Mdahalo wa maadhimisho ya kumbukumbu ya 17 ya Mwalimu Nyerere.

Mdahalo wa maadhimisho ya kumbukumbu ya 17 ya Mwalimu Nyerere.

Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kupitia Chuo cha Sanyansi za Jamii na Hyumanitia (College of Social Sciences and Humanities) kwa heshima na taadhima kinapenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha wananchi na taasisi mbalimbali kwenye Mdahalo wa kuadhimisha kumbukumbu ya 17 ya Mwalimu Nyerere.

Mada itakayojadiliwa ni: Kuelekea Tanzania ya Viwanda: Nini Nafasi ya Sekta ya Kilimo? Matarajio na Changamoto kwa Serikali ya Awamu ya Tano.

Mchokoza mada katika maadhimisho hayo ni Mchumi Mahiri Prof Honest Ngowi.

Mdahalo utafanyika siku ya Tarehe 13 Oktoba, 2016 kuanzia saa 3.30  asubuhi hadi saa 9.30 mchana katika ukumbi wa Nelson Mandela Freedom Square, Kampasi ya Solomon Mahlangu, Mazimbu Morogoro.

 

Sponsored Links

Leave a Comment