaam) panda basi liendalo moja kwa moja Bumbuli.
∙Endapo hutapata basi liendalo moja kwa moja Bumbuli, waweza kupanda mabasi yaendayo Mombo au Soni kisha upande mabasi yaendayo Bumbuli.
Nakutakia kila la kheri katika mafunzo yako.
Dr. Wilson William
NAIBU MAKAMU MKUU WA CHUO (TAALUMA)