TUMA TAARIFA KWA UMMA-UDAHILI AWAMU YA TATU
TAARIFA KWA UMMA
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa Awamu ya Pili ya Udahili wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na masomo ya shahada za awali ulimalizika tarehe 10 Oktoba 2017. Kutokana na waombaji wengi kutochaguliwa kwa sababu mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa Awamu ya Tatu kuanzia tarehe 16 hadi 18 Oktoba 2017. Tume inapenda kusisitiza yafuatayo:
a)Awamu hii itawahusu waombaji waliokosa nafasi kwenye Awamu ya Kwanza na ya Pili kutokana na ushindani au kukosa sifa katika programu walizoomba;
b)Waombaji waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja; wanatakiwa kuamua mara moja kwa kuchagua chuo kimoja tu na hatimaye kukiarifu chuo husika;
c)Awamu hii haitawahusu waombaji wapya (ambao hawajawahi kutuma maombi katika awamu mbili zilizopita);
d)Waombaji ambao hawatathibitisha uchaguzi wao au kujithibitisha zaidi ya chuo kimoja hawatatambuliwa na Tume katika udahili wa mwaka 2017/18
e)Waombaji kuwasiliana moja kwa moja na mara kwa mara na vyuo husika kwa masuala yote yanayohusiana na zoezi la udahili badala ya kuja TCU.
f)Waombaji wote kutembelea Tovuti za vyuo ili kufahamu hatima ya maombi yao. Aidha, Tume inapenda kusisitiza kuwa utaratibu wa kutuma maombi na kuthibitisha ni ule ule uliotumika katika awamu mbili zilizopita za Udahili.
Imetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania 16 Oktoba 2017
See also
HESLB | Higher Education Students Loan Board |
Fisheries Education and Training Agency | FETA |
TCU | Tanzania Commission for Universities |
National Council for Technical Education | NACTE |
Admissions for Universities in Tanzania
Examination Results for Universities in Tanzania
Selected Candidates / Applicants
Necta Examination Results
International Scholarships for Tanzanians to Study Abroad