Mbeya University Tangazo la Zabuni Ya Kuendesha Biashara Ya Kuuza Chakula na Vinywaji

Mbeya University Tangazo la Zabuni Ya Kuendesha Biashara Ya Kuuza Chakula na Vinywaji

TANGAZO

YAH: ZABUNI YA KUENDESHA BIASHARA YA KUUZA CHAKULA NA VINYWAJI(CATERING SERVICES) KATIKA JENGO LILILOPO NDANI AYA ENEO LA CHUO.

KOTESHENI NAMBA:

1. PA/047/2017/2018/T/01 KUKODISHA JENGO LA MIST SOCIAL CLUB.

2. PA/047/2017/2018/T/02, KUKODISHA CHUMBA CHA MAMA LISHE/BABALISHE NO 1 CHENYE UKUBWA WA MITA ZA MRABA132.

3. PA/047/2017/2018/T/03 KUKODISHA CHUMBA CHA MAMA LISHE/BABALISHE NO 2 CHENYE UKUBWA WA MITA ZA MRABA 99.

1.Chuo Kikuu cha Sayansi na Tekinolojia Mbeya kinatangaza zabuni ya kuendesha biashara ya kuuza chakula na vinywaji kwenye jengo lililopo ndani ya Chuo.

2.Kotesheni hii ina mabunda (lots) matatu, Bunda namba moja ni Kutoa huduma ya chakula na vinywaji ndani ya Mist Social Club, bunda namba pili ni Kutoa huduma ya chakula na vinywaji ndani ya chumba chenye mita za mraba 132 na bunda namba tatu ni Kutoa huduma ya chakula na vinywaji ndani ya chumba chenye mita za mraba 99. Unaweza kuomba mojawapo ya kotesheni au kotesheni zote tatu .

3.Chuo Kikuu cha Sayansi na Tekinolojia Mbeya kinawakaribisha wazabuni waliosajiriwa na Wakala wa Huduma wa Ununuzi Serikalini (GPSA) kwa mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kutoa huduma ya chakula na vinywaji (Catering services).

4.Mwombaji anaweza kuja kulikagua jengo husika siku ya Jumanne tarehe 2/09/2017 kuanzia saa nne asubuhi.

5.Fomu ya Kotesheni zinapatikana ofisi ya manunuzi(PMU) iliyopo chuoni saa za kazi kuanzia saa 07:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri baada ya kulipia kiasi cha shilingi elfu kumi tu (10,000/=) kwa kila kotesheni kiasi hicho kipelekwe NBC – MUST Mekazi Shop account namba 016101002687 na kuonyesha risiti iliyolipiwa kuanzia siku ya jumatatu hadi ijumaa isipokuwa siku za sikukuu.

6.Fomu zote ziwasilishwe zikiwa zimejazwa vizuri na zimefungwa kwenye bahasha (sealed) na ziambatanishwe na kiapo cha zabuni (Tender Securing Declaration) kwa katibu wa zabuni, Chuo Kikuu cha Sayansi na Tekinolojia Mbeya, P.O Box 131, Mbeya.

7.Mwisho wa kupokea ni tarehe 11/09/2017 saa 05:00 asubuhi siku ya Jumatatu na itafunguliwa mbele ya wazabuni watakaokuwepo siku hiyo katika ukumbi wa Nyerere ulioko ndani ya chuo cha sayansi na Teknolojia Mbeya eneo la Iyunga saa 05:30 asubuhi siku ya Jumatatu tarehe 11/09/2017.

8.Fomu zitakazotolewa baada ya tarehe tajwa hapo juu, au fomu zitakazocheleweshwa hazitapokelewa.

MAKAMU CHUO,

CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKINOLOJIA MBEYA,

S.L.P 131,

MBEYA.

See also

HESLB | Higher Education Students Loan Board |

Fisheries Education and Training Agency | FETA |

TCU | Tanzania Commission for Universities |

National Council for Technical Education | NACTE |

Admissions for Universities in Tanzania

Examination Results for Universities in Tanzania

Selected Candidates / Applicants

Necta Examination Results

International Scholarships for Tanzanians to Study Abroad

Sponsored Links

Leave a Comment