St. Joseph University In Tanzania Certificate Courses For Form Five
UKWELI KUHUSU KOZI YA SHAHADA YA MIAKA MITANO YA CHUO CHA
MTAKATIFU JOSEPH – KAMPASI YA ARUSHA
1. UTANGULIZI
Chuo Cha Mtakatifu Joseph Kampasi Ya Arusha kilianzishwa mwaka 2013, kikiwa na lengo la kukabiliana na upungu wa walimu wa sayansi nchini. Kampasi hii ilianza kwa program mbili za ualimu ambayo moja ilikuwa ikitolewa kwa kipindi cha miaka 3 na nyingine kwa kipindi cha miaka 5. Program ya miaka mitano ilikuwa ni program maalum ikiwa na lengo la kuimarisha na kuongeza idadi ya walimu wa sayansi na hesabu nchini. ufundishaji wa program ya miaka mitatu iliwahusisha wanafunzi waliomaliza kidato cha sita (VI) na wenye Diploma, program ya miaka mitano iliwahusisha wanafunzi wa kidato cha nne (IV).
2. TATIZO
Program Maalum ya miaka mitano ilianzishwa ili kuweza kuziba pengo linalotokea pindi wanafunzi wanapomaliza kidato cha pili (FORM II) na wanapomaliza kidato cha nne (FORM IV). Pengo hili linatokea kwasababu ni katika kipindi hicho ndio wanafunzi huchagua michepuo ya masomo na kuendelea nayo katika masomo yao ya mbeleni
Kutokana na takwimu za Wizara Ya Elimu Na Ufundi Tanzania (2013) ilionekana kuwa Tanzania kuna upungufu wa walimu wa sayansi takribani 26,998. Tatizo linaaza kuonekana wakati wa kuchagua mchepuo wa sayansi au mingine, ambapo imeonekana takribani asilimia kumi(10%) ya wanafunzi huchagua michepuo ya sayansi na asilimia tisini (90%) huchagua michepuo ya sanaa. Na hii husababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo uhaba wa walimu wa kuwafundisha masomo ya sayansi, ukosefu wa maabara, kukosekana kwa mvuto katika fani ya ualimu n.k sababu hizi zimechangia hata idadi ya wanaojiunga na vyuo vikuu kuzidi kupungua.
1
TAKWIMU A
Idadi Ya Ufaulu Wa Wanafunzi Kutoka Shule Za Msingi Mpaka Sekondari
VIPENGELE |
WANAODAHILIWA |
UFAULU |
|
|
|
ELIMU YA MSINGI |
865,534 |
265,873 |
|
|
|
SEKONDARI (CSEE) |
|
159,747 |
|
|
|
SEKONDARI (ACSE) |
|
40,785 |
|
|
|
UNIVERSITIES |
86000 |
|
|
|
|
TAKWIMU B
|
|
Total Number of Teachers |
65,513 * |
Total Number of Qualified |
< 10, 000* |
|
Science Teachers |
||
|
||
|
|
|
|
Courtesy BEST |
8
Udahili wa walimu katika vyuo vikuu
Kutokana na takwimu hizi SJUIT ikishirikana na wadau wengine wa elimu ilikaa chini na kuangalia jinsi gani ya kutatua tatizo. Katika utafiti wake na kwa kupitia kuangalia nchi zingine duniani ziliwezaje kutatua tatizo, SJUIT iliweza kuona njia ambazo zingeweza kupunguza /kuondoa tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi Tanzania kwa kufanya yafuatayo:
Kuogeza idadi ya shule za sayansi
Kuongeza idadi ya walimu wa sayansi
Kutoa ufadhili/mikopo kwa shule za sayansi na wanafunzi wa sayansi
Kuwawezesha wanafunzi wa kidato cha pili, cha tatu na cha nne
Kuongeza idadi ya vitabu vya sayansi
2
Kutenegeneza program mpya kulingana na takwimu zinavyosema
Kuongeza wanafunzi wa sayansi katika ngazi zote
Kuanzisha mitaala mipya kama 70;30 ( mfano Ethiopia wanatumia hii)
Katika njia zote zilizo orodheshwa hapo juu, St Joseph University In Tanzania iliona njia ambayo ingeweza kuondoa tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi katika shule za sekondari ni kwa kutengeneza mtaala kama ulivyoainishwa hapa chini:
3. SHAHADA YA SAYANSI YA UALIMU YA MIAKA 5
Chuo cha Mtakatifu Yosefu kiliona tatizo, na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wa elimu, chuo kilikuja na program maalum ya miaka mitano katika ualimu wa sayansi. Programu hii ilidadavuliwa katika semina iliyoandaliwa Whitesands na ilipatwa kusikiliza na wadau mbalimbali wa elimu, Tume ya vyuo vikuu ikiwa moja wapo.
Tarehe 9/7/2013 Chuo Cha Mtakatifu Yosefu kilipata kibali kutoka Tume Ya Vyuo Vikuu kuanzisha Programu hii maalum ya miaka mitano katika mwaka wa masomo 2013/2014. Na kibali hicho kilionyesha mwanafunzi atabobea katika somo la sayansi kama inavyoonyesha hapa chini.
∙Shahada ya ualimu wa sayansi ( fizikia)
∙Shahada ya ualimu wa sayansi ( kemia)
∙Shahada ya ualimu wa sayansi (mathematics)
∙Shahada ya ya ualimu wa sayansi (biolojia)
∙Shahada ya ualimu wa sayansi (sayansi ya kompyuta)
Program hii ilitolewa katika kampasi za Songea (SJUCAST &SJUCIT), and katika kampasi kuu iliyopo Luguruni, Dar es Salaam. Kampasi ya Arusha ilipata kibali kutoka Tume Ya Vyuo Vikuu cha kutoa hizi program mwaka 2013.
3.1 Sifa za muombaji kama zilivyoainishwa katika Mtaala;
∙Cheti cha kidato cha nne , awe amefaulu michepuo ya sayansi sio chini ya masomo manne yakiwemo ya sayansi
3
∙Cheti cha kidato cha nne , awe amefaulu siyo chini ya masomo manne yakiwemo Hesabu na Biolojia
∙Mtu mwenye mchepuo wa sanaa aliyefaulu biolojia na hesabu ataruhusiwa kuomba kozi ya ualimu wa sayansi katika hesabu /biolojia
Wanafunzi wote wa kozi ya miaka 5 waliodailiwa chuoni wana sifa zilizoanishwa na kupitishwa na Tume Ya Vyuo Vikuu kama inavyoonekana hapo juu. Hakuna mwanafunzi aliyedailiwa chini ya kiwango hicho. Na kwakutumia sifa hizo chuo kilidahili wanafunzi kwa mara ya kwanza mwaka 2013 mwezi wa kumi (October) takribani wanafunzi 102 walidahiliwa. Udahili wa pili ulikuwa mwaka 2014 June, chuo kilipata wanafunzi 199, udahili wa tatu ulikuwa mwaka 2014 Septemba chuo kilipata wanafunzi 155. Kati ya hao wanafunzi wote, wanafunzi 396, walikuwa wananufaika na mkopo kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu.
3.2Kozi Maalum ya miaka mitano kama jibu la upungufu wa walimu wa sayansi nchini
Kama inavyoonekana katika jedwali la picha hapo juu (SJUIT PLAN) moja ya njia zilizotajwa katika kuondoa tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi, SJUIT iliona njia moja wapo ni kuandaa madarasa ya ziada ili waweze kuwafundisha wanafunzi wa kidato cha tatu na cha nne katika masomo ya hesabu na sayansi
Njia nyingine ya kutatua tatizo ilikuwa; kwakuwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne na kupata Division IV ni wachache , na kundi hili la watu mara nyingi hupotea kwasababu moja au nyingine SJUIT iliona inaweza kuliokoa kundi hili nakutafuta jinsi ya kuwaendeleza kimasomo huku ikiwajengea msingi imara wa masomo ya sayansi, kwakuwadahili katika Program maalum ya kozi ya miaka 5 ya elimu katika sayansi (5 year intergrated B.Sc.Ed).
Kwa miaka miwili ya masomo mwanafunzi huyu wa miaka 5 atafundishwa masomo ya sayansi ili kumjengea msingi imara , masomo haya ni fizikia , kemia, biolojia hesabu na sayansi ya kompyuta. Lengo la kumfundisha haya masomo katika program hii ni kumjengea uwezo wa kuweza kuyafundisha huko mbele, lakini pia katika miaka miwili
4
hii mwanafunzi huyu anakuwa hana tofauti na yule aliesoma kidato cha tano na cha sita. Kwa sababu chuo kina waalimu waliobobea katika maswala ya sayansi, mwanafunzi atafundishwa masomo haya katika njia rahisi, na itakayo muwezesha kuona kuwa masomo haya si magumu.
|
|
BACHELOR |
• EXIT WITH BACHELOR IN SCIENCE EDU |
|
|
H. DIPLOMA |
• NO EXIT |
O. DIPLOMA |
• EXIT @ DIPLOMA |
CERTIFICATE |
• SEMESTER |
|
• TRIMESTER (3 TERMS) |
17
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Programme |
Entry Level |
Entry Qualifications |
|
|
|
s |
|
|
|
|
|
|
|
Certificate of Secondary Education (Form IV) with a minimum |
|
|
|
|
|
of three passes or equivalent recognized by NECTA. |
|
|
|
5 years – |
|
Mathematics with Science combination in CSEE can apply |
|
|
|
Bachelor of |
Form IV or |
for the courses B. Sc. Ed. in Mathematics/ Physics/ Chemistry/ |
|
|
|
Science in |
Equivalent |
Biology/Computer Science. |
|
|
|
Education |
|
Mathematics with Arts combination in CSEE can apply for |
|
|
|
|
|
the courses B. Sc. Ed. in Mathematics/ Biology/ Computer |
|
|
|
|
|
Science |
|
|
|
|
|
Advanced Certificate of Secondary Education (Form VI) with |
|
|
|
|
|
two principal passes in any of the following Combinations: |
|
|
|
3 years – |
|
PCM, PCB, PGM, CBG, CBN and CBA (P-Physics, C-Chemistry, |
|
|
|
Bachelor of |
FormVI or |
M-Mathematics, B-Biology, N-Nutrition Science, A- |
|
|
|
Science in |
Equivalent |
Agricultural Science and G-Geography) or equivalent. If the |
|
|
|
Education |
|
principal passes do not include the selected subject of study, |
|
|
|
|
|
the candidate must have subsidiary pass in that subject at A |
|
|
|
|
|
level or credit pass at ‘O’ level. |
18 |
|
Kwa mantiki hiyo ukiangalia jedwali hapo juu (5 year intergrated path) utagundua kuwa kimsingi hii ni kozi ya elimu tofauti na ile ya miaka mitatu inayowachukua wanafunzi wa kidato cha sita. Utofauti wake uko katika sehemu zifuatazo:
1.Kwanza mwanafunzi anaeingia hapa ni aliemaliza kidato cha nne
2.Pili mwanafunzi huyu katika miaka 5 ya kusoma , miaka yake miwili ya kwanza ni sawasawa na kidato cha tano na cha sita , tofauti ni kuwa yuko chuoni na katika mazingira yaliyoboreshwa zaidi kuanzia walimu, maabara n.k
3.Tatu kozi hii inamruhusu mwanafunzi kuishia mwaka wa pili ambapo atatoka na cheti (certificate in proficiency science) ambayo inamruhusu kwenda kusoma kozi ingine yoyote ya science (alama za ufaulu kuzingatiwa) atakayoipenda ingawa serikali ya awamu ya nne iliondoa hiki kipengele.
4.Mwanafunzi aliefaulu kwa miaka hiyo miwili ya mwanzo huruhusiwa
kuendelea na mwaka wa tatu, ambao ndo huwa wanaungana na wale waliomaliza kidato cha sita na mwanafunzi anapoanza kusoma shahada yake ya kwanza katika elimu. Kama mwanafunzi huyu ataamua kuishia mwaka wa tatu atatoka na diploma ya ualimu katika masomo ya sayansi
5
Mwaka wanne (4) mwanafunzi haruusiwi kutoka (exit), na wanaomaliza mwaka wa tano ndo anakuwa ameweza kufanikiwa kupata shahada yake ya kwanza katika elimu ya sayansi (bachelor in science education)
Kuishia ngazi moja wapo (Cheti, Stashahada au Shahada) ni uamuzi wa mwanafunzi hasa ikiwa alama zake za ufaulu zinamruhusu kuendelea. Na katika kipindi chote tangu kuanzishwa kwa program hii hakuna mwanafunzi alieishia katika ngazi ya cheti wala stashahada.
Kwa maelezo haya uongozi wa chuo unapenda kuutaarifu umma na wadau wa elimu kuwa, program hii ya shahada ya miaka mitano ilipitishwa na tume ya vyuo vikuu kwajili ya wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na sio kama program za kawaida za miaka mitatu kwaajili ya wanafunzi waliomaliza kidato cha sita.
Katika kipindi chote cha udahili wanafunzi wote waliodahiliwa wanasifa kama ilivyopitishwa na tume ya vyuo vikuu.
Imetolewa na
Makamu mkuu wa chuo cha mtakatifu Yoseph- Tanzania
P.O.BOX 11007
Luguruni, Kibamba
Dar es Salaam.
About St. Joseph University In Tanzania
St. Joseph University In Tanzania Courses
St. Joseph University In Tanzania Application forms
St. Joseph University In Tanzania General Instructions
St. Joseph University In Tanzania Contact Details
St. Joseph University In Tanzania Bank Account Details
St. Joseph University In Tanzania Fees Structure
St. Joseph University In Tanzania Prospectus
St. Joseph University In Tanzania Scholarship